Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya
ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati
wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wasanii
wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani
wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao
wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika katika Uwanja wa
Jamhuri mijini Morogoro.
Wakulima
wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano leo wakati wa
sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamtandao wa Jumuiya ya
wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi maandamano ya
wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR.
0 Responses so far.
Post a Comment