Mwanamuziki Jose kamilion kutoka Uganda nae alishiriki katika tamasha kubwa la muziki linaloshirikisha wanamuziki kutoka sehemu mbalimbali duniani alikuwepo katika usiku wa sauti za busara huko Zanzibar...jamaa yupo mbioni kutoa albamu zake mbili na baada ya hapo anategemea kujiingiza katika fani ya uigizaji wa filamu.
Mwanadada Chiwoniso kutoka nchini Zimbabwe akifanya vitu vyake katika tamasha la SAUTI ZA BUSARA huko ngome Kongwe (stone town)
Mfalme wa Hip Hop kutoka Rock City- Mwanza Falid Kubanda (Fid q) nae alikuwepo.
photo
SAUTI ZA BUSARA
Maduhu Emanuel (wa kwanza kushoto)ambaye pia ni katibu wa Kampuni ya Acappella Kwanza,Amani mwaipaja-Mwenyekiti wa Kampuni ya Acappella Kwanza (mwenye Batiki),Enos Kazuzu (wa tatu kutoka kushoto-mkuu wa mawasiliano)na Yusuph Mcharia (makam mwenyekiti-mwenye shati jeupe). Picha hii imepigwa mara tu baada ya kutoka kuzungumza na waandishi wa habari juu ya Tukio la tamasha kubwa la kihistoria la muziki wa A cappella litakaloshirikisha vikundi mbalimbali nchini Tanzania.

Hawa ni vijana wa Sonda ya Dlhu kutoka ukonga jijini Dar es salaam..vijana hawa wanaimba muziki wa A cappella ama muziki usiotumia ala za muziki.Ni vijana wadogo kiumri lakini hufanya mambo makubwa wawapo jukwaani.Wanaimba muziki wa Injili.Vijana hawa pia watakuwepo katika Tamasha la muziki wa Acappella litakalofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa Msimbazi centre.Vijana hawa uimbaji pia nyimbo za makabila mbalimbali.Wana albam moja ambayo itazinduliwa hivi karibuni.
Ni jambo la kawaida tunapokuwa Tukuyu kuvaa makoti kama haya...jamaa wamenitumia picha hii wakiwa wamepozi walipotembelea Tukuyu...vipi hapa kwetu Bongo?
NITAPITA ULIPOPITA NA KUACHA ALAMA ZA NYAYO ZAKO

Mzee Mandela katika pozi siku ya hepibathdei yake
Mara moja moja huwa anapiga suti
Akina mama wakifurahia matunda ya Tanzania.katikati..Mh Asha Rose migiro aliyekula bingo baada ya kuchaguliwa kuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa...Aunt emmy umeiona hii?
Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam lile tamasha la muziki wa A cappella lilokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu sasa limewadia....ni tarehe 11/03/2007 katika ukumbi wa Msimbazi centre kwa kiingilio cha shs 3000 kwa watu wazima na shs 1000 kwa watoto...usikose kuja kushuhudia tamasha la waimbaji wenye vipaji...nimedokezwa kuwa mgeni rasmi atakuwa yule mama aliyekuwa mbunge wa jumuiya ya Africa mashariki....mama Hulda Kibacha.
Waandaaji wa Tamasha hilo..A cappella Kwanza wamejipanga vizuri kwa ajili ya tamasha hilo la kihistorianchini.... hili ni tamasha la kwanza la aina hii kufanyika nchini likishirikisha vikundi mbalimbali vinavyoimba muziki waAcappella.
Mratibu watamasha hilo enos misoji kazuzu anadokeza kuwa baadhi ya vikundi vitakavyoshiriki katika tamasha hilokubwa ni pamoja na
1. busy bee kutoka temeke
2. sonda ya dilu kutoka ukonga
3. jerusalem brothers
4. king's ambassadors
5. the final trumpet
6. the voice A cappella kutoka magomeni
7. steps to christ
na vikundi vingine vingi
Tamasha hilo pia litasindikizwa na waimbaji wanaotumia vyombo kama the peace,nuru kitambo,prince amos,nyakorema na wengineo wengi
usikose ...kaka michuzi umeipata hii?matukio mbalimbali kuhusu tamasha hilo yatawajia kupitia blog hii makini...
Aunt Emmy upo hapo?...nawe pia usikose
Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam lile tamasha la muziki wa A cappella lilokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu sasa limewadia....ni tarehe 11/03/2007 katika ukumbi wa Msimbazi centre kwa kiingilio cha shs 3000 kwa watu wazima na shs 1000 kwa watoto...usikose kuja kushuhudia tamasha la waimbaji wenye vipaji...nimedokezwa kuwa mgeni rasmi atakuwa yule mama aliyekuwa mbunge wa jumuiya ya Africa mashariki....mama Hulda Kibacha.
Waandaaji wa Tamasha hilo..A cappella Kwanza wamejipanga vizuri kwa ajili ya tamasha hilo la kihistorianchini.... hili ni tamasha la kwanza la aina hii kufanyika nchini likishirikisha vikundi mbalimbali vinavyoimba muziki waAcappella.
Mratibu watamasha hilo enos misoji kazuzu anadokeza kuwa baadhi ya vikundi vitakavyoshiriki katika tamasha hilokubwa ni pamoja na
1. busy bee kutoka temeke
2. sonda ya dilu kutoka ukonga
3. jerusalem brothers
4. king's ambassadors
5. the final trumpet
6. the voice A cappella kutoka magomeni
7. steps to christ
na vikundi vingine vingi
Tamasha hilo pia litasindikizwa na waimbaji wanaotumia vyombo kama the peace,nuru kitambo,prince amos,nyakorema na wengineo wengi
usikose mtu wangu...kaka michuzi imeipata hii?matukio mbalimbali kuhusu tamasha hilo yatawajia kupitia blog hii makini...usikose
Aunt Emmy upo hapo?...nawe pia usikose

Kwa muda mrefu nimekuwa kimya baada ya kutingwa na masomo ya sheria huko ughaibuni....chuo kikuu mzumbe kampas ya mbeya
kuanzia sasa kaa mkao wa kula kupata habari mbalimbali zinazojili huku kwetu ughaibuni kwa mapicha na maelezo yakinifu
ndesanjo upo?
photo
mara mojamoja huwa napozi namna hii...nipo ughaibuni-chuokikuu mzumbe-meya kampas