Na Anna Nkinda – Maelezo, Mafia 
Wazazi na walezi wilayani Mafia wametakiwa kutokubali kupokea mahari za watoto wao wakiwa wanafunzi bali wawasimamie na kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kufika elimu ya chuo kikuu. 
 Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanafunzi pamoja na wazazi wa shule ya Sekondari Bweni iliyopo kata ya Kanga wilaya ya Mafia mkoani Pwani. 
 Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema baadhi ya wazazi wanapokea mahari za watoto wao na kuwaozesha wakiwa na umri mdogo jambo ambalo huwafanya kukatisha masomo yao na wanawanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu. 
 “Mtoto akisoma atakuwa na maisha mazuri hapo baadaye ataweza kufanya kazi za kitaalamu za kuajiriwa au kujiajiri yeye mwenyewe, kujikomboa na umaskini, kuwasaidia wazazi wake, ataepukana na mimba za utotoni na kujiepusha na maradhi yanayotokana na ngono zembe kwani elimu ni msingi wa kila kitu”. 
Wanawake wenzangu mtoto wako wa kike akiwa mwali usikubali kumuweka ndani ili asubiri mwanaume wa kumuoa na ukisikia mmeo kapokea mahari ili binti huyo aolewe katoe taarifa sehemu inayohusika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake”, alisisitiza Mama Kikwete. 
 Kwa upande wa wanafunzi aliwaasa kujiepusha na kitendo cha kujiingiza katika mapenzi wakiwa na umri mdogo bali wasome kwa bidhii , wawe na nidhamu kwa walimu wao na kuwa na malengo katika maisha yao kwa kufanya hivyo watatimiza ndoto zao. 
 Alisema, “Wanangu someni kwa bidii msitake utajiri wa haraka, watoto wa kiume mnaacha kwenda shule, mnakatisha masomo na kukimbilia kuvua samaki kwa kudhani kuwa mtapata maendeleo kumbukeni elimu ni urithi usioweza kutoweka katika maisha yenu”,. 
 Aidha Mwenyekiti huyo wa WAMA aliwahimiza wazazi kwenda Hospitali kupima ugonjwa wa saratani za shingo ya kizazi, matiti na tezi dume ambazo zikigundulika katika hatua ya awali mgonjwa anaweza kutibiwa na kupona kabisa. 
 Kuhusu utunzaji wa ardhi Mama Kikwete alisema wilaya hiyo imejaliwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba inayowavutia watu wengi na kuwasihi wananchi kutoiuza kiholela bali waitunze, kama kuna wawekezaji utaratibu maalum ufuatwe. 
 Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndekilo aliwahimiza wananchi hao kuona umuhimu wa kuwarithisha watoto wao elimu ambayo ni ufunguo wa maisha na siyo mali kama uvuvi, ng’ombe na mashamba. 
 Eng. Ndekilo alisema atakuwa mkali kwa mtu yoyote atakayekatisha elimu ya mtoto wake na katika suala la mtoto kuacha shule baada ya kupewa ujauzito mahakama ndiyo itakayotoa maamuzi na siyo wazazi kumalizana wenyewe kwa wenyewe. 
 Akisoma taarifa ya shule Mwalimu mkuu Mohamed Msossow alisema shule hiyo ilifunguliwa mwaka 2007 ikiwa na walimu wanne na wanafunzi 199 kati ya hao wavulana walikuwa 147 na wasichana 52 . Hivi sasa kuna walimu 20 na wanafunzi 131 kati ya hao wavulana 61 wasichana 70 na walimu 20. Aliyataja mafanikio waliyo nayo ni walimu wa kutosha wa masomo ya sanaa, vitabu vya kutosha vya masomo ya sayansi na sanaa kwa uwiano wa mwanafunzi mmoja kwa kitabu kimoja, madarasa ya kutosha, ushirikiano mzuri na jamii inayowazunguka na matokeo mazuri ya kitaaluma katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne. 
 “Changamoto zinazotukabili ni upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati, nyumba za walimu na vifaa vya maabara, kutokana na mazingira ya mahali shule ilipo shule inahitajika kuwa na usafiri ili kurahisisha walimu kufika wilayani”. 
 Idadi ndogo ya wanafunzi inayosababisha kupata mgao mdogo wa fedha ya ruzuku kutoka Serikalini na kusababisha ugumu katika kuendesha shughuli mbalimbali za shule, ukosefu wa umeme na uhaba wa vyanzo vya maji”,alisema Mwalimu Msossow. Mama Kikwete yuko wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na akiwa shuleni hapo aliwapatia wanafunzi zawadi ya shilingi milioni moja. 
 Shule ya Sekondari Bweni imejengwa na Taasisi ya Maendeleo ya Kisiwa cha Mafia (MIDEF) chini ya usimamizi wa Dkt. Ramadhan Dau ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuikabidhi kwa Serikali ambapo hivi sasa ni Shule ya Sekondari ya kata ya Kanga.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kuanza ziara ya siku mbili wilayani humo tarehe 13.3.2015
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mwalimu Mariam Halfan Haji mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kama ishara ya upendo na kumkaribisha rasmi kutembelea wilaya ya Mafia tarehe 13.3.2015
 Akina mama wa Mafia waliofika kumpokea Mama Salma Kikwete wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia wanaonekana wakiwa wamebeba mabango ya kumkarisha wilayani humo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau alikuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliofika kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kwa ajili ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili wilayani humo tarehe 13.3.2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi/albino aliyekuwa amebebwa na mama yake. Mama Salma alikutana na mtoto huyo wakati alipowasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau akitoa maelezo mafupi kuhusu Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia ambayo imejengwa na “Mafia Island Development Foundation, MIDEF”. Dkt. Dau ni mmoja wa viongozi wa Taasisi hiyo. Mama Salma alitembelea  Shule hiyo tarehe 13.3.2015. Waliokaa kutoka kushoto ni Mbunge wa Mafia Mheshimiwa Abdulkarim Shah, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo,  Ndugu Mohamed Msosa, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo na mwisho ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mafia.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia  tarehe 13.3.2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi. PICHA NA JOHN LUKUWI

photo , ,

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wawekezaji wa Misri wanaotaka kuwekeza katika Sekta ya Viwanja Wilayani Mkuranga, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo leo, Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri,alikohudhuria mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Misri, Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya mkutano huo, uliofanyika jana Machi 13, 2015 mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake Wawekezaji wa Misri wanaoataka kuwekeza katika Sekta ya Viwanda Wilayani Mkuranga, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri alikohudhuria mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati akiwa katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Machi 13, 2015 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi na Maendeleo nchini Misri. Mkutano huo umeandaliwa na Rais wa Misri Mheshimiwa Abdel Fattah Al Sisi na umehudhuriwa na viongozi karibu wote kutoka katika nchi za Kiarabu, marais na viongozi wakubwa wa nchi mbalimbali za Afrika pamoja na wakuu wa vyombo mbalimbali vya Kimataifa akiwemo pia Waziri wa Mmabo ya Nje wa Marekani John Kerry.
Akizungumza katika Mkutano huo, Rais wa Misri aliueleza ulimwengu kuwa Misri imepita jaribio kubwa na sasa iko imara tayari kusonga mbele hivyo wale wote walio na nia ya kuwekeza nchini Misri wafanye hivyo kwa kuwa serikali yake itashirikiana nao katika kuwalinda wao na mali zao. Pia Rais Sisi alifafanua kuwa, nchi yake inarejesha heshima yake iliyokuwa nayo zamani kutokana na mchango wake katika Umoja wa nchi za Kiarabu huku pia akisisitiza kuwa Misri sasa inarejea Afrika ambako anatambua kuna ndugu wa dhati.
Akihutubia mkutano huo Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal aliishukuru Misri kwa kuialika Tanzania kuhudhuria mkutano huo na akafafanua kuwa Tanzania inafurahia uamuzi wa Misri wa kujijenga upya huku ikikumbuka historia ya kutaka kujiwekea nafasi yake katika Afrika na katika nchi za Kiarabu.
“Mheshimiwa Rais, uitishaji wako wa mkutano huu mkubwa ni kiashirio kuwa sasa Misri inajijenga upya na kwamba inarejesha heshima yake katika Bara la Afrika, Nchi za Kiarabu na Dunia kwa ujumla,” alisema Mheshimiwa Dkt Bilal na kuendelea kuwa:
“Tunakupongeza kwa uongozi thabiti uliouonesha hadi sasa ambapo Misri inaonekana kuwa imara na thabiti. Uhusiano wetu ni wa kihistoria hivyo Tanzania inakupongeza na inaahidi kushirikiana nanyi katika ujenzi mpya wa Taifa lenu.” Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alitumia nafasi hiyo kuueleza mkutano huo kuwa eneo ilipo Misri linaunganisha Afrika, Nchi za Kiarabu na Ulaya na Tanzania nayo iko katika eneo la kitajiri kijiografia ambapo ukiwekeza nchini Tanzania unakuwa unapata fursa za ziada za kuwekeza katika nchi za Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Afrika.
“Ukiwekeza Tanzania utakuwa na uhakika wa soko la watu wasiopungua milioni 400 na nchi zetu ni lango la nchi zipatazo nane ambazo hazina bahari,” mheshimiwa Makamu wa Rais alisema na kufafanua kuwa Tanzania inakaribisha wawekezaji kama ambavyo Misri inafanya na zaidi akaeleza kuwa fursa za uwekezaji Tanzania ni nyingi na hasa sasa ambapo tunaelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Katika mkutano huu, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata nafasi ya kukutana na Mheshimiwa Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi na kuzungumza naye na kisha kuhudhuria mada ya kiuchumi iliyowasilishwa na Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake wanarejea nyumbani kesho tayari kuendelea na majukumu mengine ya Kitaifa.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Sharm el Sheikh, Machi 14, 2015

photo


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa kwa furaha alipowasili uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 kuongoza kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani  iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo
 Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Mohamed Aziz Abood 
 Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mkoa wa Morogoro
 Rais Kikwete akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez
 Sehemu ya umati uliofurika uwanjani hapo
 Rais Kikwete akiwa meza kuu. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Rajab Rutengwe, Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez
 Bendi ya Jeshi la Polisi likiongoza maandamano makubwa ya wanawake yakiingia uwanjani
 Rais Kikwete na Meza kuu ikipokea maandamano hayo
 Maandamano
 Kinamama wakisherehekea siku yao
 Rais Kikwete akipungia maandamano
 TTCL wamependeza na miavuli yao
 Benki ya posta








 Kina baba hawakuwa nyuma






 Msanii Starah Thomas akiimba wimbo maalum akisaidiwa na wanafunzi
 Msanii Peter Msechu akiimba na kucheza na wanafunzi
 Mtoto Miriam Edward akitumbuiza
 Mwanadada hodari  Hazala 'The Ball Juggler' Mohammed akipiga danadana
 Vijana wa Sifa Theatre Troupe wakitumbuiza
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Rajab Rutengwe akisoma utangulizi wa sherehe hizo
 Mwakilishi wa kinamama wajasiriamali wa Morogoro Bi. Emmy Kiula akisoma Risala yao
 Rais Kikwete akipokea risala toka kwa Mwakilishi wa kinamama wajasiriamali wa Morogoro Bi. Emmy Kiula
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia kwa Kiswahili fasaha
 Rais Kikwete akimpongeza Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez kwa hotuba nzuri, Kushoto ni Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba 
 Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Ulaya (EU) Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi pia akihutubia hadhara hiyo kwa Kiswahili fasaha
 Sehemu ya Umati
 Umati wa wakaazi waMorogoro na vitongoji vyake
 Mabalozi wa nchi mbalimbali walihudhuria
 Mabalozi na viongozi wa taasisi mbalimbali zinasohudumia wanawake
 Umati


 Viongozi wa vyama vya siasa wakitambulishwa
 Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba akimkabidhi Rais Kikwete tuzo maalum ya Wanawake kwa mchango wake mkubwa wa kujali maslahi yao
 Rais Kikwete akifurhia tuzo yake
 Rais Kikwete akimkabidhi tuzo Celina Ompeshi Kombani  mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki
 Rais Kikwete akimtuza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe Muhingo Rweyemamu kwa kazi kubwa aliyoifanya kuendeleza elimu ya wasichana alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni
 Mwakilishi wa TAMWA akipokea tuzo kwa kazi nzuri inayofanywa na taasisi hiyo
  Mwakilishi wa TAMWA akipokea tuzo ya pili kwa kazi nzuri inayofanywa na taasisi hiyo

 Tuzo kwa kazi nzuri
 Tuzo kwa masista wanaosaidia kupiga vita ukeketaji 
 Rais Kikwete akihutubia
 Rais Kikwete akifafanua jmbo katika hotuba yake
 Rais Kikwete akiagana na viongozi wa dini
 Baada ya hotuba Rais Kikwete akipiga picha ya pamoja na makundi mbalimbali ya wadu wa Wanawake



 Rais Kikwete akitembelea mabanda ya maonesho
 Rais Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa PPF Morogoro
Rais Kikwete akiongea na mtoto Reuben Boniface mwenye umri wa miaka 9 na manafunzi wa darasa la nne shule ye Elu Children Care
 Rais Kikwete katika banda la WOGE
 Rais Kikwete akikagua banda la Halmashauri ya Mkoa wa Morogoro
Rais Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Halmashauri ya Morogoro

photo ,