Pichani ni
Jengo litakalojengwa jijini Dar es salaam na litagharimu Dola za
kimarekani milioni 77,kutakuwa na hoteli ya hadhi ya Nyota Tano, Ofisi
za Biashara, kutakuwa na Sehemu ya kuegesha magari, jengo hili
litatakuwa kivutio kwa Wawekezaji na Utalii.
(23 Juni 2014)
Baadhi
Malori na Vifaa vingine vya kutendea kazi vikiwa tayari kuahiria ujenzi
huu unaanza mara moja baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi
kukamilika.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye sherehe ya uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo la Malimu Nyerere Foundation Square
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamini Mkapa akizungumza na
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Cleopa Msuya wakati wa shughuli za uwekaji wa
jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo refu la ghorofa la Mwalimu Nyerere
Foundation.
Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuwekwa jiwe la msingi katika eneo
litakapojengwa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam.
Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (kulia) wakijippongeza baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo
litakapojengwa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam.
Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakimwaga mchanga
kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini
Dar es salaam,Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akibadilishana mawazo na
Profesa Shivji pamoja na Wazee wengine wakati wa shughuli za uwekaji wa
jiwe la msingi wa Ujenzi wa jengo la Mwalimu Nyerere Foundation Square.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku akihutubia wakati wa
Uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo la Mwalimu Nyerere Foundation
Square.
Picha ya Pamoja baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la Msingi kukamilika.
(Picha na Adam Mzee)
0 Responses so far.
Post a Comment