Waendeshaji
wa Show ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa
kwa steji, tayari kwa kuendelea na show hiyo iliyofanyika katika Ukumbi
wa Mkaumbusho ya Taifa Jijini Dar Es Salaam.
Mshiriki
Ally Kiwendo ambae alikuwa ni mmoja kati ya washindi watatu kutoka
kanda ya Kusini mkoani Mtwara akitoa maneno ya shukrani kwa Kampuni ya
Proin Promoitons ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT
mara baada ya kutangazwa kuaga shindano hilo kutokana na Kura kuwa
chache, huku pia akiwashukuru watazamaji na wote waliompigia kura
Joyce
Kalinga Mshiriki wa Shindano la TMT ambae apia alikua mshindi kutoka
Kanda ya Kati Mkoani Dodoma akitoa maneno yake ya shukrani na pia
kuwashukuru wadau, Kampuni ya Proin Promotions na watazamaji na
waliompigia kura japokuwa bahati haikuwa yake kutokana na kutolewa
kwenye kinyanganyiro hiko kutokana na uchache wa kura kutoka kwa
watazamaji
Lulu
na Joti wakitoa maelekezo kwa washiriki wawili wa Shindano la TMT ambao
waliweza kutolewa katika kinyanganyiro hiko kutokana na kupata kura
chache kutoka kwa watazamaji wa Kipindi cha TMT kinachorushwa Kila
Jumamosi saa Nne usiku.
Baadhi
ya washiriki wakiwa na nyuso za simanzi kutokana na Washiriki wenzao
wawili kuaga mashindano hayo.Picha zote na Josephat Lukaza.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Shindano
la Tanzania Movie Talents (TMT) Linaelekea Ukingoni ambapo mwisho wa
Mwezi huu wa nane Mshindi mmoja wa shindano hilo la TMT ataondoka na
kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa.
Shindano
la TMT ni shindano ambalo limekuwa likiteka hisia za washiriki pamoja
na wadau na watazamaji wa kipindi hiko cha TMT ambacho kimejizolea
umaarufu nchini na nje ya Nchini kutokana na Umahiri wake ambapo awali
shindano hilo lilianza kanda ya ziwa Mkoani Mwanza kwaajili ya kusaka
vipaji vya kweli vya kuigiza ambapo baadae safari ilielekea katika kanda
nyingine za Tanzania ambapo washindi watatu kutoka kila kanda waliweza
Kupatikana na hatimaye kufanya jumla ya washiriki ishirini kutokana
kanda sita za Tanzania Kuwasili Jijini Dar Es Salaam, Mwishoni mwa Mwezi
wa Sita ambapo waliweka kambi na kuanza kupewa mafunzo na Mwalimu
Kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam aitwaye Dk Mona Mwakalinga akisaidia
na Mwl Issa.
Washiriki
Hao 20 waliweza pia kupata fursa ya kufanya filamu fupi ambazo ziliweza
kupima uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kutoka darasani na hatimaye
kupelekea watazamaji kuweza kuwapigia kura huku wakisaidiana na majaji
wa Shindano hilo. Majaji wa shindano hilo ni Roy Sarungi, Vyonne Cherry
na SIngle Mtambalike.
Mpaka
sasa Jumla ya Washiriki 7 wameshatoka kwenye kinyanganyiro na kupelekea
kubaki na washiriki wengine 13 ambapo washiriki watatu wanatakiwa kutoka
na kubaki washiriki 10 huku kumi hao wakiwa wameingia fainali sasa ya
kuzisaka zile Milioni hamsini ambazo Mshindi mmoja atajinyakulia siku ya
Fainali inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi wa 8.
Ili
kuweza kumbakiza mshiriki wako unachotakiwa kufanya ni Kumpigia Kura kwa
wingi kupitia Simu yako ya mkononi kwa kuandika Neno "TMT" acha nafasi namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano "TMT" 00 halafu tuma kwenda 15678 au Pia unaweza kumpigia kura mshiriki umpendae kupitia ukurasa wetu wa facebook kwa kutembelea anuani ifuatayo https://www.facebook.com/tztmt.
Washiriki
Kumi watakaoingia Kwenye Fainali ya Kusaka Milioni 50 watakuwa chini ya
Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Usamabazaji wa filamu za Kitanzania
ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la
Tanzania Movie Talents, Shindano Bora na kubwa Tanzania na la Kwanza
kufanyika Afrika Mashariki na Kati
0 Responses so far.
Post a Comment