Showing posts with label JESHI LA MAGEREZA. Show all posts
Showing posts with label JESHI LA MAGEREZA. Show all posts

 Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi wa Magereza (SACP) Annethy Laurent.
 Mwili wa Marehemu Anneth ukiwasili katika Kanisa Katoliki Parokiani Segerea. Walio mbele ni Pamela  (mtoto wa dada yake na Marehemu) na aliyebeba picha ni mtoto wa Pamela ( Mjukuu wa Marehemu). Walioshika jeneza kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Dk.Kato Rugainunura, kulia ni Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Magereza Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Rajab Nyange
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati wa ibada ya kumuombea Marehemu.
 Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Mallya akitoka salaam za Jeshi la Magereza kwa wafiwa kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa  Magereza John C. Minja.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga akitoka salaam za pole kwa wafiwa kwa niamba ya Kamati yake ambayo pia aliongozana nayo katika msiba huo (hawapo pichani)
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga(Mwenye miwani) akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. Wa pili ni Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akifuatiwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakhim Maswi wakitoa salaam zao za mwisho.
Mwili wa  Marehemu Anneth ukiwasili katika kanisa katoliki parokiani Segerea tayari kwa misa takatifu ya kumuombea marehemu.
PIX 8: Baada ya misa takatifu  msafara wa kuelekea makaburini ulianza ukiongozwa na Kamishina Jenerali wa Magereza (CGP) John Minja.
Picha zote na Mkaguzi wa Magereza Moses Sebastian
Makao Makuu ya Magereza.

photo , , ,


Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akiwakaribisha Wanahabari ambao wakitembelea gerezani hapo Desemba 19, 2014. Wanahabari hao wapo katika ziara ya kikazi katika miradi mbalimbali ya Uzalishaji mali inayotekelezwa kwa mafanikio makubwa na Jeshi la Magereza(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mororogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula.
Wafungwa wa kike wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro wakifuma mashuka katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza hilo. Wafungwa hao wanapitiwa ujuzi wa aina mbalimbali ikiwemo Ushonaji wa nguo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu za Urekebishaji ndani ya Magereza hapa nchini.
Muonekano wa mashuka na mito yake yanayofumwa na Wafungwa Wanawake katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro.
Wanahabari wakionja chakula cha Wafungwa katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014(kulia) ni Mwandishi kutoka Gazeti la Habari Leo, Bi. Regina Kumba(kushoto) ni Mwandishi kutoka Gazeti la Daily News, Bw. Finning Simbeye(katikati) ni Mwanahabari kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Bi. Rose Mdami.
Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akipokea rasmi msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Wanahabari hao kwa ajili ya Wafungwa wa kike gerezani hapo walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014.
Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akikabidhi msaada huo kwa Mfungwa wa Kike ambaye ndiye Nyampara Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro. Wafungwa wa Gereza hilo wamewashukru Wanahabari hao kuwatembelea pamoja na msaada huo walioutoa na wameahidi kuwa raia wema mara wamalizapo vifungo vyao.
Msaada wa vitu mbalimbali vya Kibinadamu na vinavyoruhusiwa Magerezani vilivyokabidhiwa na Wanahabari walipotembelea Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro Desemba 19, 2014.
Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wanahabari walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kato Rugainunula.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

photo ,

Wafungwa wa Gereza Idete wakilima shamba kwa kutumia trekta kama inavyoonekana katika picha. Wafungwa hao wamepatiwa ujuzi wa kulima na trekta wakiwa gerezani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji zinazofanywa na Jeshi la Magereza hapa nchini. Kwa wastani Wafungwa hao hulima hekari 10 kwa siku.
Mkuu wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Beno Hunja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) walipotembelea Ofsini kwake Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi unaoendelea wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mradi huo unajengwa kwa kutumia fedha za ndani na utagharimu kiasi cha Bilioni 2.8 hadi kukamilika kwake hivyo kukamilika kwa mradi huo kutalifanya Jeshi la Magereza kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi kuliko hivi sasa.
Mkuu wa Gereza Idete, Beno Hunja akiwaongoza Waandishi wa Habari kutembelea eneo kunakojengwa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.
Sehemu ya Mbanio na chanzo Kikuu cha kupokelea maji yatakayotumika katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakifanya mahojiano na Mkuu wa Gereza Idete(hayupo pichani) walipofanya ziara yao ya kikazi Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.
Mfereji ambao tayari umekamilika kujengwa katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)

photo , ,


Kamishna Jenerali wa Jeshi Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) kabla ya kusaini Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la Magereza na Kmapuni hiyo ya uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill leo Agosti 21, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) wakisaini nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia katika mradi wa uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) wakibadilishana nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la Magereza na Kampuni ya Twiga Cement katika mradi wa uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiaji sahini wa Makubaliano ya ubia wa mradi wa uchimbaji madini ya Ujenzi katika Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza walioshiriki hafla ya utilianaji sahini Makubaliano ya ubia huo wakimsikiliza Mtaalam Mshauri wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Said Abdallah(hayupo pichani) namna Jeshi la Magereza litakavyonufaika na mradi huo wa madini.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Na; Lucas Mboje

Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la Magereza limeingia makubaliano rasmi ya mradi wa uchimbaji madini ya Chokaa na Kampuni ya Saruji ya Twiga katika eneo la Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salam.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Alhamisi 21 Agosti, 2014 katika Ukumbi wa Mkutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wanahabari, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amesema kuwa ushirikiano huo kati ya Shirika la Magereza na Twiga Cement unalenga kuimarisha Shirika la Magereza ili liweze kujiendesha kibiashara kwa kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi.

Ametaja madini na maeneo ambayo Jeshi hilo litafanya uchimbaji madini kwa ubia ni pamoja na Chokaa, mawe, kokoto, mchanga, zahabu na moramu   katika maeneo ya Magereza mbalimbali hapa nchini ambayo ni Maweni(Tanga), Lilungu(Mtwara), Bahi(Dodoma), Msalato(Dodoma), Majimaji(Songea), Kalilankulukulu(Mpanda).

“Tayari Jeshi la Magereza limepata leseni 164 za Uchimbaji wa madini ya Ujenzi, vito na zahabu katika maeneo mbalimbali ya magereza hapa nchini” Alisema Kamanda Minja.

Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa upatikanaji wa leseni hizo ni mojawapo ya hatua ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Magereza, hususani katika kuipunguzia Serikali gharama za kuhudumia magereza na kuongeza pato la Kodi kwa Taifa.

“Vyanzo vilivyobuniwa kuongeza tija ni pamoja na kuingia ubia na Wawekezaji wenye nia ya dhati ya kushirikiana na Jeshi letu katika madini hayo” Alisisitiza Kamanda Minja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw.Alfonso Rodrudges amesema kuwa Kampuni yake ipo tayari kwa dhati kushrikiana na Shirika la Magereza katika mradi huo wa uchimbaji madini ya ujenzi na kuwa yapo mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika Ujenzi wa Barabara katika Jiji la Dar es Salaam.

“Makubaliano haya ya ubia yataongezea uhakika wa upatikanaji wa madini ya chokaa katika maeneo ya karibu na Kiwanda chetu hivyo kuongeza uzalishaji wa saruji nchini na kuwa na muda mrefu zaidi(lifespan) wa kuendesha shughuli za Kiwanda chetu” Alisema Bw. Rodrudges.

Pia ameongeza kuwa mbali na kuliongezea mapato Jeshi la Magereza katika mradi huo pia Kampuni yake itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi Maofisa na Askari wa Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam hivyo kupunguza changamoto kubwa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari.

Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Makubaliano hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa Shirika la Magereza katika kukuza mtaji na kubadilishana ujuzi katika miradi mbalimbali ya madini hayo.

photo ,