morgan-tsvangirai 
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kanda ya Afrika Kusini, Bernard Membe, ameelezea wasiwasi mkubwa kuwa daftari la wapiga kura lingali kutolewa siku moja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo.
Hii ni licha ya kuwa daftari hilo kuwa kiungo muhimu kwenye uchaguzi utakaofanyika Jumatano.
Taarifa zinazohusiana
Siasa
Chama cha MDC chake hasimu wa rais Mugabe, Morgan Tsvangirai, kimesema kinajiandaa kwenda mahakamani kuweza kupata daftari hilo.
Shughuli ya kupiga kura itamaliza serikali ya Muungano kati ya MDC na chama cha rais Mugabe Zanu-PF .
Rais Mugabe anataka kugombea urais hata baada ya kuitawala nchi hiyo kwa miaka 33. Anamenyana na waziri mkuu Morgan Tsvangirai
Ikiwa imesalia siku moja kabla ya upigaji kura, hakuna chama kilichopokea sajili la wapiga kura.
Mahasimu hao wawili wakuu, wamekuwa wakigawana mamlaka tangu mwaka 2009, baada ya mkataba kuafikiwa kwa usaidizi wa muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini SADC, ili kumaliza mgogoro wa kisiasa uliosababisha vurugu za baada ya uchaguzi 2008.
Bwana Membe, ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Tanzania alisema kuwa daftari la wapiga kura sio siri kubwa na kuwa lilipaswa kutolewa zamani sana.
“lazima itolewe kwa wapiga kura ili waweze kuhakiki majina yao, waweze kujua watakapopiga kura,” alisema bwana Membe.
Katibu mkuu wa chama cha MDC Tendai Biti alisema kuwa chama hicho kitachukua hatua za kisheria dhidi ya tume ya uchaguzi ili kuweza kupata sajili hilo.
Chanzo:BBC

photo

0 Responses so far.