Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Comminication, Samuel Nyalla (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Saed Kubenea kutoka Mwanahalisi Publishers na Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akisalimiana kwa kumbatiana na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari.
 Wadau na wamiliki wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wanahabari na wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale
WAMILIKI wa Vyombo vya habari nchini (MOAT) wameitaka serikali kutosaini muswada wa vyombo vya habari kutokana na kutokuwa wa haki na kwamba unavibana vyombo vya habari.

Pia wamiliki hao wamesema kama serikali inataka kuupitisha isubiri Rais ajaye ndiyo aupitishe wakati huohuo wameunda kamati maalumu itakayoenda Mjini Dodoma kuuzuia usipitishwe wala kujadiliwa bungeni.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi  alisema anashangazwa sana na wanasisa kusahau walipotoka kutokana na kusapoti muswada huo kupitishwa.

Alisema serikali imeamua kufanya hivyo kutokana na kusahau waliowasababishia kupata madaraka kutokana na shida yao kuisha hivyo vyomba vya habari vimejifunza.

"Tumejifunza kuwa sisi ni8 watu wa kutumika  wanapotaka kututumia hivyo wanataka kutumaliza na muswada huu hivyo sioni kama wana nia njema na sisi, "Alisema Mengi.

Aliongeza nia ya kupitishwa kwa muswada huo so njema na kwamba haki ya kupata habari sio tuu haki ya msingio bali ni ya kikatiba hivyo serikali isije ikajihusiasha na kuvunja katiba ya nchi bali inatakiwa kuonesha mfano bora.

Akizungumzia kuhusu Demokrasia alisema mtu hawezi kufanya vitu visivyozingatia demokrasia ili kudhibiti demokrasia au kuhakikisha unapata demokrasia kwa kutumia njia za kidemopkrasia bali anapaswa kutumia amani.

"Huwezio kuheshimu sheria kwa kutumia nguvu, hivyo muswada ukiwa na sheria onevu na isiyokubalika au kukiuka katiba ya nchi lazima hali itakuwa mbaya nchini,"

Kwa upande wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu alisema watanzania tunaelekea kwenye mchakato huo lakini hatuwezi kuwa na uchaguzi huru ikiwa vyombo vya habari havina uhuru wa kupokea na kuandika habari ili watanzania waweze kuelewa hivyo serikali inatakiwa kujadili kwa makini ili kunusuru machafuko yanayoweza kujitokeza.

"Hatuwezi kuficha vitu wakati mambo yanatakiwa yawe wazi, na kama tungekuwa tunataka uwazi tusingeruhusu vyombo vya habari kuwa wazi, hivyo muswada huo utatupa matatizo kwenye uchaguzi na hauwezi kluwa huru pasipo wananchi kujua nuini kinaendelea kupitia vyombo hivyo,"alisema Mengi. 

Hata hivyo mengi aliongeza kuwa hakuna amani endelevu bila kuwepo uhuru na haki kwa kuwa ni rasilimali kubwa ya taifa na kwamba si ya mtu mmoja, kikundi wala chama bali ni yetu sote hivyo serikali ikijaribu kuichezea itakuwa inacjhezea wananchi wa tanzania.

Kwa upande wake Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Godfrey Mpandikizi  akizungumzia changamoto zilizopo kwenye muswada huo,alisema vitu vilivyopo kwenye muswada huo vinakinzana na katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hivyo aliwataka wahariri kwenda Dodoma kuuzuia.

Alisema muswada huo pia unazuia jamii kujua mambo yanayoendelea hivyo itasababisha hali ya nchi kuwa mbaya kwa siku zijazo kurtokana na kuwa na mapungufu zaidi ya 10 katika kila kifungu pamoja na tafsiri zaidi ya 20.

"Sheria hiyo ni chafu, na hairuhusiwi kwenda bungeni hivyo isubiri Rais ajaye na katiba mpya ndiyo ujadiliwe ili uwe na haki hivyo wamiliki nendeni Dodoma mkauzuie usijadiliwe na wabunge waka kupitishwa,"alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mwananchi, Francis Nanai aliwataka wamiliki hao kuonana na wanasheria, wabunge na mashirika mengine kwenda mahakani kupinga sheria hiyo chafu.

Abdala Majura alisema anaungana na vyombo mablimbali vya habari kuukataa muswada huo usijadiliwe bungeni na kwamba utasababisha kufa kwa taaluma za uandishi wa habari. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com).

photo ,


ACACIA has been operating in Tanzania for over a decade and during that time the company has made a significant progress in mining industry in the country. To value this achievements, in the beginning of this year 2015, Acacia has recognized it's employees by rewarding them, some for long service and others for their outstanding performance under the company's six desired behaviors' culture.

All team members are exposed to a unique world class Cultural Transformation Programme, called Tufanikiwe Pamoja. The Programme embeds the Company's expectations and the accountabilities of every leader and team member with respect to their behavior and approach to work.
To ensure a high performance culture and become the best Company in Africa, the company has articulated six desired behaviors which all team member  are expected to practice. These including, "We plan the work and work to  plan, We hold people accountable and recognise performance, We work as a team (collaborate) and communicate openly, We do what we say we will do, We act with a sense of urgency, We develop our people to do their best".
At the end of this week it was the turn of Acacia Dar office employees, where 46 employees were awarded for a long service at a colorful event  held on Friday evening at the company's main office along Bagamoyo road. Long servicing employees is the company's Buzwagi, North Mara and Bulyanhulu gold mine sites have also been rewarded since last month.
Those recognized on Friday were the staff who worked for 5, 10 and 15 years, since the company commenced it's operation in Tanzania. The awards were meant to show the company's appreciation for the workers commitment and loyalty that's reflected by their long years of service.
Acacia’s top leadership,DeoMwanyika, (First-L), Peter Gelete, (2rd-L), Andrey Wrey, (3rd-R), Asa Mwaipopo, (2nd-R), and Janet Reuben Lekashingo, (First-R),  pose for a group photo with two awards’ recipients of 15 years of service, Hamisi Hussein Juma, (3rd-L), and Omary Ally, (4th-L), during the awards giving ceremony held at the main office off Bagamoyo road in Dar es Salaam
Acacia’s Executive General Manager, Organisational Effectiveness, Peter Geleta, (L), presents a certificate of appricietion for long service, to the company’s Head of Government Relations, Alex Lugendo, during the awards giving ceremony held at the main office along Bagamoyo road, Friday May 22, 2015. Lugando joined the company 5 years ago.
Acacia’s Vice President, (Corporate Affairs), Deo Mwanyika, delivers his speech during the awards giving ceremony held at the company’s main office in Dar es Salaam.
Acacia’s Chief Financial Officer, (CFO), Andrew Wrey, makes his speech.
Acacia’s General Manager, Organizational Effectiveness Janet Reuben Lekashingo, (L), presents a certificate of appreciation to Bonifacia Bernard Mlenga, from aviation department during award giving ceremony for long service.
Acacia’s Vice President (Corporate Affairs), Deo Mwanyika, (L), presents a certificate of appreciation to the company’s Chief Advisor Occupational Health and Safety Zumbi Musiba, who joined the company 10 years back.
Vice President Corporate Affairs, Deo Mwanyika, (R), joins the representatives from all three groups, to cut a cake to signify the award giving ceremony success.
Acacia’s Vice President, (Corporate Affairs), Deo Mwanyika, (C), Chief Financial Officer, Andrew Wrey, (4th-R), Executive General Manager, Organisational Effectiveness, Peter Geleta,, (3rd-L),  GM Sustainability Asa Mwaipopo, (3rd-R), GM Organizational Effectiveness, Janet Reuben Lekashingo(First-R), pose for a group photo with awards’ recipients of 10 years of service, left to right, Caroline Lucas Materu, Ritesh Divecha, Joseph Mbanya, and the company’s Chief Advisor Occupational Health and Safety, Dr.  Zumbi Musiba.
Acacia’s employees, carry a balloon named Acacia, to show the spirit of working as a team (collaborate), during the event.
Elated awards’ recipients display they certificates to a photographer.
Acacia’s top leadership poses for a group photo with awards’ recipients of 5 years of service.
Acacia’s Sustainability General Manager Asa Mwaipopo, presents a certificate of appreciation to the company’s Corporate Community Relations Manager Stephen Kisakye for long service.

photo ,


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mkoani Morogoro. Waziri Magufuli amewapongeza TANROADS kwa utendaji kazi wao mzuri ujenzi wa Barabara nchini.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma risala kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli.TANROADS imepata TUZO ya mfanyakazi bora na mwajiri bora kutoka TAMICO.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa ameshikana mikono na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara, TANROADS Eng. Patrick Mfugale kushoto pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe kulia wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS.
Baadhi ya Wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia tuzo aliyokabidhiwa na Wafanyakazi wa TANROADS kwa kutambua uongozi wake bora katika kuanzisha na kule Wakala huo tangu mwaka 2000-2015.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mara baada ya mkutano uliofanyika mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mkoani Morogoro. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

Waziri wa Ujenzi DKT, JOHN MAGUFULI amewataka wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANRODS), kufanyakazi kwa ubunifu,uzalendo na uadilifu ili kuharakisha maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

Akifungua mkutano wa tano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mjini Morogoro Waziri Magufuli amesema asilimia 14.3 ya pato la taifa linatokana na kukua kwa sekta ya usafirishaji ambayo asilimia 99.3 ya usafirishaji wote nchini unatumia barabara.

“Ni asilimia 0.7 tu ya bidhaa zote nchini zinatumia usafiri wa anga,reli na bahari hivyo ni wazi kuwa sekta ya barabara ni nguzo  muhimu ya uchumi wa nchi”, amesisitiza Waziri Magufuli.
Waziri Magufuli ameipongeza TANROADS kwa mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha miaka 15 tangu ianzishwe na kufanikiwa kuwa mwajiri bora wa TAMICO mwaka 2014/2015.

Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe amepongeza TANROADS mkoani Morogoro kwa kazi nzuri wanazofanya na kuitaka kushirikiana na taasisi nyingine katika kudhibiti ajali za barabarani.

Amehimiza umuhimu wa TANROADS kudhibiti magari yanayoegeshwa kiholela barabarani  na kuongeza mizani zinazotembea ili kudhibiti uharibifu wa barabara unaosababishwa na magari kuzidisha uzito.

Akizungumza katika Baraza hilo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS na Mwenyekiti wa Baraza hilo Injinia Patrick Mfugale amewataka wajumbe kuwa huru ili kuwezesha kujitathmini  kwa haki na hivyo kuongeza tija katika utendaji kazi.

Injinia Mfugale amewataka Wahandisi kuwa wabunifu na wanaozingatia thamani ya fedha ili miradi ya ujenzi idumu kwa muda mrefu na kuchochea maendeleo ya nchi.

Amesema TANROADS imechaguliwa kuwa ya tatu kwa utendaji bora wa kazi kwa taasisi za ujenzi barani Afrika ikitanguliwa na nchi za Afrika Kusini na Namibia.

TANROADS ilianzishwa mwaka 2000, kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa barabara kuu na za mikoa hapa nchini ambapo hadi sasa inasimamia ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 35,000.

photo ,


DSC_0023
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia), Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na mkalimani wa Balozi wa China wakifurahi jambo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani) akiwasili kwenye chumba cha mikutano Wizara ya Elimu kwa ajili ya hafla fupi ya kutiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Modewji blog team
SERIKALI na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana wametiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini.

Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema mradi huo ni mkombozi mkubwa katika maandalizi ya kufundisha kwa kutumia Tehama nchini.

Alisema mpango huo wenye kuwezesha walimu kujifunza Tehama unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ambao ndio wamepitisha fedha zao UNESCO.

Katika utiaji saini huo ambapo Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing alikuwepo, katika jumla ya uhai wa mradi ambao ni miaka miwili , miundombinu ya ufundishaji masomo ya sayansi na hesabu katika vyuo vya walimu vya Monduli na Tabora itaboreshwa.

Katika mradi huo walimu watafundishwa elimu ya Tehama, namna ya kufundisha na kujifunza.

Katibu mkuu Mchome alisema kwamba vyuo hivyo viwili vitawezeshwa kuwa na mtandao ambao utaunganishwa na vyuo vingine vinane vya masomo ya sayansi na hesabu kwa ajili ya kubadilishana taaluma.
Pia vyuo hivyo vitawezeshwa kuandaa programu zenye kuelezea mfumo wa utoaji huduma za Tehama kwa ajili ya walimu wa masomo ya sayansi na hesabu.
DSC_0037
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimina kwa furaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na kushoto ni Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (aliyeipa mgongo kamera).

Profesa Mchome alisema ili taifa liweze kusonga mbele katika mpango wake wa kufundisha kwa kutumia Tehama ni vyema kuandaa walimu na fedha za China kupitia Unesco zitasaidia maandalizi hayo.

“Tunaamini tukiwekeza katika vifaa vya kupromoti Tehama, walimu wakifundishwa na kuandaliwa vyema, wataenda kusaidia kufundisha na kuwezesha matumizi ya Tehama katika shule zao.” Alisema Profesa Mchome.
Alisema japo zipo program ndogo nyingine , program waliyotia saini jana ilikuwa kubwa na yenye tija itakayoimarisha ubora wa elimu kwa kuwapa wanafunzi elimu ya kujitegemea, elimu yenye kuwakwamua kiujuzi na kuutumia ujuzi huo kwa maendeleo yao na taifa.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa barani Afrika ambayo mapema wametambua thamani ya kufundisha kwa njia ya Tehama ili kuboresha elimu na mfumo wa elimu.

Taasisi zitakazohusika na mradi huo ni pamoja na Chuo Kikuu Huria (OUT) na Taasisi ya Elimu nchini(TIE) kwa kuratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
DSC_0074
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) pamoja na Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto) kabla ya kutiliana saini mkataba huo.
DSC_0080
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo kabla ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome na Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi. Waliosimama wakishuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Joel Nanauka wa UNESCO, Afisa tawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem, Afisa mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi, Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing, Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha.
DSC_0084
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome wakitiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing (wa pili kushoto), Ofisa anayeshughulikia masuala ya elimu kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar (wa pili kulia), Afisa mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha na Kulia aliyeketi ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0086
Zoezi la kusaini mkataba likiendelea.
DSC_0089
Wakifurahi kwa pamoja mara baada ya zoezi la kutia saini kukamilika.
DSC_0090
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome wakibadilishana hati za mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing(wa pili kushoto) pamoja na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia).
DSC_0091
DSC_0103
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo baada ya kutiliana saini mkataba huo.
DSC_0068
Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia) akizungumza jambo na Afisa wa ubalozi wa China (katikati) na Kushoto ni Afisa Utawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem.

photo , , ,