Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(kulia) pamoja na
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand, Mhe. Sura Pong
Tovichakehaikul(kushoto)wakisa ini Mkataba wa kubadilishana Wafungwa
kati ya Tanzania na Thailand(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
photo
DIPLOMASIA
Rais Kikwete akimjulia hali mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Said Mohamed Saad.
HABARI KAMILI
Said
ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, yenye maduka
mengi makubwa ya vitu vya nyumbani ndani ya Dar es Salaam na mikoa
kadhaa ya Tanzania, anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini lakini
mmoja wa watu waliomshuhudia, amefafanua jinsi hali ilivyo mbaya.
“Ameungua sana, tunatarajia kati ya kesho au keshokutwa (wikiendi
iliyopita) atafanyiwa oparesheni ya jicho. Jamani tindikali ni mbaya
sana, usimmwagie mwenzako. Ndugu yetu ameharibika sana,” kilisema chanzo
chetu kwa ombi la kutotajwa jina gazetini, kikaongeza:
“Kila anayemjua vizuri, anapomwona anamwaga machozi. Picha za jinsi
alivyoathirika baada ya kumwagiwa tindikali zimevuja mpaka kwa familia,
ni kilio kwa ndugu. Wanawake wanalia zaidi.”
JK ATINGA HOSPITALI
Wiki iliyopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete, alikuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini
alipokwenda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini ya Afrika (SADC).
Mkutano huo ni wa Pande Tatu za SADC (Troika of SADC) na akiwa huko,
alipata fursa ya kwenda kumjulia hali katika hospitali aliyolazwa ambayo
haijajulikana jina.
Chazo chetu kilisema: “Rais Kikwete alisikitika sana. Wakati anatoka
wodini alisonya. Alionesha jinsi alivyosikitishwa na unyama aliotendewa
Said.”
photo
Majanga
OPRAH WINFREY (KUSHOTO) KIWA AMEPOZI ALIPOTEMBELEA MBUGA YETU YA SERENGETI
photo
MGENI

Maaskofu
wa Kanisa Katoliki nchini wameitaka Serikali kutumia njia ya mazungumzo
kumaliza migogoro, badala ya kutumia jazba na nguvu.
Vilevile,
wamesema kuwa hawako tayari kukaa kimya huku wakiona amani na utulivu
nchini ikivurugika, badala yake wataendelea kusema ili amani na utulivu
viweze kurejea.
Kauli
hiyo imekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuwataka maaskofu hao na
viongozi wengine wa dini nchini kuendelea kuisaidia Serikali katika
kuimarisha amani na upendo miongoni mwa wananchi.
Akizungumza
wakati wa kuadhimisha Jubilee ya miaka 25 ya uaskofu wake kwenye
sherehe zilizofanyika jana katika Seminari ya Mt Peter mjini Morogoro,
Askofu wa Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, alisema meza ya mazungumzo
ni lazima itumike katika kuimalisha amani na upendo wa Watanzania
badala ya kutumia jazba na nguvu.
Mkude
alisema kwa hivi sasa kumeibuka mivutano ya kidini na kisiasa na kutoa
mfano wa vurugu zilizoibuka wilayani Sengerema mkoani Mwanza juu ya nani
ana haki ya kuchinja au kutokuchinja kati ya waumini wa madhehebu ya
Kikristo na Waislamu.
Pia
vurugu za mikutano ya kisiasa, makanisa kuchomwa, mapadri na watumishi
wengine kuuawa na kuteswa, kutupwa kwa mabomu katika mikusanyiko ya watu
ikiwamo makanisa na kwamba yote hayo yangeweza kumalizwa katika meza ya
mazungumzo.
Vurugu
kubwa zilitokea Jumamosi iliyopita mjini Arusha baada ya mtu ambaye
bado hajajulikana, kutupa bomu katika mkutano wa Chadema wa kampeni ya
uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika viwanja vya Soweto na kuua
watu wawili na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Mei
2, mwaka jana, Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud
Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na bomu na askari polisi katika vurugu
zilizotokea katika eneo la Nyololo mkoani Iringa.
Februaria
18, mwaka huu, Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili, Mji
Mkongwe, Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi asubuhi wakati akienda
kuendesha misa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia eneo la Mtoni.
Mtuhumiwa wa tukio hilo, Omar Musa Makame, anaendelea na kesi mahakamani
kujibu tuhuma za mauaji.
Tukio
lingine ni lile la watu wawili kuuawa na polisi mjini Songea, Februari
22, mwaka jana, wakati wakizuia maandamano ya wananchi wenye hasira kali
waliokuwa wakipinga mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikiana.
Hivi karibuni maaskofu hao walitoa tamko la kuitahadharisha Serikali, kudhibiti vurugu za kidini na kisiasa nchini.
Walionya
kuwa iwapo vurugu hizo hazitadhibitiwa huenda nchi ikaingia katika
machafuko.Awali, jana Rais Kikwete akizungumza katika hafla hiyo licha
ya kumpongeza Askofu Mkude kwa utumishi wake mwema wa miaka 25 ya
uaskofu wake, lakini pia alimpongeza kwa kuwa na mchango katika jitihada
za maendeleo zinazofanywa na Serikali.
Alisema Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro limekuwa msaada
katika kuimarisha huduma za jamii ikiwamo sekta ya elimu na afya na
kwamba baadhi ya zahanati na vituo vya afya vimejengwa na kupandishwa
hadhi kama Hospitali ya Mt Kizito na Turiani.
Rais Kikwete aliongeza kuwa mbali ya askofu huyo
kuisaidia Serikali katika nyanja hizo, pia amekuwa akiiunga mkono katika
jitihada zake za kujenga amani na upendo miongoni mwa wananchi ili
taifa liweze kuwa na raia wema.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es
Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alimtaja Askofu Mkude kuwa ni
kuhani asiyekuwa na mwanzo wala mwisho, kwa vile anashiriki katika
ukuhani wa Yesu Kristo asiyekuwa na mwanzo wala mwisho.
Alisema mpaka kufikia umri huo katika utumishi wake
amekutana na mambo mengi magumu, lakini kutokana na kumtegemea Mungu
zaidi ameshinda na kwamba akawaomba waumini wa Kanisa Katoliki kuendelea
kumwombea na kumpa ushirikiano ikiwa ni zawadi yao pekee .
Askofu Mkude aliteuliwa kuliongoza Jimbo Katoliki la
Tanga mwaka 1988 na aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa
Paulo II (kwa sasa ni marehemu), mwenye heri na miaka mitano baadaye
alihamishiwa katika Jimbo la Morogoro ambako amelitumikia kwa miaka 20
mpaka sasa
photo
MAASKOFU
UONGOZI WA BLOG HII UMEPATA NAKALA YA MKANDA WA VIDEO UNAOONYESHA TUKIO ZIMA LA NAMNA MLIPUKO WA BOMU KATIKA MKUTANO WA CHADEMA ULIVYOTOKEA. UONGOZI WA BLOG UNAWASILIANA NA WANASHERIA KUONA KAMA VIDEO HIYO INAWEZA KUBANDIKWA KATIKA BLOG HII. TUTAWAJUZA SOON
photo
BREAKING NEWS
Katika hali yakushangaza , mbunge wa
mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, mh. SUGU ameporomosha tusi
zito kwa waziri mkuu wa tanzania ( mh. PINDA ) akidai kuwa Tanzania haijawahi kuwa na waziri mkuu mpumbavu kama yeye.....
Tusi la Sugu limekuja baada ya
waziri mkuu kuwaruhusu rasimi polisi kutumia nguvu ya ziada
kuwadhibiti wananchi kwa kuwashushia kichapo ili wazitii
sheria.....
photo
SIASA
Baada ya mh.waziri mkuu mizengo pinda kutoa ruhusa kwa polisi kupiga
wananchi..Mh mbunge zitto kabwe nae atoa lake juu ya mh.waziri
mkuu...Kupitia tweet yake Zitto alisema "Viongozi wa kisiasa lazima
wajue kuweka akiba ya maneno yao ,kuropoka hovyo hovyo wakati kama huu
wenye taharuki ni hatari sana"..Aliongezea "Ni lazima viongozi
wawajibishwe kwa maneno wanayotamka.Mh. Pinda anahamasisha ukiukwaji wa
katiba na sheria Asipowajibishwa.!"
photo
SIASA
Taarifa
ambazo zimepatikana kwenye mitandao ya Ki-jamii zinaelezwa kuwa, jana usiku
katika kata ya Minepa jimbo la Ulanga Magharibi, vijana waliosadikiwa
kuwa wa “green guard” waliwavamia viongozi wa CHADEMA na kuwajeruhi...
Waliojeruhiwa ni Mwenyekiti wa Jimbo bw. Kibam Ally Mohammed (aliyevaa shati ya michirizi), Katibu wa Jimbo bw. Lucas Lihambalimo (aliyevaa shati jekundu) na Bw. Severin Matanila, Katibu Mwenezi tawi la Minepa (aliyekaa, mwenye bandeji), ndiye mlinzi wa mgombea.
photo
Majanga
KIPANDE CHA VIDEO KIKIOYESHA NAMNA MLIPUKO ULIVYOTOKEA
Kutoka kushoto mwenye Fulana Nyekundu ameumia vibaya sana, mtu wa pili kwake ni mwanadada Judy ambaye alipoteza maisha palepale. aliyeshika laptop ni mwana jamii forum
Baadhi ya Watoto waliokaa hapo juu ndiyo waliokufa na baadhi kuumia vibaya kwa bomu, hapo ndipo bomu lilipo angukia..
photo
Majanga