Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly  (wa katikati mwenye Tai ya rangi ya chungwa)  akiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa na  ujumbe kutoka Tanzania( hawapo kwenye picha)mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile wakiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile  na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akitoa ufafanuzi na majibu kwaswali aliloulizwa na Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  wakijadiliana juu ya ku kubaliana kuto kukubaliana kwa baadhi ya sheria za (IMF) na Bw. Nikoloz Gigineishvili ambaye ni Mchimi  mwandamizi wa Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile walipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose ofisini kwake wakiwa mjini Washington DC.Walio ambatana na Mhe. Waziri  kutoka kushoto ni Bw. Beda Shallanda Kamishina wa Sera,Bw.Ngosha Said Magonya Kamishina wa Fedha za nje na Bw. John Cheyo Kamishina wa Bajeti na wa pembeni ni mfanyakazi wa Benki ya Dunia.
 
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose ofisini kwake mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose wakiagana mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile , Bw. Beda Shallanda Kamishina wa Sera na Bw. Paul  Mwafongo ambaye ni Afisa katika ubalozi wa Tanzania na kutoka kushoto ni Bw.Ngosha Said Magonya Kamishina wa Fedha za nje Bw. John Cheyo Kamishina wa Bajeti na wa pembeni ni mfanyakazi wa Benki ya Dunia.

Picha zote na Ingiahedi Mduma- Washington DC.

photo ,


 Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya  Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa (kulia) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majuku ya Bodi kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela leo (Jumatano, Aprili 22, 2015) jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela ameilekeza Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wadaiwa wake na umma kwa ujumla ili kuongeza makusanyo ya marejesho na hatimaye kuwa na mfuko endelevu wa mikopo ya wanafunzi.
Akizungumza na uongozi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 22, 2015), Naibu Waziri Malecela amesema wadaiwa wa Bodi hiyo wakielewa umuhimu wa kulipa mikopo yao, kasi ya ulipaji itaongezeka.
“Ongezeni juhudi zaidi na hasa tengenezeni matangazo ya televisheni yanayotoa elimu ili kuwakumbusha wadaiwa na wananchi kwa ujumla juu umuhimu wa kulipa,” amesema Naibu Waziri wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Maelekezo ya Naibu Waziri yalifuatia taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi iliyowasilishwa na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB Bw. Cosmas Mwaisobwa ambaye alitaja changamoto mbalimbali zinazoikabli HESLB ikiwemo wakopaji wengi na waajiri kutokutoa ushirikiano kwa Bodi katika urejeshwaji mikopo.
“Wakopaji wengi ambao mikopo yao inapaswa kuanza kurejeshwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa Bodi katika kurejesha mikopo yao, na hili linachangiwa pia na kutokuwepo kwa Vitambulisho vya Kitaifa ambavyo vingerahisisha ugunduzi wa wapi walipo wadaiwa hao,” amesema Mwaisobwa katika kikao na Naibu Waziri.
Mwaisobwa alitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na mtazamo potofu kuwa fedha zinazotolewa na Bodi hiyo ni ruzuku badala ya mikopo na kuongezeka kwa idadi ya waombaji mikopo wakiwemo hata wale ambao wazazi wao wana uwezo wa kuwagharamia.
Kwa mujibu wa Mwaisobwa, changamoto nyingine ni pamoja na baadhi ya wazazi, walezi na waajiri na wafadhili wenye uwezo kujitoa katika kugharamia wanafunzi wanaosoma katika taasisi za elimu ya juu kwa kutegemea mikopo inayotolewa na Bodi.
Pamoja na changamoto hizo, Mwaisobwa, kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi alimweleza Naibu Waziri Malecela kuwa katika mwaka wa masomo 2014/2015, kati ya waombaji wa mikopo 39,411 wa mwaka wa kwanza waliofanyiwa tathmini ya uwezo wa kiuchumi, wanafunzi 33,595 walipangiwa mikopo.
Kati ya hao, amesema Mwaisobwa, wanafunzi 31,238 ni wa shahada ya kwanza katika vyuo vya ndani, 2,117 ni wa wanafunzi wa Diploma ya Ualimu katika fani ya sayansi na hisabati na wengine 160 ni wa mwaka wa kwanza wanaosoma nje ya nchi. Wanafunzi 80 ni wa shahada ya Umahiri na Uzamivu katika vyuo vya ndani ya nchi.
Mikopo hiyo hutolewa ili kugharamia maeneo sita ambayo ni chakula na malazi; mafunzo kwa vitendo; vitabu na viandikwa; fedha za utafiti; ada ya mafunzo; na mahitaji maalumu ya kitivo
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Kwa mujibu wa Mwaisobwa, jumla ya wanafunzi 291,582 wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kati ya mwaka 1994 na Juni mwaka jana (2014). Jumla ya kiasi cha fedha kilichokopeshwa hadi kufikia mwaka jana (Juni, 2014) ni Tshs 1.8 trilioni ambapo Tshs 51.1 bilioni zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu Juu, Sayansi na Teknolojia na Tshs 1.75 trilioni zimetolewa na HESLB tangu ilipoanza kazi rasmi Julai 2005

photo ,


Familia aliye kuwa waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine wakiwa katika ibada maalumu ya maadhimisho ya kifo chake  nyumbani kwake monduli juu, siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka
Wake wa  aliye kuwa  waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine  , wakiweka  mashada ya maua kwenye kaburi la  mume wao nyumbani kwake eneo la monduli Juu wilayani monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka.

Watoto wa kiume wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Joseph Sokoine,Tumaini Sokoine na Ibrahimu Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake.

Watoto wa kike wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Maria Sokoine,Joyce Sokoine ,Mbunge wa Viti Maalum Namelok Sokoine na Seki Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake.
 Mbunge wa Viti Maalum, Namelok Sokoine akiwa na kaka yake Ibrahim Sokoine katika kumbukumbu ya kifo cha baba yao aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
 Mbunge wa Viti Maalum na Mtoto wa  aliyekuwa waziri mkuu  wa zamani   hayati Edward Moringe Sokoine, Namelok Sokoine akiongea na baadhi ya wazee wa kimaasai baada ya misa maalumu ya maadhimisho ya kifo  cha Sokoine amabayo yalifanyika  nyumbani kwa marehemu eneo la Monduli juu wilayani Monduli mkoani Arusha .
 Mbunge wa viti maalum, Namelock Sokine akizungumza na wadau 

photo ,


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),kutokaTanzania Dkt. Albina Chuwa akifungua mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Uganda Bw. Ben Mungyereza akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwi mu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashari kikuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Rwanda Bw. Yusuf Murangwa akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa matumizi ya Takwimu baina ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisiya Takwimu Kenya Bw.Zachary Mwangi akizungumza na washiriki wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Burundi Bi. Jeanine Niyukuri akichangia wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afriki Mashariki uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi yaWashiriki wa Mkutano waWataalam wa Takwimu wanchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashari ki wakifuatilia mausuala mbalimbali wakati wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam. 

Na. Veronica Kazimoto,


Wakurugenzi Wakuu wa Ofisi za Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania wamekutana leo  jijini Dar es salaam kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.


Akifungua Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa mkutano huo pamoja na mambo mengine unazileta pamoja Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya Takwimu na mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi hizo.


Amesema kuwa mkutano huo umelenga kuongeza na kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi Wananchama wa Jumuiya hiyo katika matumizi ya Takwimu pamoja na kupitia mabadiliko ya sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya Takwimu kwa Nchi Wanachama.


Kwa upande wao wakurugenzi hao kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, na Burundi wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania kunatoa matumaini ya mwendelezo wa ushirikiano katika matumizi ya takwimu sahihi kutokana na mchango wake katika maendeleo ya nchi zao na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.


Wamesema kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana kikamilifu katika kuhakikisha kuwa kunakuwa na usimamizi mzuri wa takwimu mbalimbali zikiwemo za kilimo, Viwanda, Biashara, uchumi  na takwimu nyingine kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.


Kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ambao umehusisha wakurugenzi wakuu, wakurugenzi na maafisa wandamizi wa takwimu ni mwendelezo wa mikutano mbalimbali inayofanyika katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

photo ,