Rais wa chama cha riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akiwa Moscow |
Wakati nchi za ulimwengu zikiwakilishwa na wanariadha wake
mahiri katika mashindano ya dunia ya riadha mjini Moscow Urusi, Tanzania
imevunja rekodi ya aina yake kwa viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania
kutangulia Moscow huku wakiwaacha wanariadha nyuma.
Rais wa RT (aliyechaguliwa kinyume na katiba) bila wasiwasi,
aibu wala uzalendo amekwenda Moscow wiki iliyopita huku walengwa wenyewe wa
mashindano ya (World Athletic
Championships) ambao ni wanariadha wanaotegemewa kupeperusha bendera ya
Tanzania na kupigania medali wakibaki nyuma.
Cha ajabu zaidi ni pale ambapo kiongozi huyo wa RT
alipofuatana na kiongozi wa zamani wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa hana
uzoefu katika mikutano ya Chama Cha Riadha duniani (IAAF), kitu ambacho kinafanywa
kuwa kisingizio cha viongozi hao kutangulia.
Kimsingi kiongozi huyo wa zamani alikusudiwa kuwa kama kocha
mwandamizi atakayefuatana na wachezaji, ila sasa imekuwa sawa na rubani
kuwaacha abiria nyuma. Sijawahi kusikia kocha wa Taifa Stars akitangulia wiki moja kabla kwenye viwanja vya matukio
bila kuongozana na wachezaji wake, lakini kwa sababu RT ni mali ya TOC hakuna
cha kushangaza hadi hapo, watanzania waendelee kutafakari kwa kina tabia hiyo
mbaya inaendekezwa na nani, na kwa masilahi ya nani?.
Je inawezekana kwamba rais huyo mtata wa RT anazungukwa na
wajanja waliokwishaonja utamu wa fedha za makampuni yaliyowahi kutudhamini?, nikimaanisha
huenda kuna mpango unasukwa wa kuitapeli makampuni kama ilivyokuwa PUMA na LINING?. Ili kiongozi huyo wa RT mgeni asiyeelewa ‘umafya’ wa viongozi wa sasa na wa
zamani wa TOC wenye ushawishi mkubwa RT kutumika tu kama chambo (cheo) ili
wajanja wale ‘sinia kubwa’ wakati
kiongozi mpya akifurahia posho (per day)
huku taifa likiendelea kupoteza sifa katika viwanja vya mchezo wa riadha, ‘masikini taifa limetelekezwa na wahusika’.
Ambao wangechunguza kiini cha matatizo ya TOC na RT taifa lingekombolewa.
BMT na wizara inayohusika na michezo inastahili kuwa na
hisia ya maumivu pale Tanzania inapojikuta nyuma kila wakati panapotokea
mashindano ya kimataifa, swali muhimu ni; Je wahusika wa TOC na RT wanalindwa
na nani?, na ulinzi huo ni kwa masilahi ya nani?, na ulinzi huo utaendelea hadi
lini?. Fuatilia Blog yake hapa www.gidabuday.blogspot.com
0 Responses so far.
Post a Comment