Ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed.
Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amewafukuza kazi na kuliagiza
jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani
ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia
Agnes Gerald na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea
Afrika Kusini ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Oliver
Thambo nchini humo.
Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya
Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya
Aidha, amesema wafukuzwe mara moja ni baada ya kupitia CCTV na kuona
namna walivyohusika siku hiyo kwani walionekana wakipiga simu mara
watoke nje kinyume na sheria za chumba cha ukaguzi (vifaa hivi ni kama
vilivyotumika na CHADEMA kuwanasa polisi waliorusha bomu na baadae
kuwashambulia kwa risasi).
Hao waliotajwa hapo juu ni waliofanikisha kupitisha kilo 180 zilizokuwa zimebebwa na wasichana wawili (Masogange na mwenzake) waliokamatwa huko Afrika kusini.
Hao waliotajwa hapo juu ni waliofanikisha kupitisha kilo 180 zilizokuwa zimebebwa na wasichana wawili (Masogange na mwenzake) waliokamatwa huko Afrika kusini.
0 Responses so far.
Post a Comment