Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (katikati) akikata utepe kuzindua  Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Vito Arusha (AGF), Peter Pereira, Wa Pili Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA), Sammy Mollel na wa Pili kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje. 
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (wa kwanza kulia) akiwa katika banda la mdanyabiashara wa madini ya Vito, Bhadrash Pandit katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016. Kulia kwa Mkuu wa wilaya ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila (kushoto), Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (kulia) wakiwa katika kikao na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Vito ya Arusha yanayofanyika katika hoteli ya Mount Meru.
Baadhi ya madini ya Vito yanayopatikana katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016 katika Hoteli ya Mount Meru. Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akifungua maonesho ya kimataifa  ya madini ya Arusha Gem Fair kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix  Ntibenda leo katika hoteli ya Mount Meru . 


Kaimu Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Ally Samaje akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo,alisistiza nia ya serikali kupambana na utoroshwaji wa madini nje ya nchi. 
Mwenyekiti wa kamati ya Arusha Gem Fair,Peter Pereira akitoa neno la utanguliza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya madini yanayohudhuriwa na waoneshaji na wanunuzi zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali duniani. 
 Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa kwenye maonesho ya madini jijini Arusha.
Asteria Muhozya na Teresia Mhagama

Imeelezwa kuwa, Serikali imepata mrabaha wa kiasi cha Shilingi milioni 301 kutokana na mauzo ya madini ya vito yenye thamani ya Shilingi bilioni 7.2 yaliyofanyika wakati wa Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Vito  yaliyofanyika jijini  Arusha mwaka 2015.

Hayo yameleezwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya  Vito-Arusha, yaliyoanza tarehe 19 Aprili na kuendelea hadi tarehe 21 Aprili, 2016.

Alieleza kuwa mrabaha huo uliokusanywa na Serikali unaonesha umuhimu wa maonesho hayo ambayo yanafanyika jijini Arusha kwa mara ya Tano huku lengo likiwa ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu  cha madini ya vito Barani Afrika na hususan kuifanya Arusha kuwa kitovu cha madini hayo barani Afrika.

Alisema kuwa maonesho hayo yamekuwa yakiwakutanisha wanunuzi na wauzaji wa madini  ya Vito kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Thailand, Marekani na India ambapo wauzaji wa madini hayo kutoka Tanzania, wakiwemo wachimbaji wadogo wanapata fursa ya kutanua wigo wa kibiashara kwa kuwa wanakutana na wanunuaji wa madini ya vito kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Ukiangalia Tanzania ina aina mbalimbali za madini ya vito lakini mengi yanapatikana Arusha. Sababu hii pia inapelekea kuifanya Arusha kuwa Kitovu cha madini ya vito nchini. Lakini pia, uwepo wa Maonesho haya unasaidia kuibua changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi kupitia mijadala mbalimbali inaofanyika wakati wa Maonesho kati ya viongozi wa Wizara na wadau wa madini ya Vito.

Vilevile, aliongeza kuwa Maonesho hayo yanafanyika ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 ambayo inaelekeza kuendeleza tasnia ya madini ya Vito na uwepo wa masoko kwa madini ya  vito yanayozalishwa nchini, hivyo Mhandisi Samaje aliwaasa watanzania kutumia fursa  hiyo na kujiweka katika fursa ya kufanya biashara ya madini ya vito.

Aidha, alisema kuwa, maonesho hayo pia yanalenga katika kuongeza thamani madini ya vito kwa kuhamasisha uanzishaji  wa vituo vya kukata na kunakshi madini nchini kabla hayajasafirishwa nje ili kuyafanya madini hayo kuwa na thamani kubwa zaidi.

Wakati huo huo, Kamishna Samaje aliwataka wafanyabiashara  na wachimbaji wa madini kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanafanya biashara na kuchimba  kwa kuzingatia sheria ya Madini ya mwaka 2010.

“Wapo watanzania wasio wazalendo, wamekuwa ndio chanzo cha utoroshaji madini kwa kushirikiana na watu kutoka nje ya nchi. Wapo pia wanaotorosha na kuficha uzalishaji, ukikamatwa unafanya shughuli hizo kinyume, madini yako yatakamatwa na kupigwa mnada na Serikali,” alisisitiza Mhandisi Samaje.

Akifungua Maonesho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu, amesifu maonesho hayo kufanyika jijini Arusha na kueleza kuwa, yameileta Dunia jijini Arusha kutokana na idadi kubwa ya washiriki kutoka pande mbalimbali za dunia .

Aidha, amesema kuwa, uwepo wa maonesho hayo jijini Arusha kunachangia ukuaji  uchumi wa  Tanzania akitolea mfano wa maonesho yaliyofanyika mwaka 2015 na kiasi kilichokusanywa  wakati wa maonesho hayo.

Nkurlu, aliwataka wafanyabiashara na wauzaji wa madini ya vito kujikita zaidi katika uongezaji thamani madini hayo hapa hapa nchini kutokana na umuhimu wake katika sekta hiyo na kueleza kuwa, uongezaji thamani madini utawezesha kuyapandisha thamani madini yanayozalishwa nchini na serikali kupata kodi stahiki.

“Tunataka mapinduzi ya madini ya vito. Wafanyabiashara liangalieni kwa uzito suala la uongezaji thamani madini ili kuwezesha ukuaji uchumi, na kuzalisha ajira kupitia sekta hii,” alisema Nkurlu.

Maonesho ya Tano ya Vito ya Arusha yamehusisha takriban washiriki 900 huku 500 wakitoka nje ya nchi. Maonesho hayo yanakwenda sambamba na majadiliano ya namna ya kuboresha Sekta ya Madini, changamoto zake na namna ya kuzitatua.

photo , ,


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema kuanzisha kambi za kufanya oparesheni kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya  watoto hao kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu  wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.

Makonda amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
Amesema kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha  njia katika kufanya ufadhili wa oparesheni hiyo.

‘’Naamini watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane  ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.

Dk.Kiloloma amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya daktari juu ya oparesheni ya watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa.

Afisa  Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa oparesheni  hiyo.

Amesema kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30, Shinyanga  Mei 2 hadi 4,  Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma  10  hadi 13, Morogoro Mei 15  hadi 17 .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata na utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya kusidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimpa ufunguo za magari,Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa GSM katika hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha MOI jijini Dar es Salaam.

photo , ,



Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, Mh.Abdullah Mwinyi, (katikati-wapili kulia), akipewa maelezo na meneja wa soko la samaki Ferry, Bw.Solomon Mushi, kuhusu biashara ya samaki sokoni hapo leo Aprili 20, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wameendelea na ziara za kutembelea shughuli za kiuchumi za wananchi na leo Aprili 20, 2016 walikuwa kwenye soko la samaki la kimataifa ferry jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao wakongozwa na mwenyekiti wao, Mh. Makongoro Nyerere, Wamewaeleza viongozi wa wavuvi, wakaanga samaki na wapaa samaki fursa zilizopo kwenye ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki ambapo kwa sasa lina jumla ya nchi wanachama sita, Sudan Kusini ikiwa ndio mwanachama wa hivi karibuni kabisa.
Wabunge hao pia wametembelea na kujionea shughuli zihusianazo na samaki kwenye soko hilo. Pia walipata fursa ya kusikiliza maoni mbalimbali ya wadau hao katika soko la samaki Ferry. Soko lasamaki Ferry ni moja ya maeneo yanayotoa ajira kwa vijana wengi hapa jijini Dar es Salaam, ambao ukiacha wavuvi wao hufanya kazi ya kupaa samaki, kushusha samaki kutoka kwenye mitumbwi na kukaanga samaki. Pia kuna akina mama na baba wanaotoa huduma za chakula.
Mh. Mwinyi, akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana mawazo baina ya wabunge hao nawashika dau kwenye soko hilo, wengine kutoka kushoto ni Meneja wa soko hilo, Bw. Mushi, Mwenyekiti wa bodi ya soko ambaye pia ni diwani wa kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, Mh.Masaba, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, na Mh. Nderaikindo Kessy
Mvuvi akieleza maoni yake mbele ya wabunge hao.
Shughuli za samaki zikiendelea kwenye moja ya mabanda ya soko hilo.
Mh. Makongoro Nyerere (kulia), akizungumza. Kushoto niMwenyekiti wa Bodi ya soko ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kivukoni, Mh. Masaba.
Kijana akiwa amebeba samaki wakubwa baada ya kuwatoa magamba
Kijana akiwa amebeba samaki kuelekea mahala pa kutolea magamba
Mh. Mwinyi akipeana mikono na meneja wa soko hilo, Bw. Mushi

photo , , , ,


Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Je, kuna wakati utafika misingi ambayo taifa hili lilijengwa kwahiyo, itapitwa na wakati? Je, tuachane na mbio za Mwenge kwa sababu za gharama kuwa kubwa - wengine wanasema mwenge ni Jipu na Rais Magufuli alitumbue? Au Mbio za Mwenge zina umuhimu na ni sehemu ya msingi ambao taifa hili lilianzishwa na ni kumbukumbu ya mapambano ya kumletea mabadiliko na maaendeleo Mtanzania? Yote haya nitayatolea ufafanuzi kwenye Penyenye Fupi Fupi.


Falsafa ya Mwalimu Julis Kambarage Nyerere kuhusu mwenge wa Uhuru ilikuwa ni: “Sisi Watanganyika, tunataka  kuuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau”.

Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Ikumbukwe kwamba falsafa hii ni sehemu ya misingi ya Taifa letu..tangu ilipoanzishwa na waasisi wetu. Mataifa yaliyoendelea yameendelea kuenzi misingi iliyojenga Mataifa hayo kwa gharama zozote zile. Tutakubaliana sote kuwa Watanzania bado tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye ujinga, maradhi, na umaskini. Tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye dhuruma na chuki ambazo, ukizingatia dhana ya mazingira na wakati, zimekuwa ni tofauti zaidi ukilinganisha na wakati wa Uhuru. Japokuwa wakati wa Uhuru kulikuwa na dhuruma, ufisadi, chuki nakadharika, bado hata sasa hivi tuna ufisadi, dhuruma na chuki tena zilizoenda mbali sana. Katika dhama hizi za Magufuli, zilizotofauti kabisa na nyakati za Kikwete, Mkapa, Mwinyi na zile za wakati wa Baba wa Taifa. Tumejionea uozo wa hali ya juu kuliko ambavyo tumewahi kushuhudia. Neno hili siyo geni tena kwetu – “Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi”.  Mwenge wa Uhuru unapaswa kutukumbusha kila mara kuwa vita dhidi ya ubadhirifu, chuki, na dharau bado inaendelea. Tena falsafa ya Mwalimu ilikuwa inataka huu Mwenge umulike hadi nje ya mipaka yetu. Hii inanipeleka kwenye penyenye yangu inayofuata – Kuingiliwa kwa Uhuru wa Taifa letu na Mataifa ya Magharibi.

Tutakumbuka kuwa hivi karibuni sakata la MCC 2 lilishika kurasa nyingi sana. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar na kuhusiana na ile sharia ya makosa ya Kimtandao. Taasisi ya MCC ni kibaraka wa umagharibi, pia ina kila lengo la kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu. Maitaifa ya Magharibi kuingilia mambo ya ndani ya nchi za kiafrika limekuwa ni jambo la kawaida sana. Tumekuwa ni nchi ya amani isiyokiuka haki za binadamu, sasa kuiingiliwa kwenye mambo ya ndani ya nchi ni jambo linakiuka hadhi yetu ya kuwa Sovereign State. Mwenge wa Uhuru unatukumbusha maneno ya Mwalimu Julius Nyerere kuwa “… tunataka kuuwasha Mwenge na kuuweka juu yam lima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu...” Je msingi huu wa kuanzishwa kwa Taifa letu umepitwa na wakati, hasha.. msingi huu bado uko na unaendelea. Na kama taifa lazima tusimame kidete. Mwenge huu inabidi tuumulike ili sisi kama Watanzania tujikumbushe, na hayo mataifa ya nje yaliyo karibu nasi na yaliyo Magharibi au Mashariki. Pia ninaungana na kauli ya Mh. Rais Dk. John Joseph Magufuli kuwa ni bora kuishi kwa kula mihogo kuliko kula mkate ya masimango.

Je, kuna wakati utafika misingi ambayo taifa hili lilijengwa kwayo, itapitwa na wakati?

Mwalimu Julius Nyerere, alipohutubia Watanganyika kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu wa Tanganyika, alielekeza kuwa Tanganyika iko vitani dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini. Ni nukuu baadhi ya maneno yake: “…matatizo haya, hayanitishi mimi, hayawatishi wenzangu, na wala hatuombi kwamba yawatisheni ninyi. Tunayaona kwamba ni jaribio tu…Mara nyingi sana, nimesema nayi juu ya umaskini, ujinga, na maradhi, lakini kwa kweli adui yetu mkubwa ni umaskini. Tukiweza kumshinda adui huyu, tutakuwa tumeweza kupata silaha itakayotuwezesha kuushinda ujinga na maradhi. …tunaweza kupigana vita vya umaskini. Namuomba kila raia wa Tanganyika, aape kiapo cha kuwa adui wa umaskini. Amshambulie adui huyo mahali popote atakapoonekana.”

Japokuwa Tanganyika ilipata Uhuru wake bila mapambano dhidi ya mkoloni yaliyohusisha kumwaga damu. Msingi tuliachiwa na Baba wa Taifa ni kuwa nchi iko kwenye mapambano dhidi ya umaskini. Kila Mtanzania anapaswa kuwa vitani wakati wowote. Nikiiweka hoja hii kwenye muktadha wa Mwenge wa Uhuru ambao unajengwa kwenye msingi wa kumulika ubadhirifu na dhuruma. Tumeshuhudia ambavyo viongozi au watumishi wetu katika kada mbalimbali wakiwa mstari wa mbele kwenye ubadhirifu wa mali za umma. Kuingia mikataba isiyokuwa na tija wala maslahi ya Taifa. Watu hawa wamekuwa wakiturudisha nyuma sana kwenye vita dhidi ya umaskini ambao mwalimu alitutaka kila Mtanzania kuapa kupambana nao kila sehemu atakapoukuta. Ila katika juhudi za Mtanzania maskini kujitafutia njia za kutoka kwenye umaskini na wengine kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi, wachumia tumbo wamekuwa na mtindo wa kujinufaisha wao na vizazi vyao. Kinyume kabisa na misingi ya Taifa letu. Kila Mtanzania akiwa vitani dhidi ya umaskini inamaanisha kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato na serikali itatimiza wajibu wake kuwaletea wananchi bidhaa za umma. Ndiyo maana katika dhama hizi za Magufuli utumbuaji wa majipu unaturudisha kwenye ile vita dhidi ya dhuruma, ufisadi, na uonevu. Mwenge lazima uendelee kumulika, falsafa na itikadi ya kuwa tuko katika mapambano lazima iendelee kumulikwa.

Je, tuachane na mbio za Mwenge kwa sababu za gharama kuwa kubwa - wengine wanasema mwenge ni Jipu na Rais Magufuli alitumbue? Au Mbio za Mwenge zina umumhimu na ni sehemu ya msingi ambao taifa hili lilianzishwa kwayo na ni kumbukumbu ya mapambano ya kumletea mabadiliko na maaendeleo Mtanzania?

Kama nilivyelezea hapo juu nia, falsafa na matokeo ya kuwepo kwa mbio za Mwenge wa Uhuru bado hazijabadilika. Changamoto ambazo zilikuwepo wakati wa Uhuru wa Tanganyika, bado zipo katika kipindi cha Tanzania ya karne ya 21, na inawezekana Tanzania ya vizazi vijavyo itakutana na changamoto zinazofanana na hizi lakini kadika mazingira na wakati wa vizazi vya wakati huo.

Kama Taifa misingi ya kuanzishwa kwa Taifa lazima iendelezwe, kwani wanaosema kuachana na misingi hiyo huwezi fahamu ajenda yao iliyojificha ni mimi. Taifa lisilo na misingi ya kuanzilishwa kwake ni dhaifu. Taifa linaloweza kutupilia mbali misingi ya kuanzilishwa kwake, linaweza kuwa katika hatari kubwa sana ya siku moja kutoweka, au kuingia katika virugu na matatizo ambayo ni vigumu kuweza kurudi katika hali ya awali. Bado tunaihitaji misingi ya Taifa letu. Bado tunaipenda misingi ya Taifa letu. Gharama ya mbio za Mwenge siyo hoja, maana misingi ya kuanzishwa kwa Taifa lazima ilindwe kwa gharama zozote zile. Ufisadi uliokuwa unaendana na kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru ndiyo unaotakiwa kupigwa vita kwa juhudi zote. Mwenge kwa sababu unamulika na kuangaza palipo na ufisadi, udharimu, dharau, na chuki. Mbio za Mwenge wa Uhuru zitumike kutumbulia kila linapokuwa limemulikwa jipu, kwenye miradi ambayo imekuwa ni utamaduni kutumika kuizindua nchi nzima yaani mikoa 31 na Halimashauri 173.

Kumbukumbu ya kumletea Mtanzania mabadiliko ya kiuongozi na uundwaji wa mfumo wa utawala bora utakao ridhishwa kizazi hadi kizazi, ni jambo linalopaswa kuwa sehemu ya ujivuni wa kuwa na Mwenge wa Uhuru. Mwenge ni alama ya Uhuru wetu kuona mapungufu yetu. Mwenge ni alama ya kutuunganisha Watanzania na kupambana na uovu, udharimu, wizi, na ufisadi. Mwengi ni alama ya Uzalendo na kila Mtanzania nia akiuona anapaswa kuukumbuka wakati wa uhai wake wote, na kuwafundisha watoto na watoto wa watoto wake kuwa hiyo ndiyo ishara ya Uzalendo wa Mtanzania. Ndiyo ishara la tumaini la Mtanzania lilioanza tangu na kabla baada ya kupata Uhuru na lilikuwepo kabla ya kupata Uhuru. Wanaoupiga vita Mwenge wa Uhuru wamepoteza tumaini na wanataka Watanzania nia pia wapoteze tumaini pamoja nao. Ninachoamini mimi ni kuwa mtu aliyepoteza tumaini safari yake inapaswa kuishia kaburini. Tena kwa sisi tuliona tumaini la kizazi hiki na kutambua ukuu wa Mungu, tunaamini hata baada ya Kaburi tunatumaini kuwa siku moja tunauna uso wake. Sasa iweze sisi Watanzania tukubali mawazo haya finyu kuwa Mwenge ni Jipu, ninadhani kupoteza Tumaini ni Jipu, na dawa ya jipu ni kulitumbua na Mwenge unamwangaza kwa kutosha kumulika wakati wa Utumbuaji wa Jipu hilo.

Mnyela Jonathan N.

photo , ,


Bi Ritha Mushi (VSO Volunteer) akiongea na Vijana wenzake juu ya umuhimu wa kujitolea katika kongamano la siku ya kujitolea duniani lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Bw. Ian Tarimo anaejitolea katika Shirika lisilo la Kiserikali la Youth For Change akiongea na Vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Dr Ven kutoka DFID akiwaasa vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kijana akipata maelezo juu ya utendaji kazi wa shirika lisilo la Kiserikali la JICA wakati wa kongamano la siku ya kujitolea lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kulia akiongea na wanahabari katika maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Overseas (VSO) Dkt. Philip Goodwin.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliyevaa suti akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

photo , ,


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Algeria
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars".
Mshambuliaji machachari wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu, akionyesha umahiri wake wa kuwatoka mabeki wa timu ya Taifa ya Algeria, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Algeria, Guediora Aldane akiondoka na mpira mbele ya beki wa Timu ya Taifa Stars, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Timu ya Algeria, Ghoulam Faouzi, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Mlinda Mlango wa timu ya Taifa ya Algeria, M'bolhi Rais akipiga shuti kuondosha mpira langoni mwake.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta akiangalia namna ya kuwatoka mabeki wa timu ya Taifa ya Algeria, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.

Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars wakishangilia ushindi wao wa awali, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.





















photo , ,