Wakili Msomi Valentine Kamugisha (mwenye shati Jeupe) akiwa na Mwasisi wa Blog hii Mheshimiwa Amani Mwaipaja ndani ya Banda la Sheria lililomo ndani ya viwanja vya maonyesho ya wakulima Nanenane Morogoro
Waikili Msomi Valentine Kamugisha akiwa nje ya Banda la Sheria
BANDA LA SHERIA LAWA KIVUTIO NANENANE
Banda la sheria lililomo ndani ya viwanja vya maonyesho ya wakulima nanenane Morogoro limekuwa kivutio kwa watu mbalimbali wakiwemo wakulima, wanafunzi na wanasheria kutokana na ukweli kuwa Banda hilo limekuwa likitoa msaada wa kisheria kwa watu mbalimbali wenye matatizo ya kisheria.
Mbali na banda la sheria kutoa ushauri kuhusu masuala ya kisheria lakini ndani ya banda hilo kuna vitabu, vijarida na vipeperushi mbalimbali vinavyohusu sheria mbalimbali za nchi yetu
+-
photo
NANENANE
Wakili Msomi Valentine Kamugisha (Wa Kwanza Kulia mwenye Shati Jeupe) akiwa na baashi ya maafisa wa Banda la Wakala wa Mbegu za Kilimo-ASA
photo
NANENANE
Ndugu Abbas Mbwela, Mjasiliamali anayechipukia akiwa katika viwanja vya Maonyesho nanenane.
photo
NANENANE
Naibu Katibu wa TASO-Kanda ya Mashariki Morogoro Bwana Dastan Lukosi akiwa amepozi nje ya Banda la Sheria alipokuwa akitembelea shughuli mbalimbali ndani ya Viwanja vya Maonyesho ya Wakulima-Nanenane Morogoro
photo
NANENANE
Bi. Joyce akitoa maelezo kwa timu ya Mwaipaja Blog juu ya matumizi ya Mafuta yatokanayo na Nazi isiyokomaa
Mtafiti akitoa maelezo ndani ya Banda la Wizara ya Kilimo Chakula Na Ushirika ndani ya Banda la Wizara hiyo
Mtafiti Joseph Mbogoni akitoa maelezo kwa wanaottembelea banda hilo
Baadhi ya watu wakiangalia bidhaa na kupata taarifa ya namna wizara inavyofanya kazi zako ikiwemo kufanya tafiti za kilimo
Baadhi ya Bidhaa zikiwa katika Banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ndani ya viwanja vya maaonyesho ya wakulima-Nanenane Morogoro 2013
photo
2013
,
NANENANE
Banda la Msaada wa Sheria lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya wakulima nanenane yanayofanyika Mkoani Morogoro. Banda hili linaendeshwa kwa ufadhili wa Mwanasheria Mshauri na Mtafiti-Amani Mwaipaja
photo
NANENANE
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(kulia) pamoja na
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand, Mhe. Sura Pong
Tovichakehaikul(kushoto)wakisa ini Mkataba wa kubadilishana Wafungwa
kati ya Tanzania na Thailand(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
photo
DIPLOMASIA
Rais Kikwete akimjulia hali mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Said Mohamed Saad.
HABARI KAMILI
Said
ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, yenye maduka
mengi makubwa ya vitu vya nyumbani ndani ya Dar es Salaam na mikoa
kadhaa ya Tanzania, anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini lakini
mmoja wa watu waliomshuhudia, amefafanua jinsi hali ilivyo mbaya.
“Ameungua sana, tunatarajia kati ya kesho au keshokutwa (wikiendi
iliyopita) atafanyiwa oparesheni ya jicho. Jamani tindikali ni mbaya
sana, usimmwagie mwenzako. Ndugu yetu ameharibika sana,” kilisema chanzo
chetu kwa ombi la kutotajwa jina gazetini, kikaongeza:
“Kila anayemjua vizuri, anapomwona anamwaga machozi. Picha za jinsi
alivyoathirika baada ya kumwagiwa tindikali zimevuja mpaka kwa familia,
ni kilio kwa ndugu. Wanawake wanalia zaidi.”
JK ATINGA HOSPITALI
Wiki iliyopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete, alikuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini
alipokwenda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini ya Afrika (SADC).
Mkutano huo ni wa Pande Tatu za SADC (Troika of SADC) na akiwa huko,
alipata fursa ya kwenda kumjulia hali katika hospitali aliyolazwa ambayo
haijajulikana jina.
Chazo chetu kilisema: “Rais Kikwete alisikitika sana. Wakati anatoka
wodini alisonya. Alionesha jinsi alivyosikitishwa na unyama aliotendewa
Said.”
photo
Majanga