Mshehereshaji ambaye ni Mwanakamati ya
maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya waandishi wa habari
wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark
Bomani.(Picha zote na Zainul Mzige).
Na Mwandishi wetu
Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema lengo la
mchakato wa Katiba ni kuhakikisha kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo
ni bora zaidi kuliko zote itakayoshughulikia changamoto na kuweka
mazingira ambayo yatamrahisishia maendeleo mwananchi kwa haraka.
Akitoa risala katika maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo katika ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa AICC jijini Arusha, Jaji Mstaafu Mark Bomani, amesema jukumu
la mwanahabari ni kuwaelimisha baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la
Katiba ambao hawana uelewa mkubwa na mchakato wa Katiba hawajui maana
halisi ya Katiba mambo ambayo yanasababisha kujadili Katiba hiyo kwa
maneno mabaya, kutishiana, matusi na kejeli.
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.
“Zoezi la mchakato wa Katiba ni kubwa na
wabunge wengi wa Bunge Maalum la Katiba hawaelewi wajibu wao katika
kuijadili Katiba hiyo matokeo yake ndio hayo wanayoshuhudia Watanzania”.
Mara nyingi Watanzania wameshuhudia
mijadala ya kejeli, malumbano, matusi, kudharauliana pale hoja
zinapojengwa na upande ambao haukubaliki na upande mwingine jambo ambalo
limewavunja moyo Watanzania na kutokuwa na imani ya kupata Katiba
inayolenga kumlinda mwananchi.
Jukumu la wanahabari ni kutoa elimu ya
kutosha kuhusu yaliyomo katika Katiba Mpya na kuandika habari za
maendeleo ili majadiliano yatokanayo yawe endelevu yamtendee haki
mwananchi wa kawaida kwa lengo la kuboresha maisha yao.
Meza Kuu, kutoka kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa
Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, Mkurugenzi wa Mfuko wa
Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, Mkuu wa Wilaya ya
Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani,
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la
Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais wa Umoja wa Vilabu
vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya na Meneja
Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John
Mirenyi.
“Inasikitisha kuona kuwa hali ya
Mtanzania inazidi kudidimia au kubaki pale pale katika sehemu nyingi
hasa vijijini katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kwa kukosa fursa
muhimu za maendeleo na viongozi hawalioni hilo”, amesema Jaji Mstaafu
Mark Bomani.
Wakati huo huo mgeni huyo rasmi amekemea
tabia ya kuandika habari za kuwasifu viongozi na kupokea Rushwa hali
iliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni na kusema kwamba ni fedhea
kwa tasnia ya habari kutofuata maadili ya uandishi.
Amesema kwamba nchi itaendeshwa kwa
kusimamia haki na ukweli na kuwataka wanahabari wasichoke kuisimamia
haki na uhuru wa nchi yao bila woga kwani bila kufanya hivyo nchi
itaongozwa kiimla.
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani,
akitoa risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa
wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma.
“Kuna tabia ya vyombo vya habari ya
vyombo vya habari kununuliwa ili visiandike au kufichua maovu ni fedhea
kwani vyombo vya habari ni kioo cha jamii”.
Akizungumzia kuhusu sheria za habari za
mwaka 2007 na 2008, Jaji Mstaafu amesema ni aibu kuona mswaada wa sheria
ya habari umekwama kwa zaidi ya miaka 10 kwa sababu ambazo hadi leo
hazijaeleweka.
Amewataka waandishi wa habari wasikate
tamaa na badala yake waendelea na kupambana kuhakikisha kwamba harakati
za kupata Sheria ya Haki ya Kujua inafanikiwa ili kupunguza matukio ya
manyanyaso, kupigwa, kuteswa, kufungwa kwa vyombo vya habari na kuuwawa.
“Haki haiyombwi simamieni Haki zenu na songeni mbele”, ameongeza Jaji Bomani.
Sehemu ya wadau wa tasnia ya Habari wakisikiliza risala ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John
Mongela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha kwenye
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika
jijini Arusha kenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya
Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed
Tibanyendera, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wamikutano wa
Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Wageni waalikwa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa kwenye ukimya kumkumbuka Mwandishi aliyeuwawa mkoani Iringa Daudi Mwangosi.
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu,
Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab
Coulibaly, akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na
Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru
wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
Meneja Machapisho, Utafiti na Uhifadhi
Hati wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi, akitoa
maelezo ya machapisho mbalimbali yaliyoandaliwa na baraza hilo yakiwemo
yenye madhila mbalimbali yaliwahi kuwakumba baadhi ya waandishi wa
habari ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya
Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, akizungumzia mchango wa mfuko
huo unaowawezesha waandishi wa habari kutafuta habari za uchunguzi na
zinazoigusa jamii.
Wasanii wa Bendi ya Mrisho Mpoto
(Mjomba Band) wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa maadhimisho
ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini
Arusha mwishoni mwa juma.
Sehemu ya wadau wa tasnia ya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo.
Katibu wa Chama cha Wamiliki wa
Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika, akisoma hotuba kwa
niaba ya Dr. Reginald Mengi kwenye maadhisho hayo.
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akizungumzia wakati wa maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF),
Absalom Kibanda, akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakumba
waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka,
akizungumzia changamoto za usawa wa Kijinsia katika uongozi kwenye
Vyombo vya Habari nchini.
Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal
Shelutete, akizungumzia ushiriki wao kwenye Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani 2014 ambapo aliwataka waandishi wahabari kutumia kalamu
zao vizuri katika kukuza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Meneja Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya
Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo, akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo amewataka
waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika kupambana na suala la
Ujangili linaloendelea nchini.
Mrisho Mpoto akiwafungua vitambaa
wasaani wa Mjomba Bendi kama ishara ya kuwapa Uhuru waandishi wa Habari
kuzungumza kilio chao mbele ya mgeni rasmi kama ujumbe wa Siku ya Uhuru
wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
Mrisho Mpoto na Bendi yake akighani
mashairi na kuelezea madhila wayapatayo waandishi wa habari wawapo
kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za kila siku.
Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya
Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji akimkaribisha mgeni
rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani kuzindua Video mpya ya wimbo "Uhuru
Wangu" wa Mrisho Mpoto uliokuwa kwenye Albamu yake mpya inayoitwa WAITE.
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani,
akibonyeza kitufe kuzindua rasmi wimbo huo wakati maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
Wageni waalikwa wakitiza wimbo huo.
Mkurugenzi wa Mbeya Highlands FM, Bi.
Jacqueline Mwakyambiki, akishiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru
wa Vyombo Vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
Mgeni rasmi Jaji Mark Bomani akizindua Album mpya ya Mrisho Mpoto inayoitwa "WAITE".
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Jaji Mstaafu Mark Bomani akizindua
na kuonyesha moja ya Ripoti ya Unyanyasaji dhidi ya Uhuru wa Habari
iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Kulia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika - Taiw la Tanzania (Misa
- Tan), Bw. Mohamed Tibanyendera.
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani
Pwani, Ahmed Kipozi akiteta jambo na mmoja wa Waandishi wa Habari
wakongwe Bw. Salim Salim kutoka visiwani Zanzibar.
Waandishi wa Habari wakongwe
(Ma-Veterans) kutoka kushoto Mama Eda Sanga, Fatuma Aloo na Leila Sheikh
wakifurahi jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari yaliyofanyika jijini Arusha .
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akisalimiana na Meneja
Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo wakati
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014
yaliyofanyika jijini Arusha.
Wadau wa tasnia ya habari wakinunua Album ya msaanii Mrisho Mpoto.
Baadhi ya wasanii wa Mjomba Band wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwandishi wa habari mkongwe Leila Sheikh.
0 Responses so far.
Post a Comment