Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mb),
(Mwenye kaunda suti nyeusi) akisalimiana na Makamanda wa JWTZ mara baada
ya kupokelewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali
Samuel Ndomba (Aliyesimama kulia kwa Mhe. Waziri) muda mfupi kabla ya
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya
kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa
Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko
mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye
silaha na makomando kulengea shabaha.
Makomando
wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila
shilaha wakati wa ziara yake.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo
yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani).
Komando
wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita
juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu
alilopewa.
Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ
wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja
hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo
zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
0 Responses so far.
Post a Comment