Mwenyekiti
wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama (liesimama)
akitoa muongozo wa namna vikao vitakavyokuwa vinaendelea kufanyika
katika kumbi mbali mbali ndani ya Hoteli ya Malaika,iliwa ni muendelezo
wa Kongamano Uwekezaji Kanda ya Ziwa,unaoendelea kufanyika kwenye
Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.Wengine pichani toka kushoto ni Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo,Mh. Everist Ndikilo,Naibu Waziri
wa Nishati na Madini,Mh. Charles Kitwanga pamoja na Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza.
Mwenyekiti
wa Kikao kinachojadili maswala ya Ufugaji katika Kongamano la Uwekezaji
Kanda ya Ziwa,Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani
(katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kikao hicho (hawapo pichani) wakati
akitoa muongozo wa kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa
katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mh. Said Magalula na Kulia ni Meneja wa Kituo cha
Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Bw. Fanuel Lukwaro
Mtoa
Mada iliyohusu Fursa za Uwekezaji katika Ufugaji na Michakato ya kuwa
na Machinjio bora,Prof. Lazaro Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine
(Idara ya Sayansi ya Wanyama) akisisitija jambo wakati akiwasilisha mada
yake hiyo,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea
kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya
Malaika,jijini Mwanza.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano la Uwekezaji Kanda
ya Ziwa,Mh. Everist Ndikilo akifatilia kwa makini kikao hicho
kinachoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli
ya Malaika,jijini Mwanza.
Wajumbe wakifatilia kikao hicho.
Mwenyekiti
wa Kikao kinachojadili maswala ya Kilimo katika Kongamano la Uwekezaji
Kanda ya Ziwa,Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha
Chiza (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kikao hicho (hawapo pichani)
wakati akitoa muongozo wa kikao hicho kinachoendelea kufanyika hivi sasa
katika Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Shinganga,Mh. Yohana Balele.
Naibu
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mh. Aggrey
Mwanri (wa pili kulia) akiwa pamoja na Wajumbe wengine kufatilia moja ya
vikao vinavyoendelea kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya
Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbu wa Mikutano wa
Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Wajumbe wakipitia makabrasha mbali mbali ya Kongamano hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto)
akizungumza wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu uwepo wa Fursa za
Uwekezaji katika
Uwindaji na Hoteli wakati wa Kikao kilichokuwa kikijadili maswala ya
Miundombinu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Elimu na Afya katika Kongamano
la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye
Ukumbu wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Picha na Othman
Michuzi,Mwanza.
0 Responses so far.
Post a Comment