Na Saidi Mkabakuli
Waziri
wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu
amefanya ziara ya kujitambulisha kwa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ambayo ni moja taasisi anazoziratibu.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo Dkt. Nagu alitoa wito kwa Tume ya Mipango
ijielekeze katika kujibu changamoto kuu za kiuchumi zinazowakabili
watanzania kwa sasa ikiwemo umaskini miongoni kwa Watanzania walioko
vijijini, ukosefu wa wa viwanda vya kuongeza thamani mazao hasa kipindi
hiki Tanzania inapoelekea kwenye uchumi wa gesi.
Dkt.
Nagu aliasa Tume ya Mipango kufanya tafiti mbalimbali za kiuchumi na
kijamii zitakazotoa majibu ya changamoto hizo.
“Kwa kuwa moja ya majukumu ya Tume ya Mipango ni kuandaa mipango ya
maendeleo ya muda mrefu, kati na ile ya kila mwaka na pia kufanya tafiti
mbalimbali za kiuchumi na kijamii, napenda kusisitiza kuwa mipango
inayoandaliwa ijielekeze katika kujibu changamoto hizo kubwa
zinazowakabili wananchi wetu ili kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ya
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Dkt. Nagu.
Kwa
mujibu wa malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, serikali
imejipanga kuhakikisha maisha bora na mazuri kwa kila mtanzania, utawala
bora unaozingatia sheria, na kujenga uchumi imara, wa kisasa na
ushindani.
Akizungumza
wakati wa kumkaribisha Dkt. Nagu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango,
Dkt. Philip Mpango alisema kuwa majukumu ya msingi ya Tume ya Mipango ni
kutoa dira na mwongozo wa uchumi wa Taifa pamoja na kubuni sera za
uchumi na mikakati ya mipango ya maendeleo ya Taifa; usimamizi wa uchumi
na kufanya utafiti katika nyanja za uchumi na maendeleo ya jamii.
Dkt.
Mpango aliongeza kuwa kwa sasa Tume ya Mipango inafanya kazi ya kuratibu
utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2014/15 pamoja na uandaaji
wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2015/16 na Mapendekezo ya Mpango wa
Maendeleo wa mwaka 2016/17.
“Vilevile, Tume ya Mipango tumejidhatiti katika kuandaa Mpango wa Pili
wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 ambao utajikita katika
kuifikisha tanzania kuwa ni nchi ya viwanda,” alisema Dkt. Mpango.
Kwa
mujibu wa Dkt. Mpango, tangu kuundwa upya kwa Tume ya Mipango mwaka
2008, imefanikiwa kukamilisha kazi kubwa za kitaifa ikiwemo kufanya
mapitio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, kuandaa Mpango Elekezi wa
Miaka 15 (2011/12 – 2025/26 pamoja na kuandaa Mpango wa Kwanza wa
Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na kuratibu utekelezaji wa
Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu 2006.
Kazi
nyingine ni pamoja na kuandaa Mipango ya Maendeleo ya Taifa kila Mwaka,
kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya Matokeo Makubwa
Sasa na kuratibu uanzishwaji wa President Delivery Bureau (PDB),
Kuandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma (Public
Investiment Management - Operational Manual – PIM-OM), na kufanya tafiti
mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Waziri
wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu
(Wapili kushoto) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango alipotembelea na kujitambulisha Tume ya Mipango.
Wanaomsikiliza ni Katibu Mtendaji, Dkt. Philip Mpango (Kushoto), Naibu
Katibu Mtendaji (Miundombinu na Huduma), Mhandisi Happiness Mgalula
(Wapili kulia) na Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na ya
Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe (Kulia).
Baadhi
ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza Waziri wa
nchi (Ofisi ya Rais) na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Hayupo pichani)
alipotembelea na kujitambulisha Tume ya Mipango.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akitoa
maelezo ya kumkaribisha Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na
Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kulia) wakati alipofanya ziara ya
kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
Waziri
wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu
akizungumza na watumishi na viongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
(Hawapo pichani) wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya
Mipango.
Baadhi
ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza
kwa makini Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe.
Dkt. Mary Nagu (Kulia) wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa
Tume ya Mipango.
Waziri
wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu
(Kulia) akizungumza na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip
Mpango (Kushoto) wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya
Mipango.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Tawi la Mipango, Bw. Stephen Katemba
(aliyesimama) akizungumza wakati Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais)
Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya
kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akimkabidhi
zawadi za vitendea kazi Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na
Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume
ya Mipango.
Naibu
Katibu Mtendaji (Miundombinu na Huduma), Mhandisi Happiness Mgalula
(Kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na
Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa
Tume ya Mipango.
Naibu
Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe
(Kushoto) akimkabidhi zawadi ya kitenge Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais)
Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya
kujitambulisha kwa Tume ya Mipango. Anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa
Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango.
Naibu
Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi
Florence Mwanri (Kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa nchi
(Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto)
alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiagana na
Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu
mara alipomaliza ziara yake ya kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
0 Responses so far.
Post a Comment