Mahakama ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani
kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka
15( jina linahifadhiwa).
Mwendesha mashitaka wa serikali Archiles Mulisa aliiambia
mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni
Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa
kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na
155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu
cha 158(a) cha makosa ya kuzini.
Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada
ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la
Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa miaka minne hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe
taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito
alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni
binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali
baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa
ulidai kuwa Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15
ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa
asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu, Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa
kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali
ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote
itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda
jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu
endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo,
Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na
Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume
mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “mfa
maji haachi kutapatapa”.
0 Responses so far.
Post a Comment