Showing posts with label AFYA YA JAMII. Show all posts
Showing posts with label AFYA YA JAMII. Show all posts

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya Wastaafu, Ramadhan Maneno, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Jackline Liana, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
 Waziri Simbachawene akitoa hotuba yake
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Gerald Guninita, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba yake kuelezea huduma na fursa mbalimbali zilizopo kwenye Mfuko, wakati wa Mafunzo hayo
 Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea, ambaye pia ni Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa wakuu wa wilaya wastaafu
 Baadhi ya washiriki
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji kupitia mpango wa PSS
 Maafisa wa PSPF, wakifuatilia mafunzo hayo
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, (kulia), akiongozana na Meneja Masoko, na Mawasiliano wa PSPF, Costantina Martin, wakati wa mapumziko
Waziri Simbachawene akitoa hotuba yake

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (katikati), akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Katibu wa Wakuu wa  Wilaya Mstaafu, Betty Mkwasa,  mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Gerald Guninita, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi

 Mkuu wa wilaya mstaafu Manju Msambya, akitoa neno la shukrani
 Waziri Simbachawene, akkimsikiliza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Omar Mangochie(kulia)
 Washiriki wakifuatilia kwa kusoma vipeperushi na kusikiliza


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili kwa wakuu wa wilaya wastaafu iliyoandaliwa na PSPF na kufanyika Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Wenine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji,Mwenyekiti wa Wakuu haoi wa Wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, George Yambesi, na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji, (katikati), wakionyesha fomu za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), mara baada ya waziri kufungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakuu wa Wilaya wastaafu, na Wanachama wastaafu wa Mfuko jijin Dar es Salaam, jana Agosti 15, 2016. Wazuru alimwakilisha Rais John Magufuli kufungua mafunzo hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu
Mtaalamu wa Saikolojia Dkt. Chris Mauki, akitoa mada juu ya kudhibiti Stress
 Picha ya pamoja na viongozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
 Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, viongozi wa PSPF, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na kamati tendaji ya wakuu wa wilaya wastaafu
 Wakurugeni wa PSPF
 Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng' Issa, akitoa mada juu ya fursa zilizopo za uwezeshaji kwa watanzania
Dkt. Kijaji akiteta jambo na Mkuu wa wilaya mstaafu, Betty Mkwasa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia), akifurahia jambo baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi. Waziri Simbachawene, alijiunga na Mfuko huo mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wakuu wa wilaya wastaafu na maafisa wastaafu wa serikali kwa niaba ya Rais John Magufuli jijini Dar es Salaam Agosti 15, 2016.

photo , , ,


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema kuanzisha kambi za kufanya oparesheni kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya  watoto hao kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu  wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.

Makonda amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
Amesema kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha  njia katika kufanya ufadhili wa oparesheni hiyo.

‘’Naamini watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane  ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.

Dk.Kiloloma amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya daktari juu ya oparesheni ya watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa.

Afisa  Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa oparesheni  hiyo.

Amesema kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30, Shinyanga  Mei 2 hadi 4,  Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma  10  hadi 13, Morogoro Mei 15  hadi 17 .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata na utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya kusidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimpa ufunguo za magari,Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa GSM katika hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha MOI jijini Dar es Salaam.

photo , ,


Pichani juu na chini ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Dkt.Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akizungumza katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto akifafanua jambo kwenye kongamano la tisa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Waandishi wa habari lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya Kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya kutoka wilaya mbalimbali walioko mezani mbele wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo la tisa la NHIF,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid ndiye aliyezindua kongamano hilo lililohudhuriwa na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee na pichani kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid wakifuatilia na kusikiliza kwa makini baadhi ya maswali na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahya Nawanda akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mmpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zikijadiliwa ndani ya kongamano hilo mapema leo mchana.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto,Kaimu Mkurugenzi wa Tiba na Ushauri wa NHIF,Bwa.Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakiwa kwenye  kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma.
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima (RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).


photo ,