Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi hundi ya jumla ya Shilingi Milioni
miamoja na Hamsini 150m/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulea watoto
yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mkoa wa Geita.
Fedha hizo
si sehemu ya shilingi milioni mia saba (700m/-) alizokabidhi Rais
Kikwete jana usiku kwa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na
mapambano dhidi ya ukimwi Tanzania.Fedha hizo zinatokana na kampeni ya
kukusanya fedha kwa njia ya kupanda mlima Kilimanjaro kila mwaka ambapo
wafadhili mbalimbali huchangia watoto na watu wengine.Pichani watoto
wawili watakaopanda mlima Kilimanjaro Jacob Musa (watatu kushoto) na
Julitha Sylvester (wapili kulia) wanaofadhiliwa na kituo cha Moyo wa
huruma wakipokea hundi ya kituo chao.
Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Dr.Florence Turuka,Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS Bi Fatma Mrisho,Mkurugenzi
Mtendaji wa Geita Gold Mines Bwana Michael Van Anen (watano kushoto)
Naibu Waziri wa Afya Dr.Steven Kebwe, na kulia ni msimamizi wa kituo
cha kulelea watot yatima cha Moyo wa Huruma Sista Adalbera Mukure.
Katika hafla
ya jana ya kuchangia kampeni hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt
Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam zaidi ya shilingi milioni mia
tisa 900m/- zilikusanywa .Picha na Freddy Maro
0 Responses so far.
Post a Comment