Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam  April 28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.
Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea maandamano kwenye maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Kikundi cha OUT Jaz Band kikitumbuliza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Nicolas Mgaya akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi K. Lwakatare mkuu wa usalama na mazingira Vodacom kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi maalum Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Makongoro Mahanga wakati wa maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa taasisi mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiondoka kwenye viwanja vya mnazi mmoja baada ya kulihutubia taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa  April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

photo ,

Watanzania waishio nchini Ufaransa walikutana Jumamosi mchana tarehe 26 Aprili nyumbani kwa Balozi wa Tanzania mjini Paris ili kusherehekea miaka 50 ya muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika.
Balozi wa Tanzania Nchini Ufaranza,Mh. Begum Karim Taj akipokea keki maalum kwa ajili ya sherehe hizo za Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa Balozi,Mjini Paris Ufaransa.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa akiwa na watoto mjini Paris.
Mh. Balozi Begum Taj akiwa na baadhi ya watanzania waishio nchini Ufaranza.
Kutoka kushoto: Ndg John Kimaro (Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale), Mh Begum Taj (Balozi wa Tanzania) na Rainfrida Kapela (Mhifadhi Mkuu wa Mambokale Bagamoyo).
Mh Begum Karim Taj akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Watanzania Ufaransa Mh Delly Makombe.
Ndugu Mohammed Sheya akiimba wimbo wa Taifa.
Mama Delly , Mh Balozi Tah na Mama Matari wakikata keki.
Burudani ya uhakika ikiendelea.
Ndg John Kimaro (katikati) akiongea na wageni wakati wa sherehe za Muungano
Mama Rainfrida Kapela Mhifadhi Mkuu wa Mambo ya Kale Bagamoyo
Vyakula mbalimbali katika kuenzi miaka 50 ya muungano.
Baadaye ikawa kazi ya kufungua 'champaign' kuenzi sherehe za Muungano.Picha na Mdau Simplish Lakshi.

photo ,

Mtangazaji Mkongwe kwenye Tasnia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania Maduhu Jumanne ( Mwenye Miwani) ambaye anafanya kazi kwenye kituo cha Radio cha Morningstar Radio na Televisheni ya Morningstar Tv inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato nchini Tanzania akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtayarishaji wa Muziki wa Studio ya Kwanza Records ajulikanaye kwa jina la Vent Skillz
Mtayarishaji wa Muziki (Producer) wa Kwanza Records Vent Skillz akiwa kazini. Studio ya Kwanza Records inapatikana Morogoro Mjini ni studio maarufu na yenye mchango mkubwa katika kukuza, kuendeleza na kuibua vipaji na muziki wa Kitanzania

photo


Mkurugenzi wa kituo cha Wasaidizi wa Sheria cha Morogoro Paralegal Centre Bi. Flora Masoy akiongea na washiriki wa Mafunzo ndani ya ukumbi wa Mikutano.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa katika majadiliano ya Vikundi wakati wa mafunzo
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo wakiwa katika majadiliano.

HABARI KAMILI
Kituo cha Wasaidizi wa Kisheria cha Morogoro Paralegal Centre kinatekeleza mradi wa Kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa Huduma ya Msaada wa kisheria katika Mkoa wa Morogoro.

Mradi huo unafadhiliwa na Legal Services Facility.Ni mradi wa Miaka miwili.
 

photo


 Rais Jakaya Kikwete ameongozi taifa katika maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine katika maadhimisho yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu,tarehe 12/4/2014 Monduli Juu.
Pichani ni juu Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya miaka 30 tangu kifo chake.
 Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akiweka shada la maua
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akiweka shada la maua katika Kaburi la marehemu, Edward Moringe Sokoine.
Spika wa Bunge Anne Makinda akiweka shada la maua.
Mjumbe wa Bunge la Katiba Paul Kimiti akiweka shada la maua kwaniaba ya wajumbe wenzake.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishiriki misa maalum ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika nyumbani kwake Monduli. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenera Mkungara, na motto wa Marehemu sokoine Ndugu Joseph Sokoine
 Viongozi mbalimbali wakishiriki katika Misa maalum ya kumuombea Marehemu.

 Rais Kikwete akisalimiana na Spika wa Bunge Anne Makinda.
Rais Kikwete, akiwa katikati ya wajane wa waziri Mkuu wa Zamani Edward Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya Kiongozi huyo wa zamani wa Tanzania. Wengine kutokla kushoto ni Mjane wa baba wa Taifa, mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Spika wa Bunge, Anne Makinda na mtoto wa Marehemu sokoine Ndugu Joseph Sokoine

photo ,


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akimshukuru Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adefuye baada ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akimpa Naibu Spika Mhe Job Ndugai  Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
 Naibu Spika Mhe Job Ndugai akifurahia Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, akimsikiliza mwendesha shughuli Lady Kate Atabalong Ndi, Kamishna Masuala ya Afrika wa Gavana wa jimbo la Maryland nchini marekani kabla ya  kupokea  Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa Jumatano, Aprili 9, 2014. Kushoto ni Naibu Spika Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Marekani, ambapo alialikwa kuhudhuria hafla hiyo. Nyuma yake ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula.
 Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, akiongea machacha kabla ya  kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa leo, Jumatano, Aprili 9, 2014. Kushoto ni Naibu Spika Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Marekani, ambapo alialikwa kuhudhuria hafla hiyo. Kulia kwake  ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula.
 
  Mhe. Bernard Membe: Hakuna maendeleo bila kushirikiana na sekta binafsi
 
Tanzania itaendelea kufanya jitihada kubwa na kwa hakika itakufa ikijaribu kuimarisha ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kama njia bora zaidi ya kuleta na kudumisha maendeleo endelevu ya kiuchumi nchini.
Aidha, Tanzania imesisitiza kuwa nchi za Afrika ni lazima ziendelee kutafuta namna ya kumaliza migogoro na mizozo yake ya kisiasa na kijeshi, kama msingi mkuu wa kutafuta na kupata maendeleo endelevu na ya kudumu ya kiuchumi kwa watu wake.
Hayo yameelezwa usiku wa Jumatano, Aprili 9, 2014 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, wakati alipopokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 ambalo ametunikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., Mheshimiwa Membe amesema kuwa uzoefu wa Tanzania unaonyesha kuwa ushirikiano na uhusiano wa karibu kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ni msingi mkuu wa maendeleo ya nchi yoyote, ikiwamo Tanzania.
Amesema kuwa ushirikiano kati ya sekta hizo mbili umeleta manufaa na faida kubwa katika maendeleo ya Tanzania katika sekta za huduma za jamii na katika huduma za kiuchumi.
Waziri Membe amesema kuwa mifano ya mafanikio ya ushirikiano kati ya sekta hizo mbili ni wazi katika sekta kama ya elimu ambako Tanzania imefanikiwa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika usajili wa watoto kuingia shule na katika kuleta usawa katika watoto wa kike na kiume wanaoandikishwa kuanza shule kwa sababu Sekta Binafsi inasaidiana na Sekta ya Umma katika kuwekeza katika elimu.
“Kwa sababu ya ushirikiano huo wa karibu, sisi katika Serikali, tumefanya uamuzi kwamba mikopo ya wanafunzi isitolewe kwa wananchi wanaosoma kwenye vyuo vya umma pekee bali kwa wanafunzi wote wakiwamo wale wanaosoma katika vyuo vikuu binafsi. Hivyo, uhusiano kati ya sekta hizo mbili umeleta mafanikio makubwa katika sekta hiyo ya elimu,” amesema Mheshimiwa Membe.
Waziri Membe pia ametaja mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maeneo mengine ya maendeleo kwa sababu ya ushirikiano huo yakiwemo ya utunzaji wa mazingira, usambazaji wa huduma ya maji safi na salama, uboreshaji wa huduma za afya, maendeleo ya miundombinu hasa ya barabara na uboreshaji wa huduma katika kilimo.
Aidha, Waziri Membe amezungumzia hatua zinazochukuliwa na Serikali kuleta uwazi na usimamizi mzuri katika sekta ya gesi hata kabla ya Tanzania haijaanza kuchimba gesi akisisitiza kuwa bila uwazi sekta hiyo itagubikwa na utawala duni, rushwa na usimamizi dhaifu.
 Kuhusu umuhimu wa amani kama sharti la Maendeleo ya Afrika, Waziri Membe amesema kuwa uzoefu wa Afrika na dunia nzima unaonyesha kuwa hakuna maendeleo yoyote na hasa ya kiuchumi bila kuwepo na amani.
Wakati huo huo, Waziri Membe amekutana na kufanya mazungumzo na Gavana wa Jimbo la Maryland, Mheshimiwa Mark O’Malley katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, Marekani.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Membe amemwalika Gavana O’Malley kutembelea Tanzania na kutumia nafasi yake kuhakikisha kuwa Jimbo la Maryland linaanzisha ushirikiano na mkoa mmojawapo wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

9 Aprili, 2014

photo , ,