Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts


 Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya  Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa (kulia) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majuku ya Bodi kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela leo (Jumatano, Aprili 22, 2015) jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela ameilekeza Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wadaiwa wake na umma kwa ujumla ili kuongeza makusanyo ya marejesho na hatimaye kuwa na mfuko endelevu wa mikopo ya wanafunzi.
Akizungumza na uongozi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 22, 2015), Naibu Waziri Malecela amesema wadaiwa wa Bodi hiyo wakielewa umuhimu wa kulipa mikopo yao, kasi ya ulipaji itaongezeka.
“Ongezeni juhudi zaidi na hasa tengenezeni matangazo ya televisheni yanayotoa elimu ili kuwakumbusha wadaiwa na wananchi kwa ujumla juu umuhimu wa kulipa,” amesema Naibu Waziri wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Maelekezo ya Naibu Waziri yalifuatia taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi iliyowasilishwa na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB Bw. Cosmas Mwaisobwa ambaye alitaja changamoto mbalimbali zinazoikabli HESLB ikiwemo wakopaji wengi na waajiri kutokutoa ushirikiano kwa Bodi katika urejeshwaji mikopo.
“Wakopaji wengi ambao mikopo yao inapaswa kuanza kurejeshwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa Bodi katika kurejesha mikopo yao, na hili linachangiwa pia na kutokuwepo kwa Vitambulisho vya Kitaifa ambavyo vingerahisisha ugunduzi wa wapi walipo wadaiwa hao,” amesema Mwaisobwa katika kikao na Naibu Waziri.
Mwaisobwa alitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na mtazamo potofu kuwa fedha zinazotolewa na Bodi hiyo ni ruzuku badala ya mikopo na kuongezeka kwa idadi ya waombaji mikopo wakiwemo hata wale ambao wazazi wao wana uwezo wa kuwagharamia.
Kwa mujibu wa Mwaisobwa, changamoto nyingine ni pamoja na baadhi ya wazazi, walezi na waajiri na wafadhili wenye uwezo kujitoa katika kugharamia wanafunzi wanaosoma katika taasisi za elimu ya juu kwa kutegemea mikopo inayotolewa na Bodi.
Pamoja na changamoto hizo, Mwaisobwa, kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi alimweleza Naibu Waziri Malecela kuwa katika mwaka wa masomo 2014/2015, kati ya waombaji wa mikopo 39,411 wa mwaka wa kwanza waliofanyiwa tathmini ya uwezo wa kiuchumi, wanafunzi 33,595 walipangiwa mikopo.
Kati ya hao, amesema Mwaisobwa, wanafunzi 31,238 ni wa shahada ya kwanza katika vyuo vya ndani, 2,117 ni wa wanafunzi wa Diploma ya Ualimu katika fani ya sayansi na hisabati na wengine 160 ni wa mwaka wa kwanza wanaosoma nje ya nchi. Wanafunzi 80 ni wa shahada ya Umahiri na Uzamivu katika vyuo vya ndani ya nchi.
Mikopo hiyo hutolewa ili kugharamia maeneo sita ambayo ni chakula na malazi; mafunzo kwa vitendo; vitabu na viandikwa; fedha za utafiti; ada ya mafunzo; na mahitaji maalumu ya kitivo
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Kwa mujibu wa Mwaisobwa, jumla ya wanafunzi 291,582 wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kati ya mwaka 1994 na Juni mwaka jana (2014). Jumla ya kiasi cha fedha kilichokopeshwa hadi kufikia mwaka jana (Juni, 2014) ni Tshs 1.8 trilioni ambapo Tshs 51.1 bilioni zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu Juu, Sayansi na Teknolojia na Tshs 1.75 trilioni zimetolewa na HESLB tangu ilipoanza kazi rasmi Julai 2005

photo ,


Na Anna Nkinda – Maelezo, Mafia 
Wazazi na walezi wilayani Mafia wametakiwa kutokubali kupokea mahari za watoto wao wakiwa wanafunzi bali wawasimamie na kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kufika elimu ya chuo kikuu. 
 Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanafunzi pamoja na wazazi wa shule ya Sekondari Bweni iliyopo kata ya Kanga wilaya ya Mafia mkoani Pwani. 
 Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema baadhi ya wazazi wanapokea mahari za watoto wao na kuwaozesha wakiwa na umri mdogo jambo ambalo huwafanya kukatisha masomo yao na wanawanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu. 
 “Mtoto akisoma atakuwa na maisha mazuri hapo baadaye ataweza kufanya kazi za kitaalamu za kuajiriwa au kujiajiri yeye mwenyewe, kujikomboa na umaskini, kuwasaidia wazazi wake, ataepukana na mimba za utotoni na kujiepusha na maradhi yanayotokana na ngono zembe kwani elimu ni msingi wa kila kitu”. 
Wanawake wenzangu mtoto wako wa kike akiwa mwali usikubali kumuweka ndani ili asubiri mwanaume wa kumuoa na ukisikia mmeo kapokea mahari ili binti huyo aolewe katoe taarifa sehemu inayohusika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake”, alisisitiza Mama Kikwete. 
 Kwa upande wa wanafunzi aliwaasa kujiepusha na kitendo cha kujiingiza katika mapenzi wakiwa na umri mdogo bali wasome kwa bidhii , wawe na nidhamu kwa walimu wao na kuwa na malengo katika maisha yao kwa kufanya hivyo watatimiza ndoto zao. 
 Alisema, “Wanangu someni kwa bidii msitake utajiri wa haraka, watoto wa kiume mnaacha kwenda shule, mnakatisha masomo na kukimbilia kuvua samaki kwa kudhani kuwa mtapata maendeleo kumbukeni elimu ni urithi usioweza kutoweka katika maisha yenu”,. 
 Aidha Mwenyekiti huyo wa WAMA aliwahimiza wazazi kwenda Hospitali kupima ugonjwa wa saratani za shingo ya kizazi, matiti na tezi dume ambazo zikigundulika katika hatua ya awali mgonjwa anaweza kutibiwa na kupona kabisa. 
 Kuhusu utunzaji wa ardhi Mama Kikwete alisema wilaya hiyo imejaliwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba inayowavutia watu wengi na kuwasihi wananchi kutoiuza kiholela bali waitunze, kama kuna wawekezaji utaratibu maalum ufuatwe. 
 Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndekilo aliwahimiza wananchi hao kuona umuhimu wa kuwarithisha watoto wao elimu ambayo ni ufunguo wa maisha na siyo mali kama uvuvi, ng’ombe na mashamba. 
 Eng. Ndekilo alisema atakuwa mkali kwa mtu yoyote atakayekatisha elimu ya mtoto wake na katika suala la mtoto kuacha shule baada ya kupewa ujauzito mahakama ndiyo itakayotoa maamuzi na siyo wazazi kumalizana wenyewe kwa wenyewe. 
 Akisoma taarifa ya shule Mwalimu mkuu Mohamed Msossow alisema shule hiyo ilifunguliwa mwaka 2007 ikiwa na walimu wanne na wanafunzi 199 kati ya hao wavulana walikuwa 147 na wasichana 52 . Hivi sasa kuna walimu 20 na wanafunzi 131 kati ya hao wavulana 61 wasichana 70 na walimu 20. Aliyataja mafanikio waliyo nayo ni walimu wa kutosha wa masomo ya sanaa, vitabu vya kutosha vya masomo ya sayansi na sanaa kwa uwiano wa mwanafunzi mmoja kwa kitabu kimoja, madarasa ya kutosha, ushirikiano mzuri na jamii inayowazunguka na matokeo mazuri ya kitaaluma katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne. 
 “Changamoto zinazotukabili ni upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati, nyumba za walimu na vifaa vya maabara, kutokana na mazingira ya mahali shule ilipo shule inahitajika kuwa na usafiri ili kurahisisha walimu kufika wilayani”. 
 Idadi ndogo ya wanafunzi inayosababisha kupata mgao mdogo wa fedha ya ruzuku kutoka Serikalini na kusababisha ugumu katika kuendesha shughuli mbalimbali za shule, ukosefu wa umeme na uhaba wa vyanzo vya maji”,alisema Mwalimu Msossow. Mama Kikwete yuko wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na akiwa shuleni hapo aliwapatia wanafunzi zawadi ya shilingi milioni moja. 
 Shule ya Sekondari Bweni imejengwa na Taasisi ya Maendeleo ya Kisiwa cha Mafia (MIDEF) chini ya usimamizi wa Dkt. Ramadhan Dau ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuikabidhi kwa Serikali ambapo hivi sasa ni Shule ya Sekondari ya kata ya Kanga.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kuanza ziara ya siku mbili wilayani humo tarehe 13.3.2015
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mwalimu Mariam Halfan Haji mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kama ishara ya upendo na kumkaribisha rasmi kutembelea wilaya ya Mafia tarehe 13.3.2015
 Akina mama wa Mafia waliofika kumpokea Mama Salma Kikwete wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia wanaonekana wakiwa wamebeba mabango ya kumkarisha wilayani humo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau alikuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliofika kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kwa ajili ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili wilayani humo tarehe 13.3.2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi/albino aliyekuwa amebebwa na mama yake. Mama Salma alikutana na mtoto huyo wakati alipowasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau akitoa maelezo mafupi kuhusu Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia ambayo imejengwa na “Mafia Island Development Foundation, MIDEF”. Dkt. Dau ni mmoja wa viongozi wa Taasisi hiyo. Mama Salma alitembelea  Shule hiyo tarehe 13.3.2015. Waliokaa kutoka kushoto ni Mbunge wa Mafia Mheshimiwa Abdulkarim Shah, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo,  Ndugu Mohamed Msosa, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo na mwisho ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mafia.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia  tarehe 13.3.2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi. PICHA NA JOHN LUKUWI

photo , ,


TA1
Afisa Mwandamizi Uraghibishi wa Ushindani,Alex Mbaga akizungumza kwenye semina hiyo leo kwa wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka taasisi mbalimbali juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa.
TA2
Mkuu wa Idara ya Cartels (Makubaliano yanayodhirisha ushindani) kutoka Tume ya Ushindani Dar es Salaam,Shedrack Nkelebe akisisitiza jambo kwenye semina hiyo iliyohusisha wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka taasisi mbalimbali juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa.
TA3
wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia semina ya juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa
TA4
Wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia semina ya juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa
TA5
Washiriki wa semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja leo iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa
TA6
Washiriki wa semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja leo iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa
TA7
Bi Martha Mapalala kutoka mmoja wa waratibu wa semina hiyo inayofanyika mkoani Tanga.
...................................................................................
NA MWANDISHI WETU,TANGA MAAFISA Ugavi nchini wametakiwa kuzingatia ubora wa vitu vinavyonunuliwa kwenye maeneo yao jambo ambalo litapelekea kuondoka bidhaa feki kwenye soko.

Wito huo ulitolewa leo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Noel Mrope wakati wa semina ya wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka taasisi mbalimbali juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini hapa.

Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao juu ya umuhimu wa kufanya manunuzi yanayozingatia thamani halisi ya fedha iliyoendeshwa na bodi ya taaluma ya manunuzi na ugavi nchini (PSPTB).

“Pamoja na kuzingatia sheria za Manunuzi lakini kwa kinachonunuliwa kuanzia fedha zilizotumika kwenye manunuzi kwa sababu hali hii itawezesha kuondoa uwepo wa bidhaa feki zinazosambazwa kwenye masoko “Alisema Mdhahiri huyo.

Aidha alisema kuwa mambo ya muhimu yaliyotiliwa mkazo kwenye semina hiyo ni namna ya wataalamu hao kuangalia thamani ya kitu na jinsi gani kinaweza kutumika katika kupandisha thamani yake na ubora ili mwisho wa siku watu wengi waweze kukitumia kitu hicho. “Katika jambo hili lazima wataalamu wa manunuzi kuhakikisha kwa pamoja wanafuata taratibu za manunuzi kwa kuzingatia sheria lengo likiwa kuona uthamani na ubora wa kitu ikiwemo thamani ya fedha halisi iliyotumika “Alisema.

Alisema kuwa kuwa kimsingi maafisa hayo wanatakiwa wanapokwenda kununua vitu wasikimbilie bei ya chini bali waangalie ubora na thamani ya kitu halisia ili kuweza kuzipa changamoto bidhaa zisizokuwa na kiwango kukosa soka na hatimaye kuondoka kwenye soko la ushindani.

Hata hiyo alisema kuwa wananchi wanapobaini kuna vitu vimefanyika kwenye Halmashauri yao chini ya kiwango wanapaswa kulalamika kupitia maeneo husika ili kuweza kukabiliana na hali hiyo.

photo ,


 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akimsikiliza mtoto mwenye mahitaji maalum Mohammed Hashim aliyeweza kuimba vizuri wimbo wa Taifa.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza mtoto Mohammed Hashim mara baada ya kuimba wimbo wa Taifa.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kufundisha darasa la wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma katika Shule ya Msingi Mpilipili huko Lindi tarehe 11.2.2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpilipili mara baada ya kutembelea kitengo cha elimu maalum shuleni hapo tarehe 11.2.2015.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Salma Kikwete akisahihisha madaftari ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma Shule ya Msingi Mpilipili katika Manispaa ya Lindi mara baada ya kuwafundisha na kuwapa zoezi wanafunzi hao tarehe 11.2.2015.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Salma Kikwete akisahihisha madaftari ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma Shule ya Msingi Mpilipili katika Manispaa ya Lindi mara baada ya kuwafundisha na kuwapa zoezi wanafunzi hao tarehe 11.2.2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpilipili mara baada ya kutembelea kitengo cha elimu maalum shuleni hapo tarehe 11.2.2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpilipili namna bora ya kubeba mifagio yao ili kuepuka kuwaumiza wanafunzi wenzao.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpilipili mara baada ya kutembelea kitengo cha elimu maalum tarehe 11.2.2015.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Mtuleni B katika Kata ya Matopeni huko Lindi Mjini tarehe 11.2.2015.
 Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Mpilipili Kaskazini katika Kata ya Nachingwea huko Lindi Mjini tarehe 11.2.2015.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akisalimiana na mamia ya wananchi wenye shauku kubwa wakati alipowasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara kwenye Tawi la Mpilipili Kaskazini katika Kata ya Nachingwea huko Lindi Mjini tarehe 11.2.2015.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la CCM Mpilipili Kaskazini wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipowahutubia tarehe 11.2.2015.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la Mpilipili katika Kata ya Nachingwea huko Lindi Mjini  tarehe 11.2.2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa Kata ya Nachingwea baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Tawi la Mpilipili Kaskazini huko Lindi Mjini tarehe 11.2.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwalimu Mkuu Ndugu Fadhili Mtitima wa Shule ya Msingi Mpilipili iliyoko Manispaa ya Lindi tarehe 11.2.2015. Mama Salma alikwenda shuleni hapo kuwatembelea wanafunzi wenye mahitaji maaalum.
PICHA NA JOHN  LUKUWI

photo , ,


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.

Alielezea kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.

Mhe. Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
 Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu  hicho katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe 21.11.2014.
  Mhe. Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi  (mwenye kofia ya njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi  Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa mahafali hayo ya kumi na moja.
 Shekhe Dr.Badruh H.Sseguja akifungua kwa sala Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
  Mchungaji Ogah Ogbole akifungua kwa sala mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba ya ufunguzi wa  mahafali hayo ya kumi na moja ya chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwa utulivu tayari kabisa kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 902 walihitimu masomo yao.
 Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakiingia katika viwanja vya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam tayari kwa mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja.
   Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja ambapo aliwaasa kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
 Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala wakinyanyua kofia zao juu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali yao ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo wakifuatilia hatua kwa hatua kile kinachoendelea katika sherehe hizo.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala akitunuku shahada kwa wahitimu wa mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi ( mwenye joho la njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Membe pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo wa taifa kama ishara ya kufunga mahafali hayo ya kumi na moja.
 Mgeni rasmi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali hayo.   PICHA NA Reuben Mchome 

photo , ,