Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe,
amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa
kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na
kijamii.
Mhe.
Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha
Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia
kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana
kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.
Alielezea
kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo
hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu
wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.
Mhe.
Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza
jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
Brass
Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa
cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali
Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na
Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu hicho katika
sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe
21.11.2014.
Mhe.
Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia
katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha
Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa
Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi (mwenye kofia ya njano) akiwa
pamoja na mgeni rasmi Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa
wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa
mahafali hayo ya kumi na moja.
Shekhe
Dr.Badruh H.Sseguja akifungua kwa sala Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam
tarehe 21.11.2014
Mchungaji Ogah Ogbole akifungua kwa sala mahafali ya kumi na moja ya
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam
tarehe 21.11.2014
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Profesa Mohamed Ndaula
akitoa hotuba ya ufunguzi wa mahafali hayo ya kumi na moja ya chuo
hicho Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wahitimu wa fani mbalimbali wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala
Kampasi ya Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwa utulivu tayari kabisa kwa
ajili ya sherehe za mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho ambapo jumla
ya wanafunzi 902 walihitimu masomo yao.
Baadhi
ya wakuu wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala
wakiingia katika viwanja vya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam tayari
kwa mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho.
Mkuu
wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi
akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja.
Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo
ya kumi na moja ambapo aliwaasa kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutii
sheria za nchi.
Baadhi
ya wahitimu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala wakinyanyua kofia
zao juu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali yao ya kumi
na moja ya chuo hicho.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo wakifuatilia hatua kwa hatua kile kinachoendelea katika sherehe hizo.
Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala akitunuku shahada kwa wahitimu wa mahafali hayo.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan
Mwinyi ( mwenye joho la njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Membe
pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo wa taifa kama
ishara ya kufunga mahafali hayo ya kumi na moja.
Mgeni rasmi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali hayo. PICHA NA Reuben Mchome
0 Responses so far.
Post a Comment