Njiani kuelekea Kata ya Mvuha iliyopo katika Wilaya ya Morogoro (Vijijini)
Mwanasheria Amani Mwaipaja akiwa katika picha ya pamoja na Aliyekua Mwenyekiti wa Kijiji cha Mvuha (Morogoro Vijijini)Bwana Nyandikira muda mfupi baada ya kuwasili Katika kata ya Mvuha
Jengo la Ofisi ya Kata ya Mvuha likionekana kwa mbali
Mto Mvuha (Uliopo Morogoro Vijijini) ukiwa umefurika katika kipindi hiki cha msimu wa mvua
Washiriki wakiwa katika majadiliano ya vikundi wakati wa semina
Habari Kamili
Mwanasheria na Mtafiti Amani Mwaipaja ameanzisha program ya msaada wa kisheria kwa jamii iishiyo pembezoni mwa nchi ya Tanzania (Vijijini) Kwa lengo la Kuhamasisha Vijana-Wasomi kutumia Elimu na Rasilimali walizonazo katika kufanya kazi za kujitolea kusaidia jamii. Program hiyo imepewa jina la Jamii Kwanza.
Program ya Jamii Kwanza inatoa semina, mafunzo na kusambaza elimu kwa njia ya vitabu ili kuhakikisha kuwa jamii kubwa iishiyo vijijini inatambua haki mbalimbali ilizo nazo kwa mujibu wa sheria za Tanzania
0 Responses so far.
Post a Comment