Showing posts with label KIFO. Show all posts
Showing posts with label KIFO. Show all posts

 Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi wa Magereza (SACP) Annethy Laurent.
 Mwili wa Marehemu Anneth ukiwasili katika Kanisa Katoliki Parokiani Segerea. Walio mbele ni Pamela  (mtoto wa dada yake na Marehemu) na aliyebeba picha ni mtoto wa Pamela ( Mjukuu wa Marehemu). Walioshika jeneza kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Dk.Kato Rugainunura, kulia ni Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Magereza Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Rajab Nyange
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati wa ibada ya kumuombea Marehemu.
 Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Mallya akitoka salaam za Jeshi la Magereza kwa wafiwa kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa  Magereza John C. Minja.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga akitoka salaam za pole kwa wafiwa kwa niamba ya Kamati yake ambayo pia aliongozana nayo katika msiba huo (hawapo pichani)
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga(Mwenye miwani) akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. Wa pili ni Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akifuatiwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakhim Maswi wakitoa salaam zao za mwisho.
Mwili wa  Marehemu Anneth ukiwasili katika kanisa katoliki parokiani Segerea tayari kwa misa takatifu ya kumuombea marehemu.
PIX 8: Baada ya misa takatifu  msafara wa kuelekea makaburini ulianza ukiongozwa na Kamishina Jenerali wa Magereza (CGP) John Minja.
Picha zote na Mkaguzi wa Magereza Moses Sebastian
Makao Makuu ya Magereza.

photo , , ,


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mh Said Mecky Sadick akiongea wakati wa msiba wa Marehemu George Otieno (Tyson) leo kwenye viwanja vya leaders ambapo wakazi wa Jiji la Dar Walijitokeza kwaajili ya Kutoa Heshima zao za Mwisho kwa Marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Kenya Kwa Mazishi
 Mtoto wa Kwanza wa Marehemu George Otieno (George Tyson) wa kwanza kushoto akiwa na majonzi yakuondokewa na baba yake kipenzi huku Mama yake naye akiwa mwenye huzuni tele na simanzi.
Mwakilishi wa Wanahabari kutoka TV1 ambapo Marehemu alikuwa mfanyakazi katika kituo hiko cha Runinga akiongea machache kabla ya kutoa heshima za mwisho
 Mama Mkwe wa Marehemu George Tyson, Natasha akielekea kuketi upande wa meza kuu. Natasha ni mama mzazi wa Aliyekuwa Mke wa Marehemu George Tyson ajulikanae kama Monalisa
 Mboni Masimba akielekea jukwaa kuu kwaajili ya kuketi
 Mwimbaji wa Nyimbo za injili akiimba wimbo kwaajili ya kuwafariji wafiwa wote katika viwanja vya leaders mapema
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ambapo Marehemu kwa kusaidia na Mboni Masimba walikwenda kutoa Msaada wa madawati katika shule hiyo Mkoani Dodoma na mauti kumfika wakati wakitoka Mkoani Dodoma
 Wafanyakazi wa TV 1
 Baadhi ya Wafanyakazi wa TMT wakiwa na majonzi
 Mke aliyekuwa akiishi na Marehemu
 Umati wa Waombolezaji
Mwakilishi wa Wasanii Kutoka Morogoro
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam akitoa heshima za Mwisho
.Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

photo , ,


Mwandishi wa habari na mmiliki wa blog ya Bertha Blog Bi. Bertha Mollel (wa kike mbele) akibeba jeneza lenye mwili wa mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara, marehemu Fortunatha Ringo aliyefariki dunia Januari 10 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa ugonjwa wa kuishiwa damu na kuzikwa Januari 13 kwenye kijiji cha Mdawi Old Moshi.
Jeneza lenye mwili wa mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara, marehemu Fortunatha Ringo aliyefariki dunia Januari 10 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa ugonjwa wa kuishiwa damu, likiingizwa kaburini na kuzikwa Januari 13 kwenye kijiji cha Mdawi Old Moshi.
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoa wa Manyara, Joseph Lyimo (kushoto) na Meneja wa Radio Safina ya Arusha, Jovin Msuya wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Fortunatha Ringo, mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara aliyefariki Januari 10 jijin Dar es salaam na kuzikwa Januari 13 kijijini Mdawi Old Moshi. Na Wazalendo 25 Blog

photo

Picha ya Maktaba ikimwonyesha Waziri wa Fedha, marehemu Dk William Mgimwa akisoma bajeti ya wizara yake bungeni. 

Dar es Salaam na Iringa. Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga (CCM), Iringa, William Mgimwa amefariki dunia jana katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic, Pretoria, Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.
Habari zilizopatikana jana kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kupitia kwa Msemaji wake, Habib Awesi zilisema Waziri Mgimwa amefariki dunia mchana... “Ni kweli amefariki leo mchana tumepeleka taarifa Ikulu, Dar es Salaam.”
Baadaye jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alithibitisha kupokea taarifa za kifo hicho na kusema Waziri Mgimwa alifariki dunia saa 5:20 kwa saa za Afrika Kusini (saa 6:20).
“Kinachofanyika kwa sasa ni maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa marehemu na hilo linafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake. Taarifa zaidi zitatolewa baadaye kadiri zitakavyopatikana,” alisema Balozi Sefue.
Akizungumzia msiba huo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema: “Bunge limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Dk Mgimwa, alikuwa ni mtu mwaminifu katika kazi zake na alishirikiana kikamilifu na wabunge katika kutekeleza kazi za Serikali. Taifa limepoteza mtu makini aliyefanya kazi katika sekta ambayo aliisomea, jambo ambalo lilimfanya awe na ufahamu mzuri wa mambo katika wizara (Fedha),” alisema Ndugai.
Kikwete atuma rambirambi
Jana jioni Rais Jakaya Kikwete alitoa taarifa akielezea kushtushwa na kifo cha Waziri Mgimwa.
“Nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa,” ilisema taarifa yake kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu.
Alisema taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
Katika salamu zake kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kwa familia ya marehemu Mgimwa, Rais Kikwete alisema: “Sina maneno ya kutosha kuelezea mshtuko na huzuni yangu kubwa kufuatia taarifa za kifo cha Mgimwa.
“Binafsi nilimtembelea mara mbili hospitali alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia yake na tamaa yake ya kurejea nyumbani kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.
“Sote tunajua mchango wake katika Serikali. Sote tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya ni mapenzi ya Mungu... Natoa pole nyingi na rambirambi zangu za dhati kwa wana familia wote kwa kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi katika kuomboleza msiba huo mkubwa. Napenda mjue kuwa msiba huu ni msiba wangu pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,” alisema Rais Kikwete.
Jimboni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Vijijini, Steven Muhapa alisema jana kuwa wamepokea kwa mshituko kifo cha mbunge wao.
Muhapa alisema halmashauri yake imepata pigo la mwaka, kwani walikuwa na mipango mingi ya kutekeleza chini marehemu Mgimwa lakini sasa imeyeyuka... “Alisaidia sana kutuletelea wafadhili kutekeleza ahadi mbalimbali alizoahidi... ni mapenzi ya Mungu.”
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa alisema Mkoa wa Iringa umepoteza mtu muhimu, mahiri na mchapakazi... “Pamoja na kwamba alikuwa CCM, hakubagua mtu. Niliwahi kumpa ushauri mara kadhaa akauchukua ushauri wangu na kuufanyia kazi.”
Mwenyekiti PAC
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amemwelezea marehemu kwamba alikuwa ni mtu mnyenyekevu na hakuwa na ubaguzi katika kutekeleza wajibu wake akiwa kiongozi wa Serikali.
“Kwa kipindi kifupi nilichofanya naye kazi kwa karibu, kwanza kwenye Kamati ya Fedha, nikiwa mkaribishwa kama Waziri wa Fedha kivuli, kisha kwenye kamati ndogo niliyounda kuhusu miradi ya umeme ya Mchuchuma, Liganga na Ngaka na baadaye akiwa Waziri wa Fedha, jambo la msingi nililoliona kwake ni unyenyekevu na heshima kubwa aliyonayo kwa watu wengine.
“Hakusita kuomba ushauri licha ya kuwa na tofauti za kivyama na kwa kweli ni Waziri wa Fedha niliyeelewana naye zaidi kuliko wengine wote waliopita nikiwa ama Waziri Kivuli au Mwenyekiti wa Kamati za Hesabu.”
Imeandikwa na Raymond Kaminyoge, Florence Majani, Joseph Zablon (Dar) na Geofrey Nyang’oro (Iringa). CHANZO -MWANANCHI

photo , ,


DSC09341Mwenyekiti wa Chadema, Mh freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema wakiwa katika uwanja wa Soweto, wakati wa zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali chini ya usimamizi wa wataalamu toka Jeshini.
DSC09327
Mhe.Mbowe na Mhe. Lema wakishauriana jambo..
DSC09343Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tank hilo lilishamabuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari la matangazo lina majeraha mawili katika mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.
DSC07458
Gari ambalo linasadikiwa kutegwa bomu katika tanki la Mafuta.

DSC09360Mh. Mbowe akiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.
DSC09382James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa katika hospitali ya Seliani Jijini, Arusha.
DSC09373Mtoto Sharifa nae amelazwa hospitalini hapo kwa majeraha ya mlipuko katika hospitali ya Seliani Jijini, Arusha.
DSC09377Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bw beni akiwa majeruhi kitandani,katika hospitali ya Seliani Jijini, Arusha.Habari hii kwa hisani ya Wazalendo 25 Blog

photo , ,