Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe
akimshukuru Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adefuye
baada ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika
Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini
Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe
akimpa Naibu Spika Mhe Job Ndugai Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango
Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013
aliyopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo
kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano,
Aprili 9, 2014.
Naibu
Spika Mhe Job Ndugai akifurahia Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa
Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopewa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini
Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe,
akimsikiliza mwendesha shughuli Lady Kate Atabalong Ndi, Kamishna
Masuala ya Afrika wa Gavana wa jimbo la Maryland nchini marekani kabla
ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika
Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika
sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini
Washington, D.C., usiku wa Jumatano, Aprili 9, 2014. Kushoto ni Naibu
Spika Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Marekani,
ambapo alialikwa kuhudhuria hafla hiyo. Nyuma yake ni Balozi wa
Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula.
Balozi
wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, akiongea machacha
kabla ya kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi
Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika
sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini
Washington, D.C., usiku wa leo, Jumatano, Aprili 9, 2014. Kushoto ni
Naibu Spika Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini
Marekani, ambapo alialikwa kuhudhuria hafla hiyo. Kulia kwake ni Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula.
Mhe. Bernard Membe:
Hakuna maendeleo bila kushirikiana na sekta binafsi
Tanzania
itaendelea kufanya jitihada kubwa na kwa hakika itakufa ikijaribu kuimarisha
ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kama njia
bora zaidi ya kuleta na kudumisha maendeleo endelevu ya kiuchumi nchini.
Aidha,
Tanzania imesisitiza kuwa nchi za Afrika ni lazima ziendelee kutafuta namna ya
kumaliza migogoro na mizozo yake ya kisiasa na kijeshi, kama msingi mkuu wa
kutafuta na kupata maendeleo endelevu na ya kudumu ya kiuchumi kwa watu wake.
Hayo
yameelezwa usiku wa Jumatano, Aprili 9, 2014 na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, wakati alipopokea Tuzo la Kiongozi
Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013
ambalo ametunikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete.
Akizungumza
katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kwenye Hoteli
ya St. Regis mjini Washington, D.C., Mheshimiwa Membe amesema kuwa uzoefu wa
Tanzania unaonyesha kuwa ushirikiano na uhusiano wa karibu kati ya Sekta ya
Umma na Sekta Binafsi ni msingi mkuu wa maendeleo ya nchi yoyote, ikiwamo
Tanzania.
Amesema
kuwa ushirikiano kati ya sekta hizo mbili umeleta manufaa na faida kubwa katika
maendeleo ya Tanzania katika sekta za huduma za jamii na katika huduma za
kiuchumi.
Waziri
Membe amesema kuwa mifano ya mafanikio ya ushirikiano kati ya sekta hizo mbili
ni wazi katika sekta kama ya elimu ambako Tanzania imefanikiwa kufikia Malengo
ya Maendeleo ya Milenia katika usajili wa watoto kuingia shule na katika kuleta
usawa katika watoto wa kike na kiume wanaoandikishwa kuanza shule kwa sababu
Sekta Binafsi inasaidiana na Sekta ya Umma katika kuwekeza katika elimu.
“Kwa
sababu ya ushirikiano huo wa karibu, sisi katika Serikali, tumefanya uamuzi
kwamba mikopo ya wanafunzi isitolewe kwa wananchi wanaosoma kwenye vyuo vya
umma pekee bali kwa wanafunzi wote wakiwamo wale wanaosoma katika vyuo vikuu binafsi.
Hivyo, uhusiano kati ya sekta hizo mbili umeleta mafanikio makubwa katika sekta
hiyo ya elimu,” amesema Mheshimiwa Membe.
Waziri
Membe pia ametaja mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maeneo mengine ya
maendeleo kwa sababu ya ushirikiano huo yakiwemo ya utunzaji wa mazingira,
usambazaji wa huduma ya maji safi na salama, uboreshaji wa huduma za afya, maendeleo
ya miundombinu hasa ya barabara na uboreshaji wa huduma katika kilimo.
Aidha,
Waziri Membe amezungumzia hatua zinazochukuliwa na Serikali kuleta uwazi na
usimamizi mzuri katika sekta ya gesi hata kabla ya Tanzania haijaanza kuchimba
gesi akisisitiza kuwa bila uwazi sekta hiyo itagubikwa na utawala duni, rushwa
na usimamizi dhaifu.
Kuhusu umuhimu wa amani kama sharti la Maendeleo
ya Afrika, Waziri Membe amesema kuwa uzoefu wa Afrika na dunia nzima unaonyesha
kuwa hakuna maendeleo yoyote na hasa ya kiuchumi bila kuwepo na amani.
Wakati
huo huo, Waziri Membe amekutana na kufanya mazungumzo na Gavana wa Jimbo la
Maryland, Mheshimiwa Mark O’Malley katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye
Hoteli ya St. Regis mjini Washington, Marekani.
Katika
mazungumzo hayo, Mheshimiwa Membe amemwalika Gavana O’Malley kutembelea
Tanzania na kutumia nafasi yake kuhakikisha kuwa Jimbo la Maryland linaanzisha
ushirikiano na mkoa mmojawapo wa Tanzania.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
9 Aprili, 2014
0 Responses so far.
Post a Comment