Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam lile tamasha la muziki wa A cappella lilokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu sasa limewadia....ni tarehe 11/03/2007 katika ukumbi wa Msimbazi centre kwa kiingilio cha shs 3000 kwa watu wazima na shs 1000 kwa watoto...usikose kuja kushuhudia tamasha la waimbaji wenye vipaji...nimedokezwa kuwa mgeni rasmi atakuwa yule mama aliyekuwa mbunge wa jumuiya ya Africa mashariki....mama Hulda Kibacha.
Waandaaji wa Tamasha hilo..A cappella Kwanza wamejipanga vizuri kwa ajili ya tamasha hilo la kihistorianchini.... hili ni tamasha la kwanza la aina hii kufanyika nchini likishirikisha vikundi mbalimbali vinavyoimba muziki waAcappella.
Mratibu watamasha hilo enos misoji kazuzu anadokeza kuwa baadhi ya vikundi vitakavyoshiriki katika tamasha hilokubwa ni pamoja na
1. busy bee kutoka temeke
2. sonda ya dilu kutoka ukonga
3. jerusalem brothers
4. king's ambassadors
5. the final trumpet
6. the voice A cappella kutoka magomeni
7. steps to christ
na vikundi vingine vingi
Tamasha hilo pia litasindikizwa na waimbaji wanaotumia vyombo kama the peace,nuru kitambo,prince amos,nyakorema na wengineo wengi
usikose ...kaka michuzi umeipata hii?matukio mbalimbali kuhusu tamasha hilo yatawajia kupitia blog hii makini...
Aunt Emmy upo hapo?...nawe pia usikose
Teknolojia : DG TCAA Ahudhuria Tuzo za Wanafunzi Bora za DIT Jijini Dar es
Salaam
-
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Salim
Msangi amesema taasisi yake itafanya mashirikiano na Taasisi ya Teknolojia
Dar es...
6 hours ago
0 Responses so far.
Post a Comment