Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.

Alielezea kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.

Mhe. Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
 Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu  hicho katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe 21.11.2014.
  Mhe. Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi  (mwenye kofia ya njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi  Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa mahafali hayo ya kumi na moja.
 Shekhe Dr.Badruh H.Sseguja akifungua kwa sala Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
  Mchungaji Ogah Ogbole akifungua kwa sala mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba ya ufunguzi wa  mahafali hayo ya kumi na moja ya chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwa utulivu tayari kabisa kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 902 walihitimu masomo yao.
 Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakiingia katika viwanja vya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam tayari kwa mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja.
   Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja ambapo aliwaasa kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
 Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala wakinyanyua kofia zao juu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali yao ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo wakifuatilia hatua kwa hatua kile kinachoendelea katika sherehe hizo.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala akitunuku shahada kwa wahitimu wa mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi ( mwenye joho la njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Membe pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo wa taifa kama ishara ya kufunga mahafali hayo ya kumi na moja.
 Mgeni rasmi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali hayo.   PICHA NA Reuben Mchome 

photo , ,


Mjumbe wa Halamashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) na Mbunge wa Jimbo la Chalinze lililopo Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Ridhiwan Kikwete amefanya ziara Jimboni kwake na kugawa Baiskeli 221 kwaajili matawi yote ya CCM jimboni humo kusaidia shughukli za uchaguzi Serikali za Mitaa na Vijiji.

Baiskeli hizo ziligawiwa kwa Makatibu wa Vyama kutoka ofisi hizo za CCM.
 Katibu wa Mbunge wa Chalinze, akiwa na baadhi ya Makatibu wa Matawi ya CCM.
 Katibu wa Mbunge akiwa na mtaalam wa uchimbaji maji na vifaa vyao katika Shule ya Sekondari ya Wafugaji Moreto ambako kisima cha maji kwaajili ya wananchi kitachimbwa.
 Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akiwa na watoto jimboni kwake.
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete alifanya Mkutano na wapiga kura wake nyumbani kwa Balozi wa Chama Zimbili, huko Mandamazingara ambapo alisikiliza kero mbali mbali za wananchi na kuzungumza nao.
 Pia alizungumza na mtu mmoja mmoja ...

 Akihutubia hadhara hiyo ya Mandamazingara nyumbani kwa Balozi wa Shina.
 Akichukua namba ya simu ya Mpigakura wake..

photo , ,


Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi rasmi wa mahafali hayo jijini Dar es salaam. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Mathew Luhanga (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya Uhasibu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam mwaka 2014 wakisubiri kutunukiwa shahada zao wakati wa mahafali ya 49 yaliyofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl,Ubungo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao kwa mwaka 2014. Takribani wahitimu 3459 wametunukiwa Astashahada, Shahada na Stashahada za fani mbalimbali.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza na wahitimu 3459 wa fani mbalimbali wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao mwaka 2014.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)Prof. Mathew Luhanga akizungumza na wahitimu hao.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es salaam wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mahafari ya 49 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl jana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akisoma tamko la kuwatunuku wahitimu 3495 wa fani mbalimbali wa chuo cha CBE wakati wa mahafali ya 49 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akiondoka ukumbini akiwa ameambatana na viongozi wengine wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam mara baada ya kufunga rasmi mahafali hayo. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

SERIKALI imewataka watendaji na wamiliki wa makampuni mbalimbali kutoka ndani na  nje nchi  kuacha tabia ya kutoa nafasi nyingi za ajira kwa wageni na badala yake wawatumie vijana wa kitanzania wanaohitimu masomo  katika vyuo mbalimbali  hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Viwanda Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza na wahitimu 3363 wa fani mbalimbali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya  Dar es salaam waliohudhuria mahafali ya 49 ya  chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam. 

Amesema Tanzania ina vijana wengi wenye kukidhi viwango na uwezo wa kutekeleza majukumu ya Uhasibu,Udhibiti wa Biashara, Usimamizi wa Masoko,Manunuzi na Ugavi , Mizani na Vipimo pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa ufanisi mkubwa kutokana na mafunzo waliyopewa katika vyuo na taasisi mbalimbali  hapa nchini.

 “Tanzania tunao vijana bora na wenye kukidhi viwango wanaohitimu kila mwaka,suala la kutoa visingizio  kuwa hatuna wataalam na makampuni haya kuajiri wageni katika nafasi za kawaida na ngazi za utawala mimi sikubaliani nalo ,nakemea tabia hii”  Amesisitiza Dkt. Kigoda.

Amefafanua kuwa Serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo la ukosefu wa ajira lililopo hapa nchini kwa kujenga na kuandaa mazingira wezeshi ya kukuza utengenezaji wa ajira za kujiajiri na kuajiriwa kwa kuendeleza sekta binafsi katika eneo la Kilimo, Sekta ya Viwanda na Biashara hususan ujasiriamali mdogo na wa kati.

Ameeleza kuwa serikali inaendelea kujenga mazingira wezeshi na rafiki kwa wahitimu hao kujiajiri wenyewe kwa kuratibu mfumo wake wa kodi na tozo mbalimbali, kuangalia hatua za utoaji wa leseni na usajili wa biashara, kushughulikia tatizo la uhaba wa mikopo na riba zinazotolewa kwa wale wanaotumia mikopo kama mitaji pamoja na kushughulikia suala la mikataba inayoandaliwa na makampuni ambayo mara nyingi inawakosesha vijana fursa ya kupata ajira.

Ametoa wito kwa wahitimu hao kuwa wajasiri na wenye moyo wa kuthubutu wa kutumia taaluma na mafunzo waliyopata kuleta mabadiliko na maendeleo nchini huku akiwataka wahitimu hao kuepuka tabia ya uzembe, uvivu na Rushwa pindi watakapoingia kwenye ajira.

Kuhusu uboreshaji chuo hicho Dkt. Kigoda amesema Serikali inaendelea kukijengea uwezo chuo hicho kwa kuimarisha ubora wa mafunzo yanayotolewa hususan matumizi ya mifumo ya kompyuta na mawasiliano (ICT) ili kiweze kushindana na vyuo vya kigeni vilivyoanzisha kampasi zao hapa nchini.

Kwa upande wake  mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga akizungumzia   mahafali hayo ya 49 ya chuo hicho amesema kuwa yanakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.

Amesema tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 1965 mafanikio mbalimbali yamepatikana yakiwemo ya kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kujiunga na masomo hadi kufikia kutoka 25 pindi chuo kinaanzishwa hadi 14000 wa sasa, ongezeko la kampasi kutoka 1 hadi kufikia 4.

Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni kuongezeka kwa kozi za masomo na ngazi za mafunzo kutoka 1iliyokuwepo mwaka 1965 hadi 6 zilizopo sasa na ongezeko la wakufunzi wenye shahada ya uzamivu (PhD).

 Prof. Luhanga amefafanua kuwa chuo hicho sasa kimeanzisha ushirikiano wa elimu na vyuo vikuu vingine  vilivyo nje ya nchi kikiwemo Chuo Kikuu cha Maastricht cha Uholanzi, Chuo Kikuu cha Stockholm cha Sweeden na Chuo Kikuu cha Eastern Finland ambacho kimeshirikiana na CBE  kutoa mafunzo ya shahada ya uzamivu  kwa nchi za SADC.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akiwakaribisha wahitimu, wadau mbalimbali na Wanajumuiya wa Chuo hicho waliohudhuria  mahafali hayo  amesema  kuwa chuo chake kimepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965 ikiwemo ongezeko la idadi ya wanafunzi wa kike wanaohitimu chuoni hapo hadi kufikia asilimia 48 kwa mwaka 2014.

Amesema tangu kuanzishwa kwa chuo hicho wataalam wengi katika fani za Uhasibu,Udhibiti wa Biashara, Usimamizi wa Masoko,Manunuzi na Ugavi , Mizani na Vipimo pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wameweza kuhitimu na kutoa mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

photo ,


Pichani juu na chini ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Dkt.Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akizungumza katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto akifafanua jambo kwenye kongamano la tisa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Waandishi wa habari lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya Kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya kutoka wilaya mbalimbali walioko mezani mbele wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo la tisa la NHIF,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid ndiye aliyezindua kongamano hilo lililohudhuriwa na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee na pichani kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid wakifuatilia na kusikiliza kwa makini baadhi ya maswali na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahya Nawanda akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mmpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zikijadiliwa ndani ya kongamano hilo mapema leo mchana.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto,Kaimu Mkurugenzi wa Tiba na Ushauri wa NHIF,Bwa.Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakiwa kwenye  kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma.
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima (RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).


photo ,