Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa
TANROADS mkoani Morogoro. Waziri Magufuli amewapongeza TANROADS kwa
utendaji kazi wao mzuri ujenzi wa Barabara nchini.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma risala
kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli.TANROADS
imepata TUZO ya mfanyakazi bora na mwajiri bora kutoka TAMICO.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa ameshikana mikono na
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara, TANROADS Eng. Patrick Mfugale
kushoto pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe kulia
wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya ufunguzi wa Baraza la
Wafanyakazi wa TANROADS.
Baadhi
ya Wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wakisikiliza kwa makini hotuba ya
mgeni rasmi katika ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia tuzo aliyokabidhiwa na
Wafanyakazi wa TANROADS kwa kutambua uongozi wake bora katika kuanzisha
na kule Wakala huo tangu mwaka 2000-2015.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mara baada ya mkutano
uliofanyika mkoani Morogoro.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Dkt. Rajabu Rutengwe mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi wa TANROADS mkoani Morogoro. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
Waziri
wa Ujenzi DKT, JOHN MAGUFULI amewataka wafanyakazi wa Wakala wa
Barabara nchini (TANRODS), kufanyakazi kwa ubunifu,uzalendo na uadilifu
ili kuharakisha maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Akifungua
mkutano wa tano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mjini Morogoro
Waziri Magufuli amesema asilimia 14.3 ya pato la taifa linatokana na
kukua kwa sekta ya usafirishaji ambayo asilimia 99.3 ya usafirishaji
wote nchini unatumia barabara.
“Ni
asilimia 0.7 tu ya bidhaa zote nchini zinatumia usafiri wa anga,reli na
bahari hivyo ni wazi kuwa sekta ya barabara ni nguzo muhimu ya uchumi
wa nchi”, amesisitiza Waziri Magufuli.
Waziri
Magufuli ameipongeza TANROADS kwa mafanikio iliyoyapata katika kipindi
cha miaka 15 tangu ianzishwe na kufanikiwa kuwa mwajiri bora wa TAMICO
mwaka 2014/2015.
Naye
mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe amepongeza TANROADS mkoani
Morogoro kwa kazi nzuri wanazofanya na kuitaka kushirikiana na taasisi
nyingine katika kudhibiti ajali za barabarani.
Amehimiza
umuhimu wa TANROADS kudhibiti magari yanayoegeshwa kiholela barabarani
na kuongeza mizani zinazotembea ili kudhibiti uharibifu wa barabara
unaosababishwa na magari kuzidisha uzito.
Akizungumza
katika Baraza hilo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS na Mwenyekiti wa Baraza
hilo Injinia Patrick Mfugale amewataka wajumbe kuwa huru ili kuwezesha
kujitathmini kwa haki na hivyo kuongeza tija katika utendaji kazi.
Injinia
Mfugale amewataka Wahandisi kuwa wabunifu na wanaozingatia thamani ya
fedha ili miradi ya ujenzi idumu kwa muda mrefu na kuchochea maendeleo
ya nchi.
Amesema
TANROADS imechaguliwa kuwa ya tatu kwa utendaji bora wa kazi kwa
taasisi za ujenzi barani Afrika ikitanguliwa na nchi za Afrika Kusini na
Namibia.
TANROADS
ilianzishwa mwaka 2000, kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa barabara kuu
na za mikoa hapa nchini ambapo hadi sasa inasimamia ujenzi wa barabara
zenye urefu wa kilomita 35,000.
0 Responses so far.
Post a Comment