Baadhi
ya washiriki wa mashindano ya resi za Ngalawa wakijiandaa tayari kwa
kuanza mashindano hayo katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF
2014 linaloendelea visiwani Zanzibar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
NGALAWA
zote 11 zilizoingia majini kukamilisha mzunguko wa saa mbili wa resi za
ngalawa mjini Zanzibar zilimarisha mashamshamu hayo bila najali na timu
tatu zilipewa zawadi za ushindi.
Resi
za Ngalawa kama zinavyojulikana ni utamaduni halisi wa visiwa vya pemba
na Unguja na ni sehemu ya tamasha kubwa la filamu la kimataifa la
Zanzibar ambalo linaendelea visiwani hapa.
Kwa
wale waliozaliwa maeneo ya bara, resi hizi zilikuwa kivutio kikubwa
kwao kutokana na maandalizi yanayofanywa kabla ya kuingia majini na dau
kunyanuliwa.
Wakati
dau limenyanyuliwa, maji yamekuwa yakichotwa ama ndani ya Ngalawa au
nje katika bahari kumwagia tanga katika hali inayoelezwa kuliimarisha
katika ukinzani wa upepo.
“mbio
za Ngalawa ni kipimo kikubwa cha Uzanzibari wetu na kila mwaka ZIFF
huhitimisha utashi wake wa kuwa na tamasha la nchi za jahazi kwa kuwa na
mbio za ngalawa” alisema mshehereshaji Muslim Nassoro Abdalla katika
shamrashamra zilizofanyika ufukweni kandoani mwa hoteli ya Tembo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe.
Mahmoud Thabit Kombo (mwenye t-shirt ya njano) akupiliza Kipenga
kuashiria kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye fukwe za
Hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.
Muslim
ambaye alisema kwamba mwaka huu walitaka kuwa na mbio za timu 20
(ngalawa) walishindwa kuhitimisha ndoto hiyo kutokana na masuala nje ya
uwezo wa ZIFF.
Ili kukamilisha vyema mbio hizo kunatakiwa kuwa na boti za kutosha za uokozi kama kutatokea ajali.
Mwaka
juzi kulitokea ajali ambayo hata boti ilipofanya uokozi nayo ikazidiwa
na kulazimisha watu kukwama mpaka jioni walipopata boti nyingine kutoka
Bandarini.
Wakati
wa mbio za resi ambazo washindi wa kwanza ni timu iliyokuwa ikiongozwa
na Hatibu Suleiman waliokuwa ndani ya ngalawa Ipo Siku, ngoma mbalimbali
za asili zilipigwa ufukoni kama hamasa huku watu wakisubiri marejeo ya
ngalawa hizo.
Baadhi ya Ngalawa zinazoshiriki
mashindano hayo zikianza kukata mawimbi.
Mbio
hizo ambazo zilianzishwa na mbunge wa Kiembesamaki na Mwenyekiti wa
Bodi ya ZIFF, Mahmoud Thabiti Kombo mshindi wake wa pili alikuwa ni timu
ya haji Hassan (kama nadhodha) ndani ya ngalawa Kipanga. Aidha Hassan
Simai na wenzake waliokuwa katika ngalawa iliyoitwa peace of Love
walikuwa washindi wa tatu.
Timu
ya ngalawa ambayo inahitaji ujuzi katika utekaji tanga , kulirekebisha
na kubalansi ngalawa inahitaji watu wapatao watano na si chini ya
watatu.
Tamasha
la filamu linaendelea mjini hapa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za
mafunzo ya utunzi, utengenezaji wa filamu na uhakiki wake.
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wakazi wa Zanzibar wakishuhudia mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la
Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ( wa pili kulia) akiwa meza kuu
na mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo Mohammed
Burudani ya Ngoma kutoka Nungwi ikitumbuiza wakati wa mashindano hayo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akionyesha moja ya zawadi t-shirt kwa watoa
burudani waliokuwa wakishindana kucheza ngoma za asili.
Mkazi
wa Nungwi na Stone town (mwenye kaptura) wakishindana kutoa burudani ya
ngoma za asili za visiwani humo wakati wa mashindano hayo.
Mshehereshaji
wa tamasha la ZIFF 2014, Muslim Nassor akimuonyesha moja ya zawadi
(haipo pichani) mkazi wa Stone town aliyekuwa akisherehesha wakati wa
mashindano ya Ngalawa kwenye fukwe za hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa tatu nahodha
wa resi za Ngalawa iliyopewa jina la " Peace of life" M, Bw. Hassan Simai.
Mshindi
wa tatu nahodha wa resi za Ngalawa, "Peace of life" Bw. Hassan Simai
katika picha ya pamoja na mdhamini wa Ngalawa yao iliyopewa jina la "
Peace of life" Mkurugenzi mtendaji wa Zanlink, Bw. Sanjay Raja.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili nahodha
wa resi za Ngalawa iliyopewa jina la "Kipanga" Haji Hassan. Katikati ni
mdhamini wa Ngalawa ya Kipanga, Bi. Latifa Mohamed Omar kutoka Zan Air.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi zawadi kwa mshindi
wa kwanza wa nahodha mashindano ya resi za Ngalawa, Bw. Khatib Suleiman
katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF linaloendelea kutimua
vumbi visiwani Zanzibar.
mshindi wa kwanza wa mashindano ya resi za Ngalawa, Bw. Khatib Suleiman (kushoto) akipongezwa na mdhamini wake mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed (katikati). Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
0 Responses so far.
Post a Comment