Ikulu inavyoonekana kwa mbele. Soma historia yake fupi hapa chini
Ikulu ya tanzania ndiyo ofisi kuu ya Rais wa jamhuri ya tanzania ambapo ilianza kutumika kama ofisi ya Rais wa Tanzania mwaka 1962.
Jengo hili la Ikulu lilijengwa kwa mara ya kwanza mwaka 1919 na Gavana wa kwanza wa kijerumani ndugu Horrace Byatt. Baada ya gavana huyu kuingia madarakani alilazimika kukaa katika makazi ya muda yaliyoko karibu na Ikulu ya sasa ambayo makazi hayo yanatumika kama ofisi za wizara ya Afya.
Ujenzi huo ulikuja kukamilika mwaka 1922 huku baadhi ya nakshi za jengo hilo zikiwa zimewekwa na ndugu J. H Sinclair - Mtaalam wa majengo wakati wa ukoloni.
Mapambo mengine katika jengio hilo yalikuja kuongezeka baada ya uhuru ambapo mataifa mbalimbali yaliyotoa zawadi kama sehemu ya furaha yao katika kusherehekea uhuru wa tanzania.
Kwa faida ya wasomaji naomba kuweka kumbukumbu sawa! Sir Horace Byatt hakuwa gavana wa kwanza wa kijerumani Tanganyika. Huyu bwana alikuwa Gavana wa kwanza wa kiingereza Tanganyika mara tu baada ya Tanganyika kutwaliwa na Uingereza mara baada ya vita vya kwanza vya dunia.Mwaka 1919 Mjerumani hakuwapo Tanganyika wakati huo Tanganyika ilikuwa chini ya uangalizi wa jumuiya ya kimataifa kupitia kwa mwingereza.Utawala wa Mjerumani Tanganyika ulikoma rasmi baada ya Vita kuu ya kwanza ya dunia mwaka 1918.Naomba kutoa hoja!!!
Gavana wa kwanzamjeruman tanganyika ni Julius von soden