Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Algeria
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars".
Mshambuliaji machachari wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu, akionyesha umahiri wake wa kuwatoka mabeki wa timu ya Taifa ya Algeria, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Algeria, Guediora Aldane akiondoka na mpira mbele ya beki wa Timu ya Taifa Stars, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Timu ya Algeria, Ghoulam Faouzi, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.
Mlinda Mlango wa timu ya Taifa ya Algeria, M'bolhi Rais akipiga shuti kuondosha mpira langoni mwake.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta akiangalia namna ya kuwatoka mabeki wa timu ya Taifa ya Algeria, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.

Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars wakishangilia ushindi wao wa awali, wakati wa Mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kwenye Mashindano ya Kombo la Dunia ya Mwaka 2018, katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Hadi mwisho wa mchezo, Timu zote zimetoka suluhu ya kufungana Bao 2-2.





















photo , ,



 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(katikati)Akizungumza na Wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya kusafiri umbali mrefu Duniani Mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwenye Ofisi za Alliance Autos,Kulia ni Meneja mkuu wa Alliance Motors Bwana Wayne Mcintosh na kushoto kwake ni Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed

  Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(Wa Kwanza Kulia)akiwaelezea jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed
 Meneja mkuu wa Alliance Motors Bwana Wayne Mcintosh akielezea ni kwa namna gani magari yao yako imara kuhimili masafa marefu akitolea gari ya Volsk Wagen Aliyosafiri nayo Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(Martha Magessa)
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu ya kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI


 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
 Gari aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI inavyoonekana kwa ndani

 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh(wa pili toka kulia)wakipata picha ya pamoja na wanahabari
 

Meneja Mkuu wa Alliance Autos Wayne Mcintosh(kushoto) Akipata picha na Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof


 Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed(kushoto)akipata picha na Dereva Rainer Zietlof



Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh akisoma cheti cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka ujerumani 
-----------------------------------------

DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka 2011 na 2012.
Awali alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama 'Panamerica'ambayo ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17 wakati ile ya 'Russtralia' ilimtoa Melbourne, Australia hadi St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa 17,000.
Kwa mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na sasa Tanzania.
Dereva huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya Alliance Autos iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha, amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na barabara mbovu.
Mradi huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa na makampuni makubwa ya magari ya Tehama na Volkswagen nchini Ujerumani, Slovakia na Afrika Kusini.
Katika safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye ni mpiga picha na mchukua video huku Matthias Prillwitz ni mzoefu wa mbio
za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.

photo ,


Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 20 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (wapili kulia) ikiwa ni mchango wa IPTL kusaidia maandalizi ya Tuzo za wanamichezo bora nchini. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni ni Makamu Mweyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko, Katibu Mkuu, Amir Mhando na Mwanasheria na Mshauri Mkuu wa IPTL,Joseph Makandege na kulia ni Mjumbe wa TASWA, Rehure Richard Nyaulawa
 Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akizungumza na wanahabari baada ya kupokea fedha hizo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth akiwaeleza wanahabari furaha yake ya kuisaidia TASWA kitita hicho cha fedha kusaidia wanamichezo ambapo nae alikiri kuwa ni miongoni mwa wanamichezo na amewahi kuwa Mshindi wa tatu wa Mbio za Magari Afrika.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (katikati) akiwaongoza wanahabari kuangalia mitambo ya Kampuni hiyo ambayo inazalisha umeme. Kulia ni Katibu mkuu wa TASWA, Amir Mhando na Kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
Waandishi wa habari wakiingia kuangalia uzalishaji wa umeme katika mitambo ya IPTL.

photo , ,

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akiwakaribisha wageni walioalikwa katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel, akiongea machache katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akiongea akiongea katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Mshehereshaji wa Hafla hiyo Elisha Elia akiongea machache.
Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere akitoa shukrani zake kwa niaba ya wasanii katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mboni Masimba, Mbunge wa Temeke Mh. Abbas Mtemvu pamoja na mchambuzi wa Mpira Manara katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Wasanii walioalikwa wakipakua chakula (futari) iliyoandaliwa katika hafla hiyo.
Wasanii mbali mbali walioungana katika hafla hiyo wakipata futari.
Wafanyakazi wa TBC hawakuwa nyuma kujipongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Wasanii wakifurahia jambo na Mchambuzi wa Mpira, Mw. Kashasha.
Msanii JB akiongea na Mchambuzi wa Mpira wa Miguu, Mwl. Kashasha.
Wasanii wakijadili mambo.
Dokta Cheni akishow love.
Mw. Kashasha nae alikuwepo.
Meza kuu kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana, Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtemvu, Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia pamoja na Mdau mkubwa wa Michezo, Juma Kipingu wakifuatilia mpira wa fainali ya kombe la dunia 2014, kati ya Argentina na Ujerumani
Wasanii wakifuatilia kwa makini mpira huo.
Wafanyakazi wa TBC nao hawakuwa nyuma.
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakipongezwa kwa kazi waliyoifanya.
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

photo , ,