Mjumbe
wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu,
katika picha ya pamoja , Desemba 31, 2014 na baadhi ya wazee wasiojiweza
wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mjumbe
wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu,
akimkabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya mwaka
mpya 2015 kwa Wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa
ya Morogoro, mnamo Desemba 31, 2014, zawadi hiyo ilipokelewa na
Mwenyekiti wao Joseph Kaniki. ( Picha na John Nditi).
Na John Nditi, Morogoro
VIJANA
wa chama cha Mapinduzi UVCCM wameshauriwa kujenga tabia ya kusaidi
wazee wasiojiweza, kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwa lengo la kuwapa
faraja badala ya kuachia jukumu hilo kwa serikali pekee kama ilivyo
sasa.
Kauli
hiyo ilitolewa Desemba 31, 2014 na Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM)
wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu,wakati alipotembelea kituo cha
kuwatunza wazee wasiojiweza cha Fungafunga cha Kichangani Manispaa ya
Morogoro.
Lulu
ambaye pia ni mtoto wa mbunge wa jimbo la Temeke , Abbas Mtemvu,
alisema ametoa msaada wa mchele, mbuzi,sukari na sabuni za kufuria kwa
wazee hao zenye thamni ya sh milioni moja.
‘’
Pamoja na kuwa mimi ni mwanafunzi lakini nilijikusanya kwa muda mrefu
,kwaajili ya kutoa zawadi hii ya sikukuu kwa wazee hawa ili nao waweze
kufurahia katika sikuu ya mwaka mpya’’ alisema.
Hivyo
alitoa wito kwa vijana nchini kujenga tabia ya kusadia wazee, wajane na
watoto yatima ili kuwawezesha kuishi kwa matumaini na faraja, na kuona
jamii inawathamini.
‘’
Tukumbuke pia sisi ni wazee watarajiwa, hivyo tuone ni jukumu la jamii
nzima hususani viojana kusadia makundi hayo maalumu ambayo kwa hakika
yanahitaji msaada’’ alisema.
Kwa
upande wao wazee hao wa Funga funga walisema wamepata faraja kuona
vijana kama hao wanaona umuhimu wa kuwasaidia ili nao waweze kupata
chakula hasa katika sikukuu kama hiyo.
Akizungumza
kwa niaba ya wazee wa kituo hicho, Mwenyekiti wao ,Josefu Kaniki,
alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwapatia zawadi
ya mchele Kg 400, mafuta ya kura na mbuzi.
‘’
Tunapenda kutuma salamu zetu kwa Rais wetu Kikwete kwa kutukumbuka sisi
wazee, tunamhakikishia msaada umetufikia na tumefurahia na tunamwombe
dua ili aweze kutuongoza vema kwa hekima na busara katika kipindi chake
hiki" alisema Mwenyekiti wa wazee kituo hicho.
Pamoja
na kutoa shukrani hizo, aliiomba Serikali kuangalia uwezekeano wa
kuwalipia bili ya umeme, kwani kwa sasa wamekatiwa umeme kutokana na
kituo hicho kudaiwa deni la sh milioni nne.
‘’ Kwa
kweli tunakula tunashiba, lakini ikishafika jioni saa 12 , wazee wote
tunakosa amani, hatuna muda tena hata wa kuzungumza kama ilivyokuwa
zamani" alisema na kuongeza kuwa.
"
...Inatulazima kila mmoja awahi kitandani mwake kulala na hata kwenda
chooni ni shida hasa kwa wazee wasioweza kutembea’’ alibainisha.
Kituo
hicho cha Fungafunga kilichopo katika eneo la Kata ya Kichangani,
Manispaa ya Morogoro lina milikiwa na Idara ya Ustawi wa Jamii chini ya
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kina jumla ya wakazi 50, wakiwemo
wazee, wajane na watoto wasiojiweza.
0 Responses so far.
Post a Comment