Tacaids - 4
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi  Ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Tacaids -1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Tacaids -2
Mkiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya hali ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam mara baada ya kukamilisha ziara ya siku nne mkoani Dar es salaam. Dkt. Fatma ameeleza kuwa maabukizi yameendelea kupungua kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Tacaids -5
Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya ziara ya watendaji wa TACAIDS katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuangalia hatua iliyofikiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam.
Tacaids -6
Viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi wakichukua michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na wajumbe waliohudhuria kikao cha majumuisho ya ziara ya  viongozi wa TACAIDS mkoani Dar es salaam.
Tacaids-3
Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akitoa mchango wake kuhusu namna viongozi wanavyoweza kusaidia kupunguza vitendo hatarishi vinavyochangia maabukizi mapya ya VVU katika maeneo wanayoyaongoza, wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa-MAELEZO.
Dar es salaam.
 
Serikali imewataka viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele na kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na vitendo vyote vinavyochangia maambukizi mapya ya VVU katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
 
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam.
 
Amesema viongozi na watendaji wa jiji hilo ndio wenye dhamana na jukumu la kusimamia na kuongoza mipango yote ya mapambano ya maambukizi mapya ya VVU wakishirikiana na wananchi katika maeneo wanayoyaongoza na kufafanua kuwa janga la Ukimwi lisipodhibitiwa katika ngazi zote litaendelea kupoteza nguvu kazi na kuiongezea serikali mzigo wa kuwahudumia wagonjwa wapya.
 
“Nawaagiza viongozi wa manispaa zote tatu za mkoa wa Dar es salaam kulipa kipaumbele kikubwa suala hili la mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwa kuweka msukumo katika kutoa elimu ili tuweze kuokoa rasilimali zetu” Amesema.
 
Amesema serikali, vyombo vya habari na Taasisi zilizo kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU zimekuwa zikifanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya namna ya kujikinga na janga hili na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kwa hiari ili kujua kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali ya jiji.
 
Ameeleza kuwa licha ya mkoa kukabiliwa na changamoto mbalimbali umeendelea kuchukua hatua  za kupunguza maabukizi mapya ya VVU kwa kuweka msisitizo katika utoaji wa elimu, kupiga marufuku ngoma hatarishi za usiku zinazokesha, kutekeleza sheria mbalimbali kupitia jeshi la Polisi ambalo huendesha operesheni mbalimbali za kuwakamata wananchi wanaovunja sheria hususan waendesha biashara za madanguro,watumia madawa ya kulevya na biashara ya ngono kwenye majumba ya starehe.
 
“Tunaendelea kutoa elimu ya kujikinga na maabukizi mapya ya VVU ili kusaidia hata operesheni mbalimbali tunazofanya katika jiji letu kuzaa matunda na kuwafanya wale wote waliokuwa wakijihusisha na vitendo vinavyochangia kueneza VVU kuachana navyo” Amesisitiza.
 
Aidha, Bw. Meck Sadiki amegiza kupatiwa orodha ya maeneo yote ya jiji la Dar es salaam ambayo yanaongoza kwa kuwa na vihatarishi vya VVU ili aweze kuyafanyia kazi na kuwaomba wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kutoa ushirikiano kwa kuunga mkono juhudi za serikali na kuwafichua wanaoendesha vitendo vinavyochangia maambukizi hayo ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za kisheria.
 
Kwa upande wake Mkiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho akizungumza wakati wa majumuisho hayo amesema kuwa  hali ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam yameendelea kupungua kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
“Ni kweli hali ya maabukizi ya VVU kwa mkoa wa Dar es salaam imeendelea kupungua  mwaka hadi mwaka toka asilimia 10.9 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 6.9 za mwaka 2012 jambo linalotufanya tuendelee kuongeza juhudi zaidi ili tufikie malengo ya kitaifa na kimataifa ya kufikia sifuri tatu”. Amesisitiza.
 
Amesema ili kuhakikisha kuwa vita dhidi ya maambukizi mapya ya VVU inaendelea kufanikiwa , Serikali  inashirikiana na taasisi mbalimbali, Baraza na mitandao ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi  nchini katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na tatizo hilo.
 
Ameongeza kuwa serikali inawathamini na inaendelea kuwajengea uwezo Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi waliojiunga katika Vikundi vya Kuweka Akiba na Mikopo (VICOBA) katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na mwamko mkubwa wa kujiletea maendeleo waliouonyesha.
 
Ametoa wito kwa WAVIU kote nchini kuendelea kujiunga na mifuko mbalimbali  ukiwemo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili waweze kunufaika na huduma za afya zinazotolewa kupitia mfuko huo.

photo ,

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu Severini Niwemugizi  wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa akiwa na wasaidizi wake wakati wa Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa akiongoza ibada maalum ya Jubilei hiyo.

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu Severini Niwemugizi akizungumza katika sherehe hizo,wakati alipokuwa akitoa salamu za Baraza hilo kwa Serikali.
Mh. Lowassa akiwapungua mkono Waumini wakati alipokuwa akitambulishwa.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati wa Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono kwa kuwasalimia waumini waliofika kwenye Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Halaiki ya vijana.
Sehemu ya Waumini walioshiriki kwenye Jubilei hiyo.

photo , ,


 Pichani ni Jengo litakalojengwa jijini Dar es salaam na litagharimu Dola za kimarekani milioni 77,kutakuwa na hoteli ya hadhi ya Nyota Tano, Ofisi za Biashara, kutakuwa na Sehemu ya kuegesha magari, jengo hili litatakuwa kivutio kwa Wawekezaji na Utalii.
(23 Juni 2014)
 Baadhi Malori na Vifaa vingine vya kutendea kazi vikiwa tayari kuahiria ujenzi huu unaanza mara moja baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kukamilika.

 Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye sherehe ya uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo la Malimu Nyerere Foundation Square
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamini Mkapa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Cleopa Msuya wakati wa shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo refu la ghorofa la Mwalimu Nyerere Foundation.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuwekwa jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) wakijippongeza baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja  wakimwaga mchanga kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam,Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Profesa Shivji pamoja na Wazee wengine wakati wa shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi wa Ujenzi wa jengo la Mwalimu Nyerere Foundation Square.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku akihutubia wakati wa Uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo la Mwalimu Nyerere Foundation Square.

Picha ya Pamoja baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la Msingi kukamilika.
(Picha na Adam Mzee)

photo , ,

DSC_0217
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya resi za Ngalawa wakijiandaa tayari kwa kuanza mashindano hayo katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF 2014 linaloendelea visiwani Zanzibar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

NGALAWA zote 11 zilizoingia majini kukamilisha mzunguko wa saa mbili wa resi za ngalawa mjini Zanzibar zilimarisha mashamshamu hayo bila najali na timu tatu zilipewa zawadi za ushindi.
Resi za Ngalawa kama zinavyojulikana ni utamaduni halisi wa visiwa vya pemba na Unguja na ni sehemu ya tamasha kubwa la filamu la kimataifa la Zanzibar ambalo linaendelea visiwani hapa.
Kwa wale waliozaliwa maeneo ya bara, resi hizi zilikuwa kivutio kikubwa kwao kutokana na maandalizi yanayofanywa kabla ya kuingia majini na dau kunyanuliwa.
Wakati dau limenyanyuliwa, maji yamekuwa yakichotwa ama ndani ya Ngalawa au nje katika bahari kumwagia tanga katika hali inayoelezwa kuliimarisha katika ukinzani wa upepo.
“mbio za Ngalawa ni kipimo kikubwa cha Uzanzibari wetu na kila mwaka ZIFF huhitimisha utashi wake wa kuwa na tamasha la nchi za jahazi kwa kuwa na mbio za ngalawa” alisema mshehereshaji Muslim Nassoro Abdalla katika shamrashamra zilizofanyika ufukweni kandoani mwa hoteli ya Tembo.
DSC_0235
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (mwenye t-shirt ya njano) akupiliza Kipenga kuashiria kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye fukwe za Hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.

Muslim ambaye alisema kwamba mwaka huu walitaka kuwa na mbio za timu 20 (ngalawa) walishindwa kuhitimisha ndoto hiyo kutokana na masuala nje ya uwezo wa ZIFF.
Ili kukamilisha vyema mbio hizo kunatakiwa kuwa na boti za kutosha za uokozi kama kutatokea ajali.
Mwaka juzi kulitokea ajali ambayo hata boti ilipofanya uokozi nayo ikazidiwa na kulazimisha watu kukwama mpaka jioni walipopata boti nyingine kutoka Bandarini.
Wakati wa mbio za resi ambazo washindi wa kwanza ni timu iliyokuwa ikiongozwa na Hatibu Suleiman waliokuwa ndani ya ngalawa Ipo Siku, ngoma mbalimbali za asili zilipigwa ufukoni kama hamasa huku watu wakisubiri marejeo ya ngalawa hizo.
DSC_0241
Baadhi ya Ngalawa zinazoshiriki 
mashindano hayo zikianza kukata mawimbi.

Mbio hizo ambazo zilianzishwa na mbunge wa Kiembesamaki na Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mahmoud Thabiti Kombo mshindi wake wa pili alikuwa ni timu ya haji Hassan (kama nadhodha) ndani ya ngalawa Kipanga. Aidha Hassan Simai na wenzake waliokuwa katika ngalawa iliyoitwa peace of Love walikuwa washindi wa tatu.
Timu ya ngalawa ambayo inahitaji ujuzi katika utekaji tanga , kulirekebisha na kubalansi ngalawa inahitaji watu wapatao watano na si chini ya watatu.
Tamasha la filamu linaendelea mjini hapa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya utunzi, utengenezaji wa filamu na uhakiki wake.
DSC_0262
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wakazi wa Zanzibar wakishuhudia mashindano hayo.
DSC_0266 Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ( wa pili kulia) akiwa meza kuu na mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo Mohammed DSC_0299 DSC_0268
Burudani ya Ngoma kutoka Nungwi ikitumbuiza wakati wa mashindano hayo.
DSC_0314
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akionyesha moja ya zawadi t-shirt kwa watoa burudani waliokuwa wakishindana kucheza ngoma za asili.
DSC_0286
Mkazi wa Nungwi na Stone town (mwenye kaptura) wakishindana kutoa burudani ya ngoma za asili za visiwani humo wakati wa mashindano hayo.
DSC_0325
Mshehereshaji wa tamasha la ZIFF 2014, Muslim Nassor akimuonyesha moja ya zawadi (haipo pichani) mkazi wa Stone town aliyekuwa akisherehesha wakati wa mashindano ya Ngalawa kwenye fukwe za hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.
DSC_0581
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa tatu nahodha wa resi za Ngalawa iliyopewa jina la " Peace of life" M, Bw. Hassan Simai.
DSC_0586
Mshindi wa tatu nahodha wa resi za Ngalawa, "Peace of life" Bw. Hassan Simai katika picha ya pamoja na mdhamini wa Ngalawa yao iliyopewa jina la " Peace of life" Mkurugenzi mtendaji wa Zanlink, Bw. Sanjay Raja.
DSC_0593
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili nahodha wa resi za Ngalawa iliyopewa jina la "Kipanga" Haji Hassan. Katikati ni mdhamini wa Ngalawa ya Kipanga, Bi. Latifa Mohamed Omar kutoka Zan Air.
DSC_0594
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa nahodha mashindano ya resi za Ngalawa, Bw. Khatib Suleiman katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF linaloendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.
DSC_0598
mshindi wa kwanza wa mashindano ya resi za Ngalawa, Bw. Khatib Suleiman (kushoto) akipongezwa na mdhamini wake mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed (katikati). Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.

photo ,

Bw Harusi ,Joshua Nassari na Bi Harusi Anande Nnko wakapanda usafiri mwingine tofauti na ule waliofika nao katika Hotel ya Ngurdoto na safari hii ni kuelekea uwanja wa User-River kwa ajili ya sherehe.
Msafara ukaanza safari yake kutoka Ngurdoto huku njiani madereva wa Boda boda wakiwa wamezunguka gari la Maharusi na wengine wakionesha mbwembwe.

Baada ya mwendo kido Maasai nao wakaomba msafara wa pikipiki ukae pembeni wakidai ni zamu yao sasa kusindikiza Maharusi.
Huko uwanjani MC ,Masanja Mkandamizaji na Salum Mwalimu walikuwa bize kuweka mambo sawa.
Wageni mbalimbali walikuwepo uwanjani hapo wakingojea Maharausi miongoni mwao ni wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakiwa na wapambe wao katika pozi la kuchukua Taswira.
Taswira katika maeneo mbalimbali ya Ngurdoto Mountain Lodge.


Bi Harusi Anande Nnko akiwa amebebwa na Bwana Harusi pamoja na wapambe wake.
Pozi tofauti za Maharusi.
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wazizi wa Bi Harusi Anande Nnko pamoja na ndugu zao.
Maharusi wakiwa na Mzee Edwin Mtei pamoja na Mama Mtei.


Bwana Harusi Joshua Nassari akiwa katika pozi la picha na wazazi wake.


Mbunge wa viti maalum Lucy Owenya pia alihakikisha na yeye anakuwa kwenye kumbukumbu za Picha ,Baada ya picha safari ilikuwa ni ya kuelekea Ukumbini yote utayaona hapa hapa.
 

photo , ,