Siku chache baada ya Mwaipaja Blog kutundika picha za Msanii Manaika Sanga, Jeshi la polisi kanda ya Dar es Salaam linadaiwa kumtia mbaroni msanii anaetuhumiwa kupiga picha chafu na wanawake mchanganyiko wakiwemo mamiss maarufu na baadae kusambaza kwenye mitandao yote ya kijamii pamoja na kuripotiwa kwenye magazeti mbalimbali
 
Blog ya Mwaipaja imefanikiwa  kuzinasa  picha  za  Manaiki  akiwa chini ya ulinzi kama inavyonekana hapa chini
Habari za uhakika zilizonaswa  zinasema kuwa msanii huyo alikamatwa siku chache baada kuvuja kwa picha zake za aibu zikimuonesha akiwa na wanawake tofauti tofauti

photo

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitoa hoja yake wakati kamati hiyo ilipokutana na Shirika la Nyumba nchini (NHC) jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mbunge wa viti Maalum (CHADEMA) Suzan Kiwanga. Picha na Rafael Lubava

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge

photo

MKUU WA FFU - ARUSHA NA POLISI WENGINE WATATU WAFUKUZWA KAZI.

Imeandikwa na Lydia Churi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na mali zao.

Alisema amewachukulia hatua Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na Mei, 2013.

Waziri Nchimbi aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta Jamal Ramadhan, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Dumila Inspekta Juma Mpamba na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho na kumsimamisha kazi Inspekta Isaack
Manoni.

Alifafanua kuwa Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro alivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maafisa walio chini yake ambao walikamatwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 540 kwa kutumia gari la polisi.

Alisema askari hao wawili waliokamatwa wakisafirisha bangi,walikuwa wakifanya kazi kwenye kituo cha Ngarananyuki na baada ya kukiri kosa walifukuzwa kazi mwezi Mei mwaka huu.

Alisema kwa upande wa Inspekta Jamal Ramadhan amevuliwa madaraka yake kwa kutochukua hatua stahiki baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara wa Mvomero Samson Mwita kubambikiwa fuvu la kichwa cha binadamu na askari polisi watatu wakishirikiana na matapeli wawili.

“Katika tukio hilo Inspekta Isaack Manoni amesimamishwa kazi na atashtakiwa kijeshi kutokana na tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa,Cpl. Edward aliyekuwa dereva wa gari la Polisi lililokamatwa na bangi kitendo ambacho kimelifedhehesha jeshi la polisi” alisema Waziri Nchimbi.

Alibainisha kuwa Inspekta Juma Mpamba amevuliwa madaraka hayo kwa kuonesha udhaifu katika utendaji wake wa kazi kwa kutosimamia kikamilifu askari walio chini yake kitendo kilichosababisha askari kujipangia kazi nje ya utaratibu na kumbambikiza
mfanyabiasha huyo kesi kwa lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi.

Aliongeza kuwa askari waliohusika na tukio hilo wamefukuzwa kazi na kushtakiwa.

Waziri Nchimbi alisema ASP Daniel Bendarugaho amevuliwa madaraka kwa kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa kesi ya mauaji ya marehemu Gasper Mussa Sigwavumba aliyeuawa baada ya kupigwa na askari polisi wawili Desemba mwaka jana.

Alisema upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu huyo wa upelelezi ulisababisha kesi hiyo kuondolewa mahakamani.

Aliongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo utaanza upya ili haki itendeke.

photo

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limefanya kikao cha dharura kujadili madai kwamba wanajeshi wa serikali ya Syria wametumia silaha za kemikali pale walipofanya shambulio dhidi ya eneo lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Damascus hapo jana jumatano.

Wanaharakati wa upinzani wamesema kuwa mamia ya watu wakiwemo watoto wameuwawa huku muungano wa upinzani ukiyataja mauaji hayo ya halaiki. Serikali ya Syria imekanusha kwamba imetumia silaha hizo.

photo

Moto mkubwa umelipuka usiku wa kuamkia leo katika mitambo ya kuzalishia umeme ya Songas iliyopo Ubungo jiji ni Dar es Salaam.
Moto huo umesababisha mitambo hiyo kuzimwa na kusababisha Eneo Kubwa la mkoa aw Dar na maeneo ya jirani kukosa huduma ya umeme.

photo

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter ”  na  wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.

“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,” amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.

photo



Mnamo tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye msafara huo lilikutana na tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele kwa kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi kubwa lililokuwa likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya barabara Dodoma – Iringa yanayoendelea.

Katika ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1. STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
2. STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M] Dodoma.
3. SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
4. DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
5. T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
6. STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo. Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa matibabu na kuruhusuiwa kurudi nyumbani.

Majeruhi waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
1. JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa Kusini Unguja.
2. CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
3. DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Mailimbili.
4. AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya Dodoma.

Majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1. JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C Manispaa ya Dodoma
2. RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala Manispaa ya Dodoma
3. JUMANNE S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4. ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara, wanapaswa kuwa makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.

photo

Chopa iliyombeba Dr. Slaa ikiwa angani kuelekea Ifakara kuhitimisha mkutano wa baraza la katiba kwa mkoa wa Morogoro

Watu waliohudhuria Mkutano wakitawanyika baada ya kumalizika kwa mkutano

photo

 Waandishi wa habari kazini
 Chopa iliyombeba Dr Slaa wakati ikishuka uwanjani

 Vumbi kubwa hutawala wakati chopa inapojiandaa kutua
 DR.Slaa akisindikizwa kuelekea jukwaani
DR. Slaa akiwa wakili Msomi Edson Mbogoro tayari kwa kuhutubia

photo

Baadhi ya wananchi wakiwa tayari kujaza fomu za maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya katika viwanja vvya K-ndege ambapo Dr. Slaa anatarajiwa kuhutubia wananchi mchana wa leo.Mwenye Skafu ya Chadema ni Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kichangani
Mwasisi wa Blog hii. Kaka Amani Mwaipaja akitoa maoni yake kwenye fomu maalum ya kutolea maoni katika viwanja vya shule ya msingi K-Ndege 
Mwanasheria Amani Mwaipaja (Mwenye Miwani) akiwa na Mwanasheria Msomi Bathromew Tarimo (Wakili kwenye kesi ya Sheikh Ponda) katika Viwanja vya Mkutano
Mwasisi wa Blog hii Amani Mwaipaja (Mwenye Miwani) akiwa na Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Morogoro Mjini wakiwa katika picha ya pamoja kwenye viwanja vya Mkutano

photo

Wabongo bado tuna kasafari karefu kidogo kwa upande wa Miundombinu, Vijana tusilale,bado mapambano

photo


 Ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed.
 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amewafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agnes Gerald na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Oliver Thambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya

Aidha, amesema wafukuzwe mara moja ni baada ya kupitia CCTV na kuona namna walivyohusika siku hiyo kwani walionekana wakipiga simu mara watoke nje kinyume na sheria za chumba cha ukaguzi (vifaa hivi ni kama vilivyotumika na CHADEMA kuwanasa polisi waliorusha bomu na baadae kuwashambulia kwa risasi).
Hao waliotajwa hapo juu ni waliofanikisha kupitisha kilo 180 zilizokuwa zimebebwa na wasichana wawili (Masogange na mwenzake) waliokamatwa huko Afrika kusini.

photo

Sehemu ya Jeraha kwenye Bega la Kulia la Sheikh Ponda. Jeraha Hilo linadaiwa kuwa ni la Risasi aliyopigwa wakati wa zoezi la kumkamata mjini Morogoro



Sheikh Ponda akiwa Wodini katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

photo


Habari za uhakika toka kwa chanzo chetu kilichotushushia shehena za picha hizo kilisema msanii huyo ambae pia anaigiza pamoja na kundi la Ze Komedi la East Afrika Tv tangu apate jina amekuwa akijihusisha na vitendo viovu vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwarubuni mabinti kupiga nao picha za aibu kwa lengo la kutafuta jina na amekuwaakitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanikisha suala hilo.



 Mmoja wa Wasanii wa filamu ambaye ameingia kwenye kashfa baada ya kupiga picha na Msanii Manaiki

 Gari la Msanii Manaiki Sanga

 Akiwa kwenye pozi ufukweni

Hizi ni baadhi tu ya Picha  zilizotumwa kwetu.

Wasanii wetu wanapaswa kuelewa kuwa wao ni kioo cha jamii,Vitendo kama hivi ndivyo vinavyochangia kurudisha nyuma maendeleo ya wasanii wetu

photo


photo

Dr Slaa akiwasili katika viwanja vya Kilombero Jijini Arusha

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr Wilbroad Slaa akizungumza na wananchi wa Jijini Arusha jioni ya leo katika muendelezo wa Mikutano ya wazi ya Mabaraza ya Kitaasisi ya Chadema kukusanya maoni ya Katiba Mpya kwa upande wa Chadema kama taasisi kamili.

Dr Slaa kwa siku ya leo amefanikiwa kufanya mikutano miine ya wazi Mkoani Arusha na baadae kushiriki katika kikao kingine cha mabaraza hayo cha ndani kilinachoendelea katika hoteli ya New Arusha.

Katika mikutano hiyo Dr Slaa ameambatana na wanasheria wa chama akiwemo Mabere Marando pamoja na viongozi wengine kutoka makao makuu akiwemo mjumbe wa Kamati Kuu Dr Kitila Mkumbo.

Wananchi mbali mbali walipata fursa ya kutoa maoni yao hadharani katika mjumuiko huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, na kujaza eneo la wazi katika viwanja vya Kilombero Jijini hapa.

Chadema wamepanga kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania wakiwa na lengo la kukusanya maoni ya watu wasiopungua milioni 8. Tayari viongozi mbalimbali wa chama hicho wametawanyika maeneo tofauti ya nchi kuendesha vikao vya mabaraza hayo.

Awali wanasheria mbalimbali wa chama Mkoa wa Arusha walikuwa wakiwaelimisha wananchi masuala mbali mbali kuhusiana na Katiba na sheria kwa ujumla katika kuwaanda vyema kabla ya kutoa maoni yao.


Mratibu wa vikao vya mabaraza ya Chadema, mh Mwita Waitara akisalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Wakili Mabere Marando ambye pia alimkaribisha Dk Slaa


Mwanasheria wa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama, Wakili Mabere Marando akichambua baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba inayokusudiwa kutolewa maoni na wananchi. Marando amesema kwa upande wa Chadema wanaunga mkono zaidi ya asilimia 80 ya mambo yaliyomo katika rasimu hiyo iliyoandaliwa na Tume inayoongozwa na jaji Warioba.


Wananchi wakifuatilia kwa makini maoni mbalimbali


Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono kuashiria kukubaliana na maoni ya mwenzao aliyependekeza vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa kuondolewa kabisa kwenye katiba mpya na badala yake viongozi wa ngazi hizo wachaguliwe na wananchi wa maeneo husika. Zoezi hilo la kutoa maoni lilikuwa linasimamiwa na Dk Slaa


Wanasheria vijana wakiwafafanulia wananchi vipengele mbalimbali vya rasimu ya Katiba. Mwenye suti ni James Lyatuu na mwenye tisheti ya mistari ni Mathias Lyamunda


Kulikuwa na fomu nyingi zilizogawiwa kwa wananchi wengine kutoa maoni yao kwa kuandika kama huyu

Wakili Marando akisoma habari kwenye gazeti

Dk Slaa akibadilishana taarifa na viongozi wa Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, wakati huo huo Marando akizungumza na Ally Bananga. KWA MENGI ZAIDI BOFYA HAPA >>>

photo ,