Pichani
juu na chini ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Dkt.Seif Rashid akizungumza
wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa
Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani
humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee akizungumza katika kongamano
la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya
ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo
ni ''Tanzania
na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kabla ya uzinduzi wa kongamano
hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya
afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha
uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo
kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36
zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema
mwakani.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto
akifafanua jambo kwenye kongamano la tisa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), na Waandishi wa habari lililofanyika leo katika moja ya
ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya Kongamano hilo
ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya kutoka wilaya mbalimbali walioko mezani mbele
wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano
hilo la tisa la NHIF,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Afya,Mh.Dkt
Seif Rashid ndiye aliyezindua kongamano hilo lililohudhuriwa na
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee na pichani kati ni Mgeni
rasmi Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid wakifuatilia na kusikiliza kwa
makini baadhi ya maswali na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa
na washiriki wa Kongamano hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahya Nawanda akizungumza mbele ya washiriki wa
kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mmpango
mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana
na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika
suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya
Pichani
ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili
linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani
ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo la siku mbili
linalofanyika mkoani Dodoma.
Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zikijadiliwa ndani ya kongamano hilo mapema leo mchana.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto,Kaimu Mkurugenzi wa Tiba
na Ushauri wa NHIF,Bwa.Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF) wakiwa kwenye kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma.
Pichani
ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili
linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani
ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima
(RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki
kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa
Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya
Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa
na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
0 Responses so far.
Post a Comment