Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts


Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (katikati) akikata utepe kuzindua  Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Vito Arusha (AGF), Peter Pereira, Wa Pili Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA), Sammy Mollel na wa Pili kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje. 
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (wa kwanza kulia) akiwa katika banda la mdanyabiashara wa madini ya Vito, Bhadrash Pandit katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016. Kulia kwa Mkuu wa wilaya ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila (kushoto), Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (kulia) wakiwa katika kikao na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Vito ya Arusha yanayofanyika katika hoteli ya Mount Meru.
Baadhi ya madini ya Vito yanayopatikana katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016 katika Hoteli ya Mount Meru. Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akifungua maonesho ya kimataifa  ya madini ya Arusha Gem Fair kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix  Ntibenda leo katika hoteli ya Mount Meru . 


Kaimu Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Ally Samaje akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo,alisistiza nia ya serikali kupambana na utoroshwaji wa madini nje ya nchi. 
Mwenyekiti wa kamati ya Arusha Gem Fair,Peter Pereira akitoa neno la utanguliza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya madini yanayohudhuriwa na waoneshaji na wanunuzi zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali duniani. 
 Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa kwenye maonesho ya madini jijini Arusha.
Asteria Muhozya na Teresia Mhagama

Imeelezwa kuwa, Serikali imepata mrabaha wa kiasi cha Shilingi milioni 301 kutokana na mauzo ya madini ya vito yenye thamani ya Shilingi bilioni 7.2 yaliyofanyika wakati wa Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Vito  yaliyofanyika jijini  Arusha mwaka 2015.

Hayo yameleezwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya  Vito-Arusha, yaliyoanza tarehe 19 Aprili na kuendelea hadi tarehe 21 Aprili, 2016.

Alieleza kuwa mrabaha huo uliokusanywa na Serikali unaonesha umuhimu wa maonesho hayo ambayo yanafanyika jijini Arusha kwa mara ya Tano huku lengo likiwa ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu  cha madini ya vito Barani Afrika na hususan kuifanya Arusha kuwa kitovu cha madini hayo barani Afrika.

Alisema kuwa maonesho hayo yamekuwa yakiwakutanisha wanunuzi na wauzaji wa madini  ya Vito kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Thailand, Marekani na India ambapo wauzaji wa madini hayo kutoka Tanzania, wakiwemo wachimbaji wadogo wanapata fursa ya kutanua wigo wa kibiashara kwa kuwa wanakutana na wanunuaji wa madini ya vito kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Ukiangalia Tanzania ina aina mbalimbali za madini ya vito lakini mengi yanapatikana Arusha. Sababu hii pia inapelekea kuifanya Arusha kuwa Kitovu cha madini ya vito nchini. Lakini pia, uwepo wa Maonesho haya unasaidia kuibua changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi kupitia mijadala mbalimbali inaofanyika wakati wa Maonesho kati ya viongozi wa Wizara na wadau wa madini ya Vito.

Vilevile, aliongeza kuwa Maonesho hayo yanafanyika ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 ambayo inaelekeza kuendeleza tasnia ya madini ya Vito na uwepo wa masoko kwa madini ya  vito yanayozalishwa nchini, hivyo Mhandisi Samaje aliwaasa watanzania kutumia fursa  hiyo na kujiweka katika fursa ya kufanya biashara ya madini ya vito.

Aidha, alisema kuwa, maonesho hayo pia yanalenga katika kuongeza thamani madini ya vito kwa kuhamasisha uanzishaji  wa vituo vya kukata na kunakshi madini nchini kabla hayajasafirishwa nje ili kuyafanya madini hayo kuwa na thamani kubwa zaidi.

Wakati huo huo, Kamishna Samaje aliwataka wafanyabiashara  na wachimbaji wa madini kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanafanya biashara na kuchimba  kwa kuzingatia sheria ya Madini ya mwaka 2010.

“Wapo watanzania wasio wazalendo, wamekuwa ndio chanzo cha utoroshaji madini kwa kushirikiana na watu kutoka nje ya nchi. Wapo pia wanaotorosha na kuficha uzalishaji, ukikamatwa unafanya shughuli hizo kinyume, madini yako yatakamatwa na kupigwa mnada na Serikali,” alisisitiza Mhandisi Samaje.

Akifungua Maonesho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu, amesifu maonesho hayo kufanyika jijini Arusha na kueleza kuwa, yameileta Dunia jijini Arusha kutokana na idadi kubwa ya washiriki kutoka pande mbalimbali za dunia .

Aidha, amesema kuwa, uwepo wa maonesho hayo jijini Arusha kunachangia ukuaji  uchumi wa  Tanzania akitolea mfano wa maonesho yaliyofanyika mwaka 2015 na kiasi kilichokusanywa  wakati wa maonesho hayo.

Nkurlu, aliwataka wafanyabiashara na wauzaji wa madini ya vito kujikita zaidi katika uongezaji thamani madini hayo hapa hapa nchini kutokana na umuhimu wake katika sekta hiyo na kueleza kuwa, uongezaji thamani madini utawezesha kuyapandisha thamani madini yanayozalishwa nchini na serikali kupata kodi stahiki.

“Tunataka mapinduzi ya madini ya vito. Wafanyabiashara liangalieni kwa uzito suala la uongezaji thamani madini ili kuwezesha ukuaji uchumi, na kuzalisha ajira kupitia sekta hii,” alisema Nkurlu.

Maonesho ya Tano ya Vito ya Arusha yamehusisha takriban washiriki 900 huku 500 wakitoka nje ya nchi. Maonesho hayo yanakwenda sambamba na majadiliano ya namna ya kuboresha Sekta ya Madini, changamoto zake na namna ya kuzitatua.

photo , ,


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema kuanzisha kambi za kufanya oparesheni kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya  watoto hao kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu  wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.

Makonda amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
Amesema kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha  njia katika kufanya ufadhili wa oparesheni hiyo.

‘’Naamini watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane  ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.

Dk.Kiloloma amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya daktari juu ya oparesheni ya watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa.

Afisa  Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa oparesheni  hiyo.

Amesema kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30, Shinyanga  Mei 2 hadi 4,  Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma  10  hadi 13, Morogoro Mei 15  hadi 17 .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata na utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya kusidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimpa ufunguo za magari,Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa GSM katika hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha MOI jijini Dar es Salaam.

photo , ,


Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (Mbele) akiingia katika ukumbi wa Kings way kufungua mafunzo ya awali (Induction course) kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yanayofanyika katika Hoteli ya Kings Way Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Msadizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bibi Eliaika Manyanga (Kulia) akizungumza na waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo katika mafunzo ya awali (Induction course) yanayofanyika katika Hoteli ya Kings Way Mkoani Morogoro.
Baadhi ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakiwa katika mafunzo ya awali (Induction course) yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali ya waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo jana Mjini Morogoro.
Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway Mkoani Morogoro.
Baadhi ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (hayupo pichani).
Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akijibu maswali mbalimbali ya waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (Katikati waliokaa) na baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo. PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI.

Na Saidi Mkabakuli

Watumishi wa umma nchini wameaswa kuwa waadilifu na kuzingatia ubora wa kazi wakati wanatoa huduma kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Jasper Mero wakati akifungua mafunzo ya awali ya wiki moja kwa waajiriwa wapya 130  wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yanayofanyika katika Hoteli ya Kingsway mkoani Morogoro.

Bw. Mero amesema kuwa udilifu na ubora kwa watumishi wa umma ni kinga dhidi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na ni moja kati ya njia zinazowawezesha watumishi wa umma kuwa wachapakazi hodari.

“Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inaamini katika “Ubora”kwa kila inachokifanya ukianzia ubora wa taarifa za ukaguzi zinazotolewa, huduma bora kwa wadau wake, ubora wa watumumishi kwa maana ya taaluma, maadili, weledi,” alisema Bw. Mero.
Ameongeza kuwa Falsafa hii ya ubora ndiyo iliyoifanya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kupata umaarufu mkubwa kikanda na Kimataifa.   

“Kiwango cha juu cha Ubora wa kazi zetu na utendaji wa kazi unaozingatia weledi vitaweza tu kufikiwa kwa kuajiri watumishi wenye sifa stahiki, maadili, na bidii ya kuchapa kazi na wanaoweza kwenda sambamba na kasi kubwa ya mageuzi katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi,” aliongeza Bw. Mero.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi hiyo, Bw. Gerald Mwanilwa alisema kuwa mafunzo elekezi ni matakwa ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, hususani Kanuni Na.103 (1-6) pamoja na Kanuni za kudumu za Utumishi Serikalini za 2009 Kifungu G.3 (a na b).

“Mafunzo haya ni kwa mujibu wa matakwa ya kisheria na yanalenga kutoa uelewa mahususi kwa waajiriwa wapya kulingana na kada zao,’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Mwanilwa, kupitia mafunzo hayo, washiriki wataweza kuelewa namna ya kutekeleza majukumu yao kama Watumishi wa Umma pamoja na kupata fursa ya kujifunza Miongozo na Nyaraka mbalimbali watakazozitumia kama watumishi wa umma na wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali. 

Pia, kupitia mafunzo hayo watapata fursa ya kujifunza na kuelewa utamaduni wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi unaosisitiza kufanya kazi kwa uweledi, uadilifu na kwa kuzingatia ubora na viwango vya kitaifa na kimataifa ambapo ofisi yetu ni Mwanachama (Intosai Afrosai na Afrosai-E).

“Mafunzo haya ni ya wiki moja yatatoa fursa kwenu kujua maana ya kuwa mtumishi na kazi za mkaguzi na miiko au maadili yake. Pia mtaelezwa kwa kifupi na kupewa utangulizi kuhusu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, sheria mbali mbali, Kanuni na taratibu ili kuwawezesha kuelewa na kufanyakazi kama watumishi wa umma,” aliongeza Bw. Mwanilwa.

photo , ,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia)  nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba  wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.
Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano 
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,  Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald Mwakasendile (kushoto) wakirekodi matukio 
Rais Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.
Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke.

....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais Museven akipita katikati ya  Gwaride la heshima. 
Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Reginald Philip

photo , ,


Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil akizungumza na kuwapongeza wajumbe wa Kikao Kazi cha Uandaaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara yake wa mwaka wa fedha 2015/2016 katika kazi hicho kinachoendelea mjini Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi akitoa mwongozo wa majadiliano kwa Wakuu wa Idara, Maafisa Ununuzi, Maafisa Bajeti na Wakurugenzi Wasaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi cha wizara hiyo Mapesi Manyama katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016 kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro. Kushoto ni Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga aliyesimama ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mapesi Manyama.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Manyama Mapesi akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 wa wizara hiyo, aliyoiwasilisha katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016 kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro. Wa kwanza kutoka kulia walioketi ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi katikati ni Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga akifuatiwa na Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve.
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi cha Jeshi la Polisi Asenga akitoa maelezo na kuwapitisha katika Sheria Mpya ya Ununuzi ya mwaka 2011 katika Taasisi za Umma wajumbe wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa mwaka wa fedha 2015/2016 wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mapitio hayo yamefanyika katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016 kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Vyama Marlin Komba katika wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Kisheria kuhusu masuala ya Ununuzi katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016 kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Maafisa Ununuzi, Wakurugezi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara hiyo kinachoendelea katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro , Wanaomsikiliza ni baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Jeshi la Polisi na Uhamiaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Haji Janabi akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Kifedha yanayohusu Ununuzi katika Taasisi za Umma katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa mwaka wa fedha 2015/2016 wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kikao kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.
Mrakibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Fane Kapinga akiwasilisha Mada kuhusu Uandaaji wa Mpango wa Ununuzi wa Mwaka wa Fedha wa 2015/2016 kwa kutumia Majedwali yaliyoainishwa na Wakala wa Ununuzi Serikalini (PPRA) katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016 kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Maafisa Ununuzi, Wakurugezi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara hiyo kinachoendelea katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akifuatilia kwa makini ufafanuzi wa Sheria Mpya ya Ununuzi ya mwaka 2011 katika Taasisi za Umma wakati Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi cha Jeshi la Polisi Mathew Asenga akitoa maelezo na kuwapitisha katika Sheria Mpya ya Ununuzi ya mwaka 2011 katika Taasisi za Umma wajumbe wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa mwaka wa fedha 2015/2016 wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Makame wa kwanza kutoka kulia akifuatiwa na Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji TRITA mjini Moshi John Choma na watatu kutoka kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Piniel Mgonja wakimsikiliza kwa Makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Manyama Mapesi wakati akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 wa wizara hiyo, aliyoiwasilisha katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016 kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.

photo , ,