Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha
kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya
iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo
imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za
kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
Baadhi
ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa
uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere
,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni
hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
Afisa
Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi
wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana
kwa jina la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za
kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
======= ======= =======
HOTUBA KUHUSU UZINDUZI WA BWERERE TAREHE 07/08/2014, UKUMBI WA MKUTANO.
Kwa jina: Peter Ngota – Afisa
Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL
Ndugu, wanahabari kutoka
vyombo mbalimbali,
Ndugu Waalikwa, Wafanyakazi Wenzangu wa TTCL na
Watanzania wote
Habari za asubuhi.
Natumia
fursa
hii kuwakaribisha wanahabari,
wageni waalikwa na wafanyakazi wenzangu wa TTCL katika ukumbi huu ambapo
leo tuna tukio muhimu la uzinduzi wa huduma mpya inayo waleta
watu karibu zaidi. Ninayo furaha kubwa katika siku hii ya pekee
kuujulisha umma kuwa TTCL inatoa fursa
kwa wateja wake na umma kwa ujumla
kutumia mtandao wa TTCL kupata huduma ya
mawasiliano BORA ya simu na intaneti kwa bei nafuu zaidi.
Ndugu wanahabari ,
Siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promotion inayolenga
kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina
la BWERERE yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.
Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na
maofisini ambao wanatumia huduma ya malipo
ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga
simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe.
Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji
wa vifurushi vya intaneti(DATA) kwa njia
ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza
kupata intaneti bila kikomo.
Ndugu
wanahabari, Wageni waalikwa
Mbali na hayo Promosheni hii ya BWERERE inatoa fursa kwa
mteja kupata huduma mbalimbali; Muda wa maongezi wa BURE na Data kwa wakati mmoja na kwa bei nafuu sana.
Huduma hizo ni kama zifuatazo;
· Tsh 1 kwa sekunde:- Mteja atapata fursa ya
kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa
shilingi 1 kwa sekunde. Huduma hii haina kujiunga. Kabla ya hapo, kupiga simu
TTCL kwenda mitandao mingine ilikuwa ikigharimu Tsh 230 kwa dakika 1. Kwa sasa
mteja wa TTCL ataweza kupiga simu katika
mitandao mingine na kuweza kuongea na ndugu, jamaa na marafiki kwa Tsh 1 moja
kwa sekunde yaani kwa gharama ya shilingi sitini kwa dakika 1; Sawa na punguzo la Asilimia zaidi ya 70%
· Bwerere
Premium:-
inahusisha wateja wanaotumia huduma ya intaneti kuanzia kiwango cha 2Mbps mpaka 32 GB
watapata fursa kupiga simu TTCL kwenda TTCL bure ndani ya mwezi,
pia mteja atapata muda wa maongezi kuanzia dakika 300 mpaka dakika 600 kupiga
simu kwenda mitandao mingine ndani ya mwezi.
·
Bwerere Unlimited:- huduma hii
inahusisha watumiaji wa intaneti kuanzia kiwango cha 512Kbps mpaka 2Mbps
watapata huduma ya muda wa kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL kwa muda wa mwezi
mzima.
·
Bwerere:- kwa watumiaji wa
intaneti njia ya Broadband kuanzia 3 GB mpaka 24 GB watapata fursa ya kupiga
simu bure TTCL kwenda TTCL.
Tunaendelea
Kupanua Wigo wa uchaguzi wa huduma za vifurushi kwa watumiaji na kuwapa fursa
ya waTanzania kutumia huduma za TEHAMA kwa bei nafuu kwa maendeleo ya
M-Tanzainia na Taifa.
Ndugu
wanahabari
TTCL inapenda kuutarifu umma faida za simu za mezani, Simu
za mezani katika mawasiliano na maendeleo kwa ujumla kama ifuatavyo;
1. Simu za
mezani zinausalama mkubwa sio rahisi kwa mtu kuingilia mawasiliano ambayo
yanatolewa kwa njia ya waya yaani kitaalamu cable.
2. Vilevile
simu za mezani ni nzuri sana kwa matumizi
ya kiofisi na majumbani, ni rahisi kutambua sehemu ya ofisi au nyumba unayoishi,
pia Ni simu ambazo zinakuthibitishia uwepo wa mtu unayewasiliana naye katika
eneo husika.
3. Mwisho, simu
za mezani mawasiliano yake yana ubora
mkubwa na uhakika kiusikivu na kasi zaidi kwa intaneti.
Napenda
kuitimisha kwa kuwakaribisha wateja wote, na
ninyi wanahabari kufurahia huduma hii ya BWERERE ambayo inakupa huduma
nyingi kwa wakati mmoja.
TTCL
ni kampuni pekee hapa nchini ambayo inatoa huduma za DATA, simu zenye ubora
zaidi. Ni mtandao pekee ambao umeenea katika mikoa na wilaya zote nchini.
Sasa
ni wakati mzuri wa kutumia na huduma hii ya BWERERE na Ufaidike zaidi na TTCL kwa
UBORA wa huduma na gharama nafuu zaidi nchi nzima.
TTCL
HULETA WATU KARIBU.
Na
sasa niwakaribishe wataalamu wetu kwa maelezo zaidi
Asanteni
kwa kunisikiliza
Peter Ngota
AFISA MKUU WA MASOKO NA MAUZO.
0 Responses so far.
Post a Comment