Showing posts with label KILIMO KWANZA. Show all posts
Showing posts with label KILIMO KWANZA. Show all posts

Wafungwa wa Gereza Idete wakilima shamba kwa kutumia trekta kama inavyoonekana katika picha. Wafungwa hao wamepatiwa ujuzi wa kulima na trekta wakiwa gerezani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji zinazofanywa na Jeshi la Magereza hapa nchini. Kwa wastani Wafungwa hao hulima hekari 10 kwa siku.
Mkuu wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Beno Hunja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) walipotembelea Ofsini kwake Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi unaoendelea wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mradi huo unajengwa kwa kutumia fedha za ndani na utagharimu kiasi cha Bilioni 2.8 hadi kukamilika kwake hivyo kukamilika kwa mradi huo kutalifanya Jeshi la Magereza kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi kuliko hivi sasa.
Mkuu wa Gereza Idete, Beno Hunja akiwaongoza Waandishi wa Habari kutembelea eneo kunakojengwa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.
Sehemu ya Mbanio na chanzo Kikuu cha kupokelea maji yatakayotumika katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakifanya mahojiano na Mkuu wa Gereza Idete(hayupo pichani) walipofanya ziara yao ya kikazi Desemba 17, 2014 kujionea ujenzi wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji.
Mfereji ambao tayari umekamilika kujengwa katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)

photo , ,


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Kilwa Murtaza Mangungu, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Ngongo katika maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana Agosti 8, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri wa Kilimo Maendeleo ya chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza, na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Lindi wakati akitembelea katika Mabanda ya Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo Mkoa wa Lindi, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Jarida la Kilimo la Nanenane kutoka kwa Iman Kajula, kwa ajili ya kuzinduliwa wakati wa Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia kiatu huku akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mkuu wa Magereza, Yunge Saganda, kuhusu utengenezaji wa viatu hivyo wakati alipotembelea katika Banda la Jeshi la Magereza kwenye Kilele cha maonesho ya Sikukukuu ya Wakulima Nanenae iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wakazi wa mkoa wa Lindi waliojitokeza katika Viwanja vya Ngongo wakati akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja hivyo jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya watoto waliokuwapo eneo hilo, wakati akitembelea mabanda hayo ya maonesho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, wakatika Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana Agosti, 8, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Sophia , wakatika Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mwakilishi wa Balton Tanzania, wakatika Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana.

photo ,

Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.
Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya kuwasili Kijijini hapo.
Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatu kutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa wa Chakula ambao  wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.
Mwakilishi kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Teresa Yates Mwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi akiwakaribisha Rasmi wageni wote katika Kijiji cha Maisha plus pia kumkaribisha Mgeni Rasmi Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi  ili aweze kutoa hotuba yake
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa katikati akitoa hotuba yake fupi wakati wa Sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus, katika Hotuba hiyo aliwapongeza waandaaji na wabunifu wa Shindano hilo, pia Grow kupitia OXFAM kwa kuungana na Maisha Plus kuwaleta Mama Shujaa wa Chakula, Mwisho aliahidi kuongeza Milioni 5 kwa Mama Shujaa wa Chakula atakaye nyakua ushindi, Kutoa Milioni mbili na nusu kwa Mama Shujaa wa Chakula aliyepita ili zikamsaidie katika kilimo na Mwisho Kutoa Milioni Mbili kwa Washiriki wa Shindano la Maisha Plus ambao sasa wamebakia 16 mpaka mwisho wa Shindano Tarehe 18.05.2014
Mmoja wa washiriki wa Maisha Plus akisoma Jina la Mama yake ambaye atakuwa naye katika Kipindi hiki kilicho bakia cha Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
Vijana na Washiriki wa Maisha Plus wakiwa na Mama zao walezi ambao ndio wameingia Rasmi kijijini Jana 
Huyu Ndiye Mama Shujaa wa Kwanza kupata nafasi ya Kuwa Markia wa Kijiji cha Maisha Plus Mary J. Mwanga, na wa kwanza kulia ni Rais wa Kijiji cha Maisha Plus Abisai Caron kutoka kenya hapa akiwa anavishwa kofia ya utambulisho na Epheta Msiga Meneja Miradi kutoka DMB
Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi  Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi, Wakina Mama Shujaa wa Chakula, Vijana wa Maisha Plus pamoja na wadau mbalimbali waliofika katika sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula  Kijiji cha maisha Plus
Mkurugenzi Mtendaji wa DMB ambao ndio waendeshaji wa Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula Ally Masoud(Masoud Kipanya) Akitoa utaratibu wa jinsi Akina mama Shujaa wa Chakula watakavyo ishi na vijana hao katika kijiji hicho
Mama  Shujaa wa Chakula wakipata maelekezo Mbalimbali juu ya Kijiji Hicho
Moja ya Bendi Matata kutoka Bagamoyo wakiwa wanatumbuiza nyimbo Nzuri wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji Cha maisha Plus.
Wakipokea maelekezo kadha wa kadha
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014 

photo , ,