Jengo hili linaitwa New Planters,liko jirani na stesheni ya Reli ya Kimamba. Ni moja ya majengo kongwe katika mji wa Kimamba.

Kihistoria jengo hili lilikuwa likimilikiwa na Mgiriki tangu miaka ya 60 ambaye baada ya kufariki aliwaachia urithi wa jengo hili watoto wake wa kiume
Soko la Zamani la Kimamba
 Baadhi ya Makazi ya watu yanavyoonekana

Ofisi ya Stesheni ya Reli Kimamba
Hapa kuna mradi wa mashine ya kusaga na Kukoboa. Ni mradi wa wanakikundi akina mama.upo eneo la Mji mpya-Kimamba

photo

Soko la Kimamba

photo

 Kituo kikuu cha Mabasi cha Msamvu
 Baadhi ya Abiria wakigombea kuingia ndani ya Basi nje ya kituo cha mabasi cha Msamvu
Jamaa akishuka wakati basi likiwa katika mwendo karibu na Mzunguko wa Magari (Round About ya Msamvu).Ni hatari lakini Salama
 Round About ya Msamvu
Njia panda ya kwenda Chuo kikuu cha Mzumbe
 Mpishano
 Melela Mnadani-Njia Panda ya Kilosa,,panaitwa Melela

photo


Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akitoa mada katika Semina ya siku moja, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa ASILI YETU TANZANIA BLOG Bw. Victor Machota akiwa na Gadiola Emanuel mwenyekiti wa Arusha Bloggers Associations na Mkurugenzi wa WAZALENDO 25 BLOG katika Semina ya siku moja iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha. Kwa picha zaidi Bofya hapa>>>

photo ,

Emanuel Mabisa hakuwa mbali kumuaga Babu yake Mpendwa

photo

Leo Nyololo kwenye uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya mauaji ya Daudi Mwangaosi, Kulia ni Benson Kigaila,wapili kutoka kulia ni Mdogo wake marehemu mwangosi,anayefuata ni Winfrida,na wa kwanza kutoka kushoti ni naibu katibu mkuu,Chadema Zanzibar Hamad Yusuf

photo

Na Fatma Salum na Hassan Silayo- MAELEZO
Mfuko wa pensheni wa LAPF unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 35 katika mradi wa kituo cha mabasi eneo la msamvu Mkoani Morogoro.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa mfuko huo Kanda ya Mashariki Sayi Lulyalya alisema mradi huo ambao ni ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na mfuko wa LAPF unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu.

photo

Movie kali iliyorekodiwa kwa viwango vya kimataifa ya World of Benefit iliyohusisha mastaa kibao wa Kitanzania inaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa. 

Akizungumza na Timu ya Mwaipaja Blog, Mratibu wa Movie hiyo Macdenis Mgatha amesema kuwa Movie hiyo itaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa kwakuwa kila kitu kipo tayari kinachosubiriwa ni taratibu tu za namna ya kuiingiza kwenye soko.
Kila la Kheri World of Benefit

photo

Taifa letu linahitaji sana Busara kama zile za Waasisi wetu katika kipindi hiki chenye changamoto za kila namna kila kukicha

photo

Katika kuendeleza huduma ya Usaidizi wa Kisheria nchini Tanzania Mwanasheria Amani Mwaipaja amekuwa akiendesha vipindi vya Msaada wa Sheria Kwa njia ya Radio ambapo vipindi hivyo husikika live kupitia radio tatu tofauti za mkoani Morogoro ikiwemo Top Radio Fm- 99. 3 fm (Siku ya Jumatano Saa tatu Asubuhi), Radio Ukweli Fm 92.6 fm (Siku ya Jumatatu kuanzia saa tatu usiku na Radio Okoa Fm-106.2 fm (Siku ya Jumapili)

Picha ni Mwanasheria Amani Mwaipaja ambaye ni Mwasisi wa Blog hii akiwa na mwanadada Silvia Chilolo mara baada ya kumaliza kufanya kipindi cha Zijue Sheria ndani ya studio za Top Radio mjini Morogoro


photo



 Kundi la Vines ni moja ya kundi linaoimba muziki aina ya Acappella.
 Kundi la Acappella la Sonda ya Dilhu likiwa jukwaani likiimba kwa stail ya Acappella
Kundi la Caanan Brothers ni moja ya kundi linaloimba Acappella

photo

Tanganyika si ndoto tu, ni UKWELI wa kihistoria. Na ukweli unaishi. Unapitia hatua 3. 1. Ukiwekwa mezani hukataliwa, 2. Una gharama, kuwa wakati mwingine mwenye kuusema ajiandae kulipa gharama ya kuusema ukweli. 3. 

Udhihiri, kuwa hata ukifichwa chini ya uvungu wa kitanda kwa miaka 50, iko siku ukweli utatoka hadharani bila kusubiri kuvalishwa viatu. Na uhalali wake uanza kuhesabiwa tangu siku ile ulipokataliwa

photo

Kundi la Waimbaji wa Royal Advent Quartet wakiwajibika katika huduma ya Kiroho. Royal Advent ni moja ya makundi kongwe nchini Tanzania yanayoimba muziki wa Acappella (Muziki usiotumia vyombo vya Muziki). Kihistoria Muziki wa Acappella ni ni muziki wa kwanza kuimbwa duniani kabla ya ugunduzi wa vyombo vya muziki.
Mmoja kati ya waasisi  na mwanaharakati aliyepigania kwa kuutangaza muziki wa Acappella nchini Tanzania ni Ndugu Amani Mwaipaja ambaye kwa jitihada za pekee alifanikiwa kusajili taasisi ya Acappella Kwanza ambayo inasimamia shughuli za muziki wa Acappella nchini Tanzania. 

Katika historia ya Muziki wa Acappella nchini Tanzania, Tamasha la Kwanza la Muziki huo lilifanyika mwaka 2007 ndani ya Ukumbi wa Msimbazi Centre na kufanikiwa kuhudhuriwa na watu wengi ambao wengi wao walikuwa wakiusikia tu muziki huo kupitia radioni hasa Radio ya Morningstar ya Jijini DarEs Salaam..

Amani Mwaipaja mpaka sasa ni Mwenyekiti wa taasisi ya Acappella Kwanza ambayo mkao yako makuu yapo jijini Dar es Salaam. Moja ya Kikundi ambacho kimefanikiwa kujulikana sana miongoni mwa watanzania ni kundi la Acappella la The Voice ambalo lilijipatia umaarufu mkubwa kwa kutengeneza tangazo la mlio wa simu wa kampuni ya tigo

Mwaipaja Blog imefanikiwa kuongea na Mwenyekiti wa Acappella Kwanza Amani Mwaipaja ambaye ameiambia Mwaipaja Blog kuwa tamasha kubwa la Muziki wa Acappella linategemewa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Katika Picha hapo juu  toka kushoto ni Mtangazaji Maduhu, Mbaraka Mchome,Yona Japhet Msomi na Simon Mdee wakiimba kwenye mkutano wa makambi katika Kanisa la Waadventista Wasabato Morogoro Mjini july 7,2007.

photo

 Baadhi ya Vitu vinavyopatikana kwenye mnada wa Wami Dakawa
 Mbuzi hawa walishauzwa mapema
 Nyama Choma hupatikana kwa wingi
 Mbuzi Choma pia wapo

Baadhi ya Vibanda vinavyotoa huduma ya chakula na vinywaji

photo

Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, wakaati wa pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa wa Dunia uzito wa Super Middle (WBF) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu. Katika pambano hilo Bondi Mtanzania Francis Cheka ameweza kumgalagaza kwa Pointi mpinzani wake na kutwaa ubingwa huo.
*******************
Na Mwandishi Wetu
HATA hivyo pambano hilo pamoja na yale ya utangulizi yaliingia dosari baada ya wachezaji kama Alfonce Mchumiatumbo, aliyekuwa akizichapa na Chupac Chipindi katika pambano lao la utangulizi la raundi sita, kugoma kupanda ulingoni kwa kile walichokuwa wakieleza mabondia hao kuwa wanahitaji kumaliziwa pesa zao za mkataba wa kucheza mechi hizo kabla ya kupanda ulingoni. 
Nao mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali, pia waligoma kupanda ulingoni wakishinikiza kumaliziwa pesa zao kwanza jambo ambalo lilifanya kuzua taflani ukumbini hapoa huku mapambano yakichelewa kuanza.
Ilipofika muda wa Cheka kupanda ulingoni pia alisikika mtangazaji akimuita muandaaji wa mapambano hayo ili kufika chumba alichokuwa Bondia mtanzania, Francis Cheka ili kumalizana naye mkwanja ili akubali kupanda ulingoni.
Alisikika Cheka akimuwakia muandaaji huyo kuwa, '' Nini Mmarekani hata angekuwa Mchina, nimalizie changu kwanza ili nipande ulingoni, ambalo pia lilichukua muda wa majadiliano hadi kuingiliwa kati na wadhamini na wadau wa ngumi waliotangaza kujikomiti kulipa pesa hizo wanazodai mabondia, ndipo mabondia hapo wakapanda ulingoni.

Aidha katika pambano la raundi 10 la mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali la kuwania Ubingwa wa WBF wa Afrika, Thomas Mashali ameweza kumshinda kwa pointi 2 tu mpinzani wake Mada Maugo na kutwaa Mkanda huo wa ubingwa wa WBF wa Afrika.
Na katika pambano la Utito wa Juu la utangulizi la Raundi sita kati ya Bondia Alfonce Mchumiatumbo na Chupac Chipindi, Mchumiatumbo amemchapa kwa KO mpinzani wake katika raundi ya tano, baada Chupac kunyoosha mikono juu kuashiria na wasaidizi wake kutupa taulo ulingoni kuashiria kushindwa kumalizia mchezo huo.  
 Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (katikati) akipozi na mabondia Phill na Cheka, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pambano hilo la kimataifa.
 Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (wa pili kushoto) akimvisha Mknda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF Bondia Francis Cheka baada ya kumchapa kwa Pointi mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
 Mashabiki wa Cheka wakifurahi na kumbeba baada ya kutangazwa mshindi.
 Bondia Mmarekani Phill Williams (kulia) akichapana na Francis Cheka wa Tanzania katika pambano lao lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Mabondia hao wakiliana Timing.......
 Cheka (kulia) na Phill wakichapana......
 Cheka (kulia) na Phill,wakiendelea kuchapana 
We subiri inakuja hiyooooo
 Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani. kwa Picha Zaidi Bofya hapa>>>

photo ,