photo

Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bi. Lulu Kiwia akitoa ufafanuzi kuhusu Kadi ya Usalama wa Kemikali (Material Safety Data Sheet-MSDS) wakati wa mafunzo
 Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye majadiliano
 Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye majadiliano
Mshiriki wa mafunzo akiwasilisha baada ya majadiliano ya vikundi wakati wa mafunzo
Wataalam wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakiwajibika wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari na taasisi zisizo za kiserikali
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa ndugu Daniel Matata akitoa mada wakati wa Mafunzo
Mkemia wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ndugu Fidelis Segumba akitoa ufafanuzi akielezea sheria DNA na Kanuni zake

photo

k
Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali ndugu Sabanitho Mtega amewaasa waandishi wa Habari kutumia Taasisi na Wataalam wa ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kupata majibu sahihi yanayotokana na Uchunguzi unaofanywa na taasisi hiyo ili kuisadia jamii kupata majibu na taarifa iliyo sahihi kutoka kwenye ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali amesema kuwa ili waandishi wa habari waweze kuandika habari za uhakika ipo haja ya wanahabari hao kushirikiana kwa karibu na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kwa kufanya hivyo watakuwa wameepuka tatizo la kuandika habari za kubahatisha.

Ndugu Mtega ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari na wadau kutoka taasisi zisizo za serikali kwenye ukumbi wa Mikutano wa Wakala wa Maabara wa Mkemia Mkuu wa Serikali

photo

 HABARI KAMILI

Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Msajili wa Kemikali za Viwandani na Majumbani ameandaa mafunzo juu ya Matumizi Salama ya Kemikali kwa ajili ya waandishi wa vyombo vya habari (TV,Radio na Magazeti) na asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu matumizi salama ya Kemikali.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mafunzo. Mafunzo hayo yanafanyikia kwenye ukumbi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali uliopo ndani ya jengo la "Mkemia House" barabara ya BarackObama (Zamani Ocean Road)
 Washiriki wa mafunzo wakifuatilia Mafunzo
Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali Ndugu Sabanitho Mtega (Katikati) akifungua mafunzo juu ya Matumizi Salama ya Kemikali. Kushoto kwake ni Bi. Everlight Matinga-Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali. Kulia kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa serikali ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki ndugu Daniel.

TUJENGE TAIFA LETU
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai (Forensic Science) na Vinasaba (kwa kimombo ni Director of Forensic Science and DNA Services) Bi. Gloria Cuthbert Omary ametoa wito kwa waandishi wa Habari kuwa kiungo kati ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Jamii katika kuelimisha na kuleta upatanisho kati ya taasisi hiyo na Jamii ili jamii iweze kujifunza na kuelewa juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Wakala hiyo.

Bi. Gloria amesema kuwa waandishi wa habari wana wajibu wa pekee katika kujenga taifa kwa kuandika habari zilizo sahihi kutoka mamlaka husika na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo watatoa mwanya kwa wanajamii na wadau mbalimbali kuchangia kwa usahihi hoja na mijadala inayohusiana na kazi au matokeo ya Uchuguzi unaofanywa na Wakala wa Mabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini Tanzania.

 WADAU WA KEMIKALI WAZINGATIE SHERIA NA KANUNI
Wadau wa Kemikali nchini wametakiwa kufuata Sheria na Kanuni wakati wa kuingiza, kusafirisha, kuhifadhi, kuuza, kusambaza na wakati wa kutumia kemikali hizo ili kuepusha madhara yanayoweza kuletwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali.

Hayo yamesemwa na Bi. Everlight Matinga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali (katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali) wakati akitoa ufafanuzi kwenye mafunzo hayo kuhusu sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani ambayo lengo lake ni kulinda afya za wananchi na mazingira

photo

Mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA katika kata ya Sombetini Bw. Ally Bananga :Picha na Maktaba.

 Mgombea udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Ally Bananga katika kata ya Sombetini jijini Arusha ,atangazwa Mshindi kwa kura 2564 na kumbwaga chini mgombea mwenzake wa Chama cha Mapinduzi Bw. David .L. Mollel aliyepata kura 2098 na Mgombea wa Chama cha CUF nae akaambulia kura 37. Kwa picha zaidi Bofya hapa >>>

photo ,

Mwenyekiti wa kamati ya ardhi,malaisili na mazingira,Mh James Lembeli akizungumza katika kikao cha watumishi wa hifadhi ya taifa ya Arusha na kamati ya ardhi,maliasili na mazingira.
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira,James Lembeli akiwa ameongozana na naibu waziri wa maliasili na utalii,Mahamud Mgimwa pamoja na kaimu mkurugenzi mkuu TANAPA,Martin Loibooki katika lango kuu la kuingia hifadhi ya taifa ya Arusha(ANAPA).
Baadhi ya watumishi wa hifadhi ya taifa ya Arusha.Naibu waziri wa maliasili na utalii,Mh Mahamud Mgimwa akizungumza katika kikao cha watumishi wa hifadhi ya taifa ya Arusha na kamati ya ardhi,maliasili na mazingira.Kikao cha kamati ya ardhi,malasili na mazingira na watumishi wa hifadhi ya taifa ya Arusha.
Mjumbe wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira ,Mh Humud Abdi Jumaa akizungumza katika kikao cha watumishi wa hifadhi ya taifa ya Arusha na kamati ya ardhi,maliasili na mazingira. Kwa hisani ya Wazalendo 25 Blog

photo , ,


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, wakati alipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam. Picha na OMR

photo ,


Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kitabu cha Mandela toka kwa Mkurugenzi wa Programu wa Spintelligent ya Afrika Kusini Bi. Amore Swart baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Januari 28, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Bi Meab Mdimi wa Kampuni ya Kilimo ya TECHNOSERVE  baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo katika banda la Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Kusini mwa Ukanda wa Afrika (SAGCOT)    baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

photo ,


Mhe. Tundu Lissu ambae ni kiongozi wa M4C -PAMOJA DAIMA kanda ya Kaskazini akiwa na Kamanda Daniel Urioh (Kulia) ,ambae anatarajia kuchukua Udiwani kata ya Olasiti 2015.
Chopa ikitua katika viwanja vya Sombetini-Jijini Arusha
Mama mzazi wa Diwani mtarajiwa wa CHADEMA Bw. Ally Bananga akiwa katika harakati za kumsapoti mwanae kwenye kampeni.

Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Bw. John Heche akimnadi mgombea wa Udiwani  kata ya Sombetini jijini Arusha
Aliyekuwa diwani wa kata ya Sombetini Bw. Alfonso Mawazo akimweleza Bw. John Heche imani yake kwa Ally Bananga agombee Udiwani  kata ya Sombetini.
Mhe. Tundu Lissu ambae ni kiongozi wa M4C -PAMOJA DAIMA kanda ya Kaskazini akimnadi mgombea wa Udiwani  kata ya Sombetini jijini Arusha.


Mhe. Ephata Nanyaro ambae ni Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Arusha Mjini, akimnadi mgombea wa Udiwani  kata ya Sombetini Bw. Ally Bananga.
Bw. Amani Golugwa ambae ni Mratibu wa CHADEMA kanda ya kaskazini, akimnadi mgombea wa Udiwani  kata ya Sombetini Bw. Ally Bananga.
Mhe. Joshua Nassari ambae ni Mbunge wa Arumeru Mashariki akimnadi mgombea wa Udiwani  kata ya Sombetini Bw. Ally Bananga.
Chopa ikiondoka katika viwanja vya sombetini Jijini Arusha.
Wananchi wakiishangilia CHOPA inavyoondoka katika viwanja vya Sombetini Jijini ,Arusha. Picha Zote na Gadiola Emanuel

photo ,


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini waliohudhuria Kongamano la siku mbili linalohusu Rasilimali za Gesi Asilia, Mafuta na Madini kwa Amani na Maendeleo ya Tanzania linalofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA UFUNGUZI WA...

photo

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kujaza nafasi za mawaziri watano walioacha nafasi zao wazi, kutokana na sababu mbalimbali. Katika uteuzi huo, Rais Kikwete ameteua mawaziri wapya wawili na Naibu mawaziri wapya wanane, huku akiwapandisha vyeo naibu mawaziri wanne kuwa mawaziri kamili.
Aidha katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Rais Kikwete amempumzisha kazi waziri mmoja na naibu mawaziri wanne, huku akihamisha mawaziri wawili na naibu mawaziri sita kutoka katika wizara walizokuwa wakitumikia kabla ya mabadiliko. 
Kwa mujibu mabadiliko hayo, waziri pekee aliyepumzishwa kazi ni Dk Terezya Huvisa, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Naibu mawaziri waliopumzishwa kazi ni Gregory Teu, aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Philipo Mulugo, aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Wengine ni Benedict Ole-Nangoro aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Goodluck Ole-Medeye, aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kabla ya kupumzishwa kazi kwa mawaziri hao, nafasi zilizokuwa wazi ziliachwa na Balozi Khamis Kagasheki, aliyejiuzulu katika nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, kutokana na ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyomhusisha na ukiukwaji wa sheria, uliofanywa na watendaji wa chini yake.
Wengine ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Kikwete kutokana na ripoti hiyo ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo). Nafasi nyingine iliachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, aliyefariki dunia Afrika Kusini kutokana na maradhi.
Mawaziri wapya ni Dk Asha-Rose Migiro, ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kabla ya hapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Katika mabadiliko hayo, Dk Titus Kamani, Mbunge wa Busega ndiye mteule pekee aliyetoka kuwa Mbunge na kuwa Waziri kamili katika Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Wengine wapya ambao wameteuliwa kuwa naibu mawaziri ni Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Dk Kebwe Stephen, Naibu Waziri, Afya na Ustawi wa Jamii na Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Dk Pindi Chana ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kaika Telele, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Wengine ni Godfrey Zambi, kuwa Naibu Waziri Kilimo, Chakula na Ushirika, Juma Nkamia, Naibu Waziri Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mahmoud Mgimwa, Naibu Waziri, Maliasili na Utalii.
Mbali na wateule wapya, Rais Kikwete amewapandisha vyeo naibu mawaziri wanne, akiwemo Saada Mkuya Salum kutoka Naibu Waziri wa Fedha, kuwa Waziri wa Fedha. Mwingine ni Lazaro Nyalandu kutoka Naibu Waziri Maliasili na Utalii kuwa waziri kamili katika wizara hiyo na Dk Seif Seleman Rashidi kutoka Naibu Waziri, Afya na Ustawi wa Jamii mpaka Waziri kamili wizara hiyo hiyo.
Dk Binilith Mahenge yeye amepandishwa cheo na kuhamishwa, kutoka Naibu Waziri wa Maji na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
Rais Kikwete pia amewahamisha mawaziri wawili, akiwemo Dk Hussein Ali Mwinyi kutoka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kwa uhamisho huo, Dk Mwinyi anakuwa na historia ya kuwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa mara mbili, kama ilivyo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambako amewahi kuiongoza mara mbili.
Mathias Chikawe aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, amehamishwa kwenda kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Naibu mawaziri waliohamishwa ni pamoja na George Simbachawene, kutona Wizara ya Nishati na Madini, kwenda Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Amos Makalla kutoka Wazara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwenda Wizara ya Maji.
Wengine ni Charles Kitwanga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenda Wizara ya Nishati na Madini; Adam Malima kutoka Wazara ya Kilimo, Chakula na Ushirika mpaka Wizara ya Fedha.
Pia, Janet Mbene aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, amehamishiwa Wizara ya Viwanda na Biashara na Ummy Mwalimu, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, kwenda Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira.

photo ,