Mkurugenzi kwa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.
Brass Band ya JWTZ ikitumbuiza kwenye Maadhimisho hayo wakati wa kuimba Wimbo wa Taifa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade akitoa hotuba yake kwenye kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bernard Mchomvu akitoa hotuba yake kwenye kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Adam Malima akitoa nasaha zake kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika  Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bernard Mchomvu.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha akitoa hotuba yake katika kilele cha Maadhimisho hayo yaliyofanyika Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.

Sehemu ya Wageni waalikwa kutoka nchi mbali mbali wakifatikia kwa makini hotuba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade (hayupo pichani) aliyokuwa akiitoa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yussuf Mwenda akiwa kwenye Mkutano huo wa kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya akifatilia kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa Mkutanoni hapo.
Sehemu ya Wadau wa TRA wanaoongoza kwa Ulipaji Kodi wakiwa kwenye Mkutano huo.

Sehemu ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa kwenye Mkutano huo wa kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Wachekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi wakiwa ni sehemu ya waalikwa kwenye Maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Novemba 21,kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.Toka kulia ni Seki,Masanja,Joti,LeProfeseli,Wakuvywanga na Mpoki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala,Kamishna wa Polisi Msaidizi Mwandamizi (SACP) Mary Nzuki akifatilia jambo wakati wa Mkutano huo wa kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Wachekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi kwa nyakati tofauti wakitoa burudani kwa washiriki wa Mkutano huo wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mlipa Kodi yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
MC Taji Liundi "Master T" akiwa kwenye tabasamu la nguvu kutokana na vichekesho vya Orijino Komedi.
Meza Kuu.
Massanja Mkandamizaji akimwaga maombi ya nguvu ukumbini hapo.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade akitafakati jambo.

Mkutano ukiendelea.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade akimpatia tuzo ya heshima Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya.
Washindi wa Tuzo mbali mbali.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha (kulia) amkimkabidhi Kombe na Cheti,Meneja wa Kodi wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC),Godfrey Ferdinand baada ya kuibuka washindi wa tatu kwa Walipa Kodi hodari.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha (kulia) amkimkabidhi Kombe na Cheti,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania,Rene Meza baada ya kuibuka washindi wa pili (kati ya Watatu Bora) kwa Walipa Kodi hodari.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha (kulia) amkimkabidhi Kombe na Cheti,Meneja wa Huduma za Pamoja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Alois Maleck Qande kwa kuibuka mshindi wa kwanza (kati ya Watatu Bora) kwa Walipa Kodi hodari.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Washiri watatu wanaolipa kodi vizuri.Washindi hao ni TBL (kulia),Vodacom (pili kushoto) na TCC (kushoto).
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha (kulia) akimkabidhi Kombe na Cheti,Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Tanzania Distilleries,Michael Brown (wa tatu kushoto) kwa kuibuka washindi wa jumla kwa walipa kodi wote Tanzania.
Picha ya pamoja na Makamishna Mamlaka za Mapato za nchi mbali mbali Barani Afrika.
Picha ya Pamoja na Washindi mbali mbali.

photo , , ,
Links to this post


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.

Alielezea kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.

Mhe. Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
 Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu  hicho katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe 21.11.2014.
  Mhe. Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi  (mwenye kofia ya njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi  Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa mahafali hayo ya kumi na moja.
 Shekhe Dr.Badruh H.Sseguja akifungua kwa sala Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
  Mchungaji Ogah Ogbole akifungua kwa sala mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba ya ufunguzi wa  mahafali hayo ya kumi na moja ya chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwa utulivu tayari kabisa kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 902 walihitimu masomo yao.
 Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakiingia katika viwanja vya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam tayari kwa mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja.
   Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja ambapo aliwaasa kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
 Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala wakinyanyua kofia zao juu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali yao ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo wakifuatilia hatua kwa hatua kile kinachoendelea katika sherehe hizo.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala akitunuku shahada kwa wahitimu wa mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi ( mwenye joho la njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Membe pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo wa taifa kama ishara ya kufunga mahafali hayo ya kumi na moja.
 Mgeni rasmi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali hayo.   PICHA NA Reuben Mchome 

photo , ,
Links to this post