Vanessa Mdee a.k.a Vmoney akiimba jukwaani huku akiwa na staili yake ya kipekee kabisa
Barnaba Boy akiimba juu ya jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoni Tanga mwishoni mwa wiki
Wadau nao walikuwepo kupata selfie ya Globu ya jamii ndani ya Fiesta.
Linah akilinogesha jukwaa la Fiesta na wimbo wake wa Ole Temba.
Kwa jijna la Kisanii anajiita Vmoney a.k.a Vanessa Mdee akiimba kwa hisia jukwaani
Ommy Dimpoz akiimbajuukwani wimbo wake wa Nani kama Mama
Ommy Dimpoz na vijana wake wakilishambulia jukwaa.
Ommy Dimpoz akimpagawisha shabiki wake jukwaani kwa staili ya Kantangazee...!
Ali Kiba na vijana wake wakilishambulia jukwaa la Fiesta
Msanii wa muziki wa kizazi ajulikanae kwa jina la Khadija Maumivu akiiimba jukwaani kwenye tamasha la Fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Mkwakwani,mkoani Tanga lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Anajiita Rais wa Manzese,Madee akiwaimbisha wakazi wa jiji la Tanga waliojoitokeza kwenye tamasha la Fiesha mkoani Tanga mwishoni mwa wiki.
Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesha mwishoni mwa wiki.
Pichai kati ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah akiwa sambamba na madansa wake wakilishambulia jukwaa,mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Tanga (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Mkwakwani,mwishoni mwa wiki.
Maelekezo ya hapa na pale kutoka kwa mafundi mitambo na jukwaa ilikuwa ikifanyika ili mambo yaende sawa
Umati wa watu uliofurika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kupata burudani safi wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Ilikuwa ni Sheeddaah kwa wakazi wa jiji la Tanga ndani ya uwanja wa Mkwakwani mwishoni mwa wiki.
Rachae akiiimba jukwaani.

Sehemu ya umati mkubwa wa watu ukifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati tamasha la Fiesta 2014 likiendelea
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Rachael akionesha umahiri wake wa kucheza na kuimba mbele ya umati wa watu uliofurika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga (hawapo pichani ) kwenye tamasha la Fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Khadija Mumivu, akikonga nyoyo za mashabiki walioingia katika tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga  mwishoni mwa wiki.
Kwa jina la kisanii anaitwa MO MUSIC akiwakuna wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Tanga
Mmoja wa wasanii wa kundi la ngoma asili ya Baikoko toka mjini Tanga akiwajibika jukwaani wakati wa tamasha la Fiesta 2014
Umati wa watu uliofurika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kupata burudani safi wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyoka mwishoni mwa wiki.
Sehemu ya watazamaji wakiendelea kutazama yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha hilo mwishoni mwa wiki mjini Tanga.PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-FIESTA TANGA.

photo , ,


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuzindua jengo jipya la Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha kijiji cha Kinole, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akikata  utepe  kuzindua jengo jipya la Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha kijiji cha Kinole, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. Wengine ni Mama Salma Kikwete (kulia),  Mbunge wa Viti Maalum Dkt Lucy Nkya (wa [ili kulia) na Mwenyekiti wa SACCOS ya Kinole Mzee Issa Ramadhani Kambi

 Rais Kikwete akikagua jengo jipya la SACCOS ya Kinole baada ya kulizindua
 Rais Kikwete akiwa ameongozana na Chifu Kingalu na Mwenyekiti wa SACCOS ya Kinole Mzee Issa Ramadhani Kambi baada ya kuzindua jengo la chama hicho kijijini Kinole
 Rais Kikwete na Chifu Kingalu wakiwatuza wacheza ngoma vijana wa kijiji cha Kinole waliokuwa wakitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Rais Kikwete akimtambulisha Chifu Kingalu kwa Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Mama Salma Kikwete akiongea na baadhi ya kinamama kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Mbunge wa viti maalumu Dkt Lucy Nkya akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Umati wa wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akitoa muhtasari na kukaribisha wasemaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Stephen Masele akielezea mikakati ya serikali ya kusambaza umeme vijijini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi na kueleza mikakati ya serikali katika kuendeleza na kuboresha miundombinu nchini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Mbunge Mhe Innocent Kalogeris akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Rais Kikwete akiongea na mtoto Rebecca Mbena ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kinole wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
  Mama Salma Kikwete  akiongea na mtoto Rebecca Mbena ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kinole wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
  Mama Salma Kikwete  akiongea na mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kinole wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Chifu Kingalu  Mama Salma Kikwete  akiongea na mtoto Rebecca Mbena ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kinole wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi ya Kinole Agosti 22, 2014. PICHA NA IKULU

photo ,


Kamishna Jenerali wa Jeshi Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) kabla ya kusaini Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la Magereza na Kmapuni hiyo ya uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill leo Agosti 21, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) wakisaini nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia katika mradi wa uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) wakibadilishana nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la Magereza na Kampuni ya Twiga Cement katika mradi wa uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiaji sahini wa Makubaliano ya ubia wa mradi wa uchimbaji madini ya Ujenzi katika Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza walioshiriki hafla ya utilianaji sahini Makubaliano ya ubia huo wakimsikiliza Mtaalam Mshauri wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Said Abdallah(hayupo pichani) namna Jeshi la Magereza litakavyonufaika na mradi huo wa madini.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Na; Lucas Mboje

Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la Magereza limeingia makubaliano rasmi ya mradi wa uchimbaji madini ya Chokaa na Kampuni ya Saruji ya Twiga katika eneo la Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salam.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Alhamisi 21 Agosti, 2014 katika Ukumbi wa Mkutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wanahabari, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amesema kuwa ushirikiano huo kati ya Shirika la Magereza na Twiga Cement unalenga kuimarisha Shirika la Magereza ili liweze kujiendesha kibiashara kwa kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi.

Ametaja madini na maeneo ambayo Jeshi hilo litafanya uchimbaji madini kwa ubia ni pamoja na Chokaa, mawe, kokoto, mchanga, zahabu na moramu   katika maeneo ya Magereza mbalimbali hapa nchini ambayo ni Maweni(Tanga), Lilungu(Mtwara), Bahi(Dodoma), Msalato(Dodoma), Majimaji(Songea), Kalilankulukulu(Mpanda).

“Tayari Jeshi la Magereza limepata leseni 164 za Uchimbaji wa madini ya Ujenzi, vito na zahabu katika maeneo mbalimbali ya magereza hapa nchini” Alisema Kamanda Minja.

Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa upatikanaji wa leseni hizo ni mojawapo ya hatua ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Magereza, hususani katika kuipunguzia Serikali gharama za kuhudumia magereza na kuongeza pato la Kodi kwa Taifa.

“Vyanzo vilivyobuniwa kuongeza tija ni pamoja na kuingia ubia na Wawekezaji wenye nia ya dhati ya kushirikiana na Jeshi letu katika madini hayo” Alisisitiza Kamanda Minja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw.Alfonso Rodrudges amesema kuwa Kampuni yake ipo tayari kwa dhati kushrikiana na Shirika la Magereza katika mradi huo wa uchimbaji madini ya ujenzi na kuwa yapo mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika Ujenzi wa Barabara katika Jiji la Dar es Salaam.

“Makubaliano haya ya ubia yataongezea uhakika wa upatikanaji wa madini ya chokaa katika maeneo ya karibu na Kiwanda chetu hivyo kuongeza uzalishaji wa saruji nchini na kuwa na muda mrefu zaidi(lifespan) wa kuendesha shughuli za Kiwanda chetu” Alisema Bw. Rodrudges.

Pia ameongeza kuwa mbali na kuliongezea mapato Jeshi la Magereza katika mradi huo pia Kampuni yake itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi Maofisa na Askari wa Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam hivyo kupunguza changamoto kubwa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari.

Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Makubaliano hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa Shirika la Magereza katika kukuza mtaji na kubadilishana ujuzi katika miradi mbalimbali ya madini hayo.

photo ,

 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye ukumbi wa NEC Dodoma ,akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana tayari kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Maua Abeid Daftari akijadiliana jambo na mjumbe mwenzake Samia Suluhu Hassan muda mfupi kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa hakijaanza kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC Oganizesheni Dk.Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM DK. Salim Ahmed Salim ndani ya ukumbi wa mkutano wa White House kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakijadiliana kabla ya kuanza kwa kikao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma, kutoka kuchoto ni Profesa Anna Tibaijuka, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Dodoma.

photo ,