Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), wakizindua kwa pamoja huduma mpya ya India Desk  inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia). Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia).
Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakiwa na furaha baada ya kuzindua huduma hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.

Wadau wa Benki ya CRDB.
Wadau mbalimbali wa Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya India Deski.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya India Deski uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi mpya ya India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakisakata rhumba wakati wa hafla hiyo.

photo , ,


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati akifungua Kongamano la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la tatu la Kimataifa la Mtandao wa Wanasayansi  Vijana Duniani (YES). Aidha Kongamano hilo lililoshirikisha jumla ya wajumbe zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi pia, litajadili usimamizi wa Rasilimali mbalimbali zikiwemo Mafuta na Gesi.
 Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufungua kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya sanamu la mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akipokea zawadi ya picha ya mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto)  ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  zawadi ya ramani ya Afrika, Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, baada ya ufunguzi.

photo ,


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Kilwa Murtaza Mangungu, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Ngongo katika maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana Agosti 8, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri wa Kilimo Maendeleo ya chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza, na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Lindi wakati akitembelea katika Mabanda ya Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo Mkoa wa Lindi, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Jarida la Kilimo la Nanenane kutoka kwa Iman Kajula, kwa ajili ya kuzinduliwa wakati wa Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia kiatu huku akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mkuu wa Magereza, Yunge Saganda, kuhusu utengenezaji wa viatu hivyo wakati alipotembelea katika Banda la Jeshi la Magereza kwenye Kilele cha maonesho ya Sikukukuu ya Wakulima Nanenae iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wakazi wa mkoa wa Lindi waliojitokeza katika Viwanja vya Ngongo wakati akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja hivyo jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya watoto waliokuwapo eneo hilo, wakati akitembelea mabanda hayo ya maonesho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, wakatika Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana Agosti, 8, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Sophia , wakatika Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mwakilishi wa Balton Tanzania, wakatika Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana.

photo ,



o1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Goodluck Jonathan wakati muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani Agosti 6, 2014
o3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.o2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani Agosti 6, 2014o4
o5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.o6 o7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014o8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014oo1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Afrika wakipata picha ya kumbukumbu na mwenyeji wao Rais Barak Obama wa Marekani wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.oo3
Viongozi wa Afrika wakisalimiana kwa furaha baada ya kupata picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa zaidi na ya haraka zaidi ya Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi ya chini mno ya umeme.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi ongezeko la uzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha maendeleo ya Afrika na kuleta manufaa ya dhahiri kwa kila familia na kwa kila Mwafrika.

Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatano, Agosti 6, 2014, wakati alipozungumza kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama, ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo.

Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi hizo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa ni dhahiri kuwa bila ongezeko kubwa la uzalishaji na matumizi ya umeme Bara la Afrika halitatoka kwenye uduni.

Rais amesema kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya Kanda ya Shirika la Umoja wa Mataifa Mazingira (UNEP) “Efficient Lighting in Sub Saharan African Countries” matumizi ya umeme katika Bara zima la Afrika ni asilimia 31 tu na hivyo kulifanya Bara la Afrika kutumia asilimia tatu tu ya umeme wote duniani.

Rais Kikwete amesema kuwa ili kuelewa udogo wa matumizi ya umeme ya Bara la Afrika ni kuangalia matumizi ya nishani hiyo kwa kila mkazi wa Bara hilo na yule wa Marekani. Amesema kuwa wakati kila raia wa Marekani anatumia kilowati 13, 246 katika Afrika wastani ni kilowati 440.

Ameongeza Rais Kikwete: “Ukiondoa Afrika Kusini, matumizi ya umeme kwa kila raia wa Afrika yanateremka na kufikia kilowati 160 tu.”

Amefafanua Rais Kikwete: “Uzalishaji wa jumla wa umeme wa Bara la Afrika ni gigawati 63 ambazo ni sawa na umeme unaozalishwa na nchi moja tu ya Ulaya – Hispania. Ukiondoa Afrika Kusini, nchi zinazobakia wa Afrika zina uwezo wa kuzalisha gigawati 28 tu, kiasi ambacho kinazalishwa na nchi moja tu ya Marekani Kusini ya Argentina.”

Rais Kikwete ambaye alikuwa anafafanua jinsi utoaji huduma ulio dhahiri unavyoweza kunufaisha wananchi na kujenga mazingira ya taasisi zisizokuwa za kiserikali kushamiri, ametaja mambo mengine ya msingi ambayo ni lazima yawepo ili wananchi waweze kunufaika ikiwemo elimu, ushamiri wa sekta binafsi, sera sahihi za kiuchumi, uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa kilimo.

Pia Rais Kikwete ametaja mambo mengine muhimu yanayoweza kusaidia kuboresha maisha ya wananchi kuwa ni uendelezaji na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na kulea na kukuza demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria.

Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani, anaondoka mjini Washington, D.C., leo kwenda Houston ambako atafungua na kushiriki katika mkutano wa uwekezaji katika uchumi wa Tanzania.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

07 Agosti, 2014

photo ,

 Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
 Baadhi ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere ,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.

=======  ======= =======

HOTUBA KUHUSU UZINDUZI WA  BWERERE TAREHE 07/08/2014, UKUMBI WA MKUTANO.

Kwa jina: Peter Ngota – Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL
Ndugu, wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,
Ndugu  Waalikwa, Wafanyakazi Wenzangu wa TTCL na Watanzania wote

Habari za asubuhi.

Natumia fursa hii kuwakaribisha  wanahabari, wageni waalikwa na wafanyakazi wenzangu wa TTCL katika ukumbi huu ambapo  leo tuna tukio  muhimu la uzinduzi wa huduma mpya inayo waleta watu karibu zaidi. Ninayo furaha kubwa katika siku hii ya  pekee kuujulisha umma kuwa TTCL inatoa fursa kwa wateja wake  na umma kwa ujumla kutumia mtandao wa TTCL  kupata huduma ya mawasiliano BORA ya simu na intaneti kwa bei nafuu zaidi.  

Ndugu wanahabari ,
Siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promotion inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la  BWERERE   yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.

Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na maofisini ambao wanatumia  huduma ya malipo ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe.

Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA)  kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo.

Ndugu wanahabari, Wageni waalikwa
Mbali na hayo Promosheni hii ya BWERERE inatoa fursa kwa mteja kupata huduma mbalimbali; Muda wa maongezi wa BURE na Data kwa wakati mmoja na kwa bei nafuu sana.

Huduma hizo ni kama zifuatazo;
·       Tsh 1 kwa sekunde:- Mteja atapata fursa ya kupiga simu  kwenda mitandao mingine kwa shilingi 1 kwa sekunde. Huduma hii haina kujiunga. Kabla ya hapo, kupiga simu TTCL kwenda mitandao mingine ilikuwa ikigharimu Tsh 230 kwa dakika 1. Kwa sasa mteja wa TTCL ataweza  kupiga simu katika mitandao mingine na kuweza kuongea na ndugu, jamaa na marafiki kwa Tsh 1 moja kwa sekunde yaani kwa gharama ya shilingi sitini kwa dakika 1; Sawa na punguzo la Asilimia zaidi ya 70%

·       Bwerere Premium:- inahusisha wateja wanaotumia huduma ya intaneti kuanzia kiwango cha 2Mbps  mpaka 32 GB watapata fursa kupiga simu TTCL  kwenda TTCL  bure ndani ya mwezi, pia mteja atapata muda wa maongezi  kuanzia dakika 300 mpaka dakika 600 kupiga simu kwenda mitandao mingine ndani ya mwezi.

·       Bwerere Unlimited:- huduma hii inahusisha watumiaji wa intaneti kuanzia kiwango cha 512Kbps mpaka 2Mbps watapata huduma ya muda wa kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL kwa muda wa mwezi mzima.

·       Bwerere:- kwa watumiaji wa intaneti njia ya Broadband kuanzia 3 GB mpaka 24 GB watapata fursa ya kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL.

Tunaendelea Kupanua Wigo wa uchaguzi wa huduma za vifurushi kwa watumiaji na kuwapa fursa ya waTanzania kutumia huduma za TEHAMA kwa bei nafuu kwa maendeleo ya M-Tanzainia na Taifa.

Ndugu wanahabari
TTCL inapenda kuutarifu umma faida za simu za mezani, Simu za mezani katika mawasiliano na maendeleo kwa ujumla kama ifuatavyo;
1.     Simu za mezani zinausalama mkubwa sio rahisi kwa mtu kuingilia mawasiliano ambayo yanatolewa kwa njia ya waya yaani kitaalamu cable.

2.     Vilevile simu za mezani  ni nzuri sana kwa matumizi ya kiofisi na majumbani, ni rahisi kutambua sehemu ya ofisi au nyumba unayoishi, pia Ni simu ambazo zinakuthibitishia uwepo wa mtu unayewasiliana naye katika eneo husika.

3.     Mwisho, simu za mezani  mawasiliano yake yana ubora mkubwa na uhakika kiusikivu na kasi zaidi kwa intaneti.

Napenda kuitimisha kwa kuwakaribisha wateja wote, na  ninyi wanahabari kufurahia huduma hii ya BWERERE ambayo inakupa huduma nyingi kwa wakati mmoja.

TTCL ni kampuni pekee hapa nchini ambayo inatoa huduma za DATA, simu zenye ubora zaidi. Ni mtandao pekee ambao umeenea katika mikoa na wilaya zote nchini.

Sasa ni wakati mzuri wa kutumia na huduma hii ya BWERERE na Ufaidike zaidi na TTCL kwa UBORA wa huduma na gharama nafuu zaidi nchi nzima.

TTCL HULETA WATU KARIBU.
Na sasa niwakaribishe wataalamu wetu kwa maelezo zaidi

Asanteni kwa kunisikiliza

Peter Ngota
AFISA MKUU WA MASOKO NA MAUZO.

photo ,

 Waendeshaji wa Show ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa steji, tayari kwa kuendelea na show hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkaumbusho ya Taifa Jijini Dar Es Salaam.
 Mshiriki Ally Kiwendo ambae alikuwa ni mmoja kati ya washindi watatu kutoka kanda ya Kusini mkoani Mtwara akitoa maneno ya shukrani kwa Kampuni ya Proin Promoitons ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya kutangazwa kuaga shindano hilo kutokana na Kura kuwa chache, huku pia akiwashukuru watazamaji na wote waliompigia kura
 Joyce Kalinga Mshiriki wa Shindano la TMT ambae apia alikua mshindi kutoka Kanda ya Kati Mkoani Dodoma akitoa maneno yake ya shukrani na pia kuwashukuru wadau, Kampuni ya Proin Promotions na watazamaji na waliompigia kura japokuwa bahati haikuwa yake kutokana na kutolewa kwenye kinyanganyiro hiko kutokana na uchache wa kura kutoka kwa watazamaji
 Lulu na Joti wakitoa maelekezo kwa washiriki wawili wa Shindano la TMT ambao waliweza kutolewa katika kinyanganyiro hiko kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji wa Kipindi cha TMT kinachorushwa Kila Jumamosi saa Nne usiku.
Baadhi ya washiriki wakiwa na nyuso za simanzi kutokana na Washiriki wenzao wawili kuaga mashindano hayo.Picha zote na Josephat Lukaza.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Linaelekea Ukingoni ambapo mwisho wa Mwezi huu wa nane Mshindi mmoja wa shindano hilo la TMT ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa.
 Shindano la TMT ni shindano ambalo limekuwa likiteka hisia za washiriki pamoja na wadau na watazamaji wa kipindi hiko cha TMT ambacho kimejizolea umaarufu nchini na nje ya Nchini kutokana na Umahiri wake ambapo awali shindano hilo lilianza kanda ya ziwa Mkoani Mwanza kwaajili ya kusaka vipaji vya kweli vya kuigiza ambapo baadae safari ilielekea katika kanda nyingine za Tanzania ambapo washindi watatu kutoka kila kanda waliweza Kupatikana na hatimaye kufanya jumla ya washiriki ishirini kutokana kanda sita za Tanzania Kuwasili Jijini Dar Es Salaam, Mwishoni mwa Mwezi wa Sita ambapo waliweka kambi na kuanza kupewa mafunzo na Mwalimu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam aitwaye Dk Mona Mwakalinga akisaidia na Mwl Issa.
Washiriki Hao 20 waliweza pia kupata fursa ya kufanya filamu fupi ambazo ziliweza kupima uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kutoka darasani na hatimaye kupelekea watazamaji kuweza kuwapigia kura huku wakisaidiana na majaji wa Shindano hilo. Majaji wa shindano hilo ni Roy Sarungi, Vyonne Cherry na SIngle Mtambalike.
Mpaka sasa Jumla ya Washiriki 7 wameshatoka kwenye kinyanganyiro na kupelekea kubaki na washiriki wengine 13 ambapo washiriki watatu wanatakiwa kutoka na kubaki washiriki 10 huku kumi hao wakiwa wameingia fainali sasa ya kuzisaka zile Milioni hamsini ambazo Mshindi mmoja atajinyakulia siku ya Fainali inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi wa 8.
Ili kuweza kumbakiza mshiriki wako unachotakiwa kufanya ni Kumpigia Kura kwa wingi kupitia Simu yako ya mkononi kwa kuandika Neno "TMT" acha nafasi namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano "TMT" 00 halafu tuma kwenda 15678 au Pia unaweza kumpigia kura mshiriki umpendae kupitia ukurasa wetu wa facebook kwa kutembelea anuani ifuatayo https://www.facebook.com/tztmt.
Washiriki Kumi watakaoingia Kwenye Fainali ya Kusaka Milioni 50 watakuwa chini ya Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Usamabazaji wa filamu za Kitanzania ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents, Shindano Bora na kubwa Tanzania na la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati

photo ,


 Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kulia) akibadilishana uzoefu na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga (Kushoto) wakati alipotembelea na kukagua Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
 Maafisa wa kutoka Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Assah Mwambene (Kulia), ambaye ni Mkurugenzi wa Idara hiyo na  Afisa Habari wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi  (Kushoto)wakiandika majina yao mara walipoingia kwenye Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Wapili Kulia) akizungumza na Maafisa wa kutoka Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Assah Mwambene (Wapili Kushoto), ambaye ni Mkurugenzi wa Idara hiyo na  Afisa HabAri wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi  (Kushoto) walipomtembelea Ofisini kwake. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kushoto) akizungumza na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakati wa ziara ya ukaguzi wa vitengo vya mawasiliano serikali.
 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akiagana na ugeni kutoka MAELEZO. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya hiyo, Bw. Assah Mwambene na kushoto ni Afisa Habari wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kushoto) akibalishana kadi za mawasiliano na Mkuu wa Kitengo cha Maktaba na Nyaraka kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Ally Msovu mara alipotembelea Maktaba hiyo. Kwa mujibu wa taarifa za ubora wa Maktaba za wizara za serikali hapa nchini, Maktaba hii ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ni ya kipekee na ya kupigiwa mfano na imekuwa ikiwavutia wageni wengi wa ndani na nje ya nchi wanaoitembelea Ofisi hii. Picha zote na Saidi Mkabakuli
***********************************
Na Saidi Mkabakuli
Katika kutekeleza mkakati wa kutembelea na kukagua utendaji kazi wa vitengo vya mawasiliano serikalini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene leo ametembelea Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, pia kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Philip Mpango.
Akiwa katika ziara hiyo, Bw. Mwambene ambaye ndiye Msimamizi Mkuu masuala ya Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Serikali amesema kuwa vitengo vya mawasiliano serikali vina jukumu kubwa ya kuuelimisha umma wa Watanzania juu ya masuala mbalimbali yanayojiri kwenye ofisi zao.
Bw. Mwambene ameongeza kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa vitengo hivyo ni kutoa elimu kwa umma na taarifa sahihi kwa Watanzania ambao ndiyo waajiri wakuu wa watumishi wa umma nchini, hivyo watumishi wa vitengo husika hawana budi kukidhi haja za Watanzania kwa kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati.
“Tumieni utaalamu wenu kwa kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati Watanzania ili kuweza kutoa suluhu ya masuala mbalimbali ambayo munaweza kuyajibu,” alisema.
Akizungumza wakati alipokutana na Msemaji Mkuu wa Serikali, Katibu Mtendaji wa Ofisi hiyo, Dkt. Philip Mpango, alimpongeza na kumshukuru Bw. Mwambene kwa kutenga muda na kutembelea Tume ya Mipango, ambayo ndiyo Washauri Wakuu wa Serikali katika menejimenti ya uchumi na masuala ya maendeleo.
Dkt. Mpango aliweka bayana mkakati wa Ofisi yake wa kuwafikia Watanzania wote bila kujali maeneo yao ya kijiografia kwa kuwaelimisha juu ya mipango mbalimbali ya serikali yenye dhamira ya dhati katika kuwavusha katika umaskini miongoni mwao.
“Tuna mkakati wa kuwafikia na kuwaelimisha Watanzania juu ya masuala ya mipango na maendeleo, na naomba kuchukua fursa hii kuiomba Ofisi yako kutuunga mkono katika hili ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (TDV) 2025,” alisema Dkt. Mpango.
Kwa mujibu wa TDV 2025 ni kuivusha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

photo ,