Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais
Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa
la viongozi na watu mashuhuri baada ya Kuadhimisha Kumbukumbu
ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani,
Mheshimiwa Nelson R Mandela leo Desemba 10, 2013 katika uwanja wa FNB
jijini Johannesburg.Picha na IKULU
---
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani
na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha
aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R
Mandela.
Maelfu
kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu
kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye
alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa
Afrika Mashariki.
Mheshimiwa
Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013, alikuwa
Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National Congress la Umkhoto
we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na utawala wa Makaburu.
Baada
ya kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa
Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela alitumikia
kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia kipindi cha pili.
Kiasi
cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo iliyokuwa na
kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na majonzi na wengine
wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo iliyochukua kiasi cha jumla
ya saa tano.
Mbali
na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine
mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack Obama wa
Marekani, Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza,
Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon.
Kumbukumbu
hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais watatu
wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill Clinton na
Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Uingereza,
Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.
Rais
Kikwete kesho, Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi wenzake katia
katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu Mandela ambao
utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union Buildings mjini Pretoria.
0 Responses so far.
Post a Comment