Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akikata utepe kama ishara ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akifungua bomba la maji kama moja ya zoezi lililofanyika wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akinawa mikono yake kwa maji safi na salama wakati wa kiongozi huyo akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akimtwisha ndoo ya maji bi. Asha Omary wa kijiji cha Mseta Wilayani Kongwa mara baada ya kiongozi huyo kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji ulioanza kuhudumia wananchi kijijini hapo mapema jana (Machi 22,2015) wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akiwasilisha hotuba yake ya kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya maji Mkoani Dodoma yaliyofanyika Kijiji cha Mseta Wilayani Kongwa MACHI 22, 2015.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mseta Wilayani Kongwa wakiserebuka ngoma za asili wakati wa sherehe za kilele cha wiki ya maji Mkoa wa Dodoma zilizofanyika kijijini hapo Machi 22,2015.

photo

Leo tarehe 22.03.2015 Viongozi Waandamizi wa Tuzo ya Jamii wapo safarini Kuelekea Bungeni Dodoma ambapo kati ya tarehe 23-24 March 2015 watakuwa wageni wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika ziara hiyo Viongozi hao watajifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bunge na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge
Walio katika Msafara
1.DJ Malegesi      
2.Amani Mwaipaja 
3.Sylvester N. Mayunga
4.Joan Msumi
5.Rachel Kassanda
Viongozi wa Tuzo ya Jamii, Kushoto ni Dk. Mayunga na DJ Maregesi wakiwa katika viwanja vya Bunge leo Asubuhi.

photo ,

Mwenyekiti Tanzania Awards International Ltd,Deonatus Julius Malegesi akizungumza na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam kuhusu Tuzo ya Jamii 2015
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Tuzo ya Jamii 2015 Mhandisi Sylvester Mayunga akifafanua jambo



Waandishi wa Habari wakifuatilia





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUZO YA JAMII ITAKAYOTOLEWA TAREHE 13 APRIL 2015 KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE, JIJINI DAR ES SALAAM

MGENI RASMI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete

WAGENI WAALIKWA:
Mara baada ya Hafla ya Tuzo ya Jamii ambapo Washindi wote watapewa Tuzo na Mgeni Rasmi, Kutakuwa na Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii ambayo itahudhuriwa na wageni wafuatao:

  • Wapewa Tuzo,
  • Familia za wapewa Tuzo,
  • Viongozi Waandamizi wa Serikali,
  • Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania,
  • Viongozi wa vyama vya siasa na kijamii na Wafanyabiashara,
  • Taasisi zisizo za kiserikali,
  • Watu Mashuhuri na
  • Wawakilishi kutoka makundi yenye mahitaji maalum ambapo kwa mwaka huu watawakilishwa na Watu wenye Ulemavu wa Ngozi-Albino

MUHIMU:
Tanzania Awards International Ltd imepanga kufanya hafla ya utoaji wa Tuzo ya Jamii na kisha Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii siku ya tarehe 13 ya mwezi April ya kila mwaka kwa malengo ya kuadhimisha Kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa  Baba wa Taifa,  Hayati Mwalimu Julius Kambarege Nyerere.

Kuhusu Tanzania Awards International Limited
Tanzania Awards International Limited ni kampuni iliyosajiliwa kisheria nchini Tanzania kwa Malengo ya Kufanya tafiti mbalimbali, Kutoa ushauri wa kisheria na kijamii, kuandaa na kuratibu matukio pamoja na Uandaaji na Utoaji wa Tuzo Ya Jamii.

Maana ya Tuzo ya Jamii
Tuzo ya Jamii ni Tuzo inayotolewa kwa Taasisi na Watu binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zao katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.


Malengo ya Tuzo ya Jamii
  • Kutambua, Kuthamini, Kuunga Mkono na Kutoa Tuzo kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.

  • Kuikumbusha Jamii kuona umuhimu, kujali na Kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi au Mtu Binafsi katika kuleta Ustawi na Maendeleo ya Jamii

VIPENGELE VYA TUZO YA JAMII 2015
Vipengele vya Tuzo ya Jamii, hubadilika kila mwaka kulingana na aina na matokeo ya Utafiti unaofanywa na Tanzania Awards International Limited. Kwa mwaka huu (2015), Tuzo ya Jamii itakuwa na Vipengele Vikuu vinne (4) vifuatavyo:

  1. Tuzo ya Jamii 2015
  2. Tuzo ya jamii –Tuzo ya Heshima
  3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu
  4. Tuzo ya Jamii kwa Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania

UFAFANUZI WA KILA KIPENGELE CHA TUZO YA JAMII 2015

  1. Tuzo ya Jamii 2015
Tuzo hii itatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na mchango na jitihada zake katika kusaidia na kutetea Jamii.

Mshindi wa Tuzo hii ya Jamii atapatikana kwa:

(a)   Mhusika mwenyewe kuwasilisha vielelezo au ushahidi wa mchango wake huo kwa Jamii
AU
(b)   Kwa jamii kupendekeza jina la mhusika kupitia mitandao ya kijamii
AU
(c)    Kwa Kamati ya Tuzo ya Jamii kufanya utafiti, kuchambua na kuteua jina moja miongoni mwa yale yaliyopatikana kupitia kipengele (a) na (b)

Mshindi wa Tuzo ya Jamii 2015 atatangazwa rasmi siku ya Hafla ya Tuzo ya Jamii itakayofanyika tarehe 13 April 2015 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre, Jijini Dar es Salaam

2. Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima
Watakaopewa Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima ni:
(a)  Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na

(b) Hayati Nelson Mandela –Rais wa Kwanza Mzalendo wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini
Tuzo hii ya Heshima kwa mwaka huu itatolewa kwa Waasisi hao wawili kutokana na Jitihada na Mchango wao wa kipekee na uliotukuka katika kutetea na Kulinda Maslahi ya Wanyonge



3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu
Tuzo hii inatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika Kuelimisha, kulinda, kutetea na Kuimarisha Utawala Bora nchini Tanzania

Vigezo vinavyotumika kwa mwaka huu katika kumpata mshindi wa Tuzo ya Jamii ya Haki za Bianadamu, ni hivi vifuatavyo:

·         Weredi wa Taasisi au Mtu Binafsi katika kufanya uchunguzi, Utafiti na kutoa taarifa zake kwa uhuru, pasipo upendeleo wowote kwa Serikali, Chama, Kikundi au mtu Binafsi
·         Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika Kuelimisha Jamii,  kulinda, kutetea na kuhamasisha juu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania.

·         Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha juu Amani, utulivu, Usalama wa Raia na Mali zao na Utii wa Sheria kwa ujumla

  1. Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania

Mshindi wa Tuzo hii atatangazwa siku ya hafla ya Tuzo ya Jamii baada ya mwanasiasa husika kupigiwa kura nyingi kupitia mtandao wa Push mobile ambapo mpigaji wa kura anatakiwa aende sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake ya Mkononi na kuandika namba ya Mwanasiasa husika, alafu anatuma namba hiyo kwenda 15522.

Vigezo vitakavyotumiwa na wapiga kura kupitia namba 15522 ni hivi vifuatavyo:

  • Uadilifu, Uaminifu, Heshima na Utii kwa Jamii na sheria za nchi kwa Amani ya nchi yetu

  • Jitihada binafsi katika kulinda na kutetea Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar, Umoja wa Kitaifa na Kijamii

  • Uzoefu wa Uongozi wa Umma, Taasisi za Kimataifa na Mchango wake kwa Jamii.

  • Matarajio, Mipango na nia ya Dhati ya Kuleta Maendeleo na Mafanikio kwa Watanzania

Orodha ya Wanasiasa wanaowania Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Kijana na Mtu Mzima Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania imepatikana baada ya wanajamii kupendekeza mara nyingi jina la Mwanasiasa husika kupitia Mtandao wa Push Mobile na mitandao mingine ya kijamii. Kamati ya Tuzo ya Jamii, baada ya kupitia majina yote yaliyopendekezwa kupitia mbalimbali ikiwemo Push Mobile, imepata orodha ifuatayo:

WATU WAZIMA
JINA LA MWANASIASA
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
MHE. MIZENGO PETER PINDA
MM01
MHE. PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO
MM02
MHE. DR. WILBROD PETER SLAA
MM03
MHE. ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO
MM04
MHE. SAMIA HASSAN SULUHU
MM05
MHE. JAMES FRANCIS MBATIA
MM06
MHE. DR. JOHN POMBE MAGUFULI
MM07
MHE. DR. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE
MM08
MHE. PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA
MM09
MHE. STEPHEN MASATU WASIRA
MM10
MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA
MM11
MHE. BENARD KAMILIUS MEMBE
MM12
MHE. EDWARD NGOYAYI LOWASSA
MM13

VIJANA
JINA LA MWANASIASA
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
MHE. JANUARY YUSUPH MAKAMBA
MK01
MHE. ZITTO ZUBERI KABWE
MK02
MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA
MK03
MHE. HALIMA JAMES MDEE
MK04
MHE. SAADA SALUM MKUYA
MK05
MHE. LAZARO SAMUEL NYALANDU
MK06
MHE. ESTHER AMOS BULAYA
MK07
MHE. UMMY ALLY MWALIMU
MK08
MHE. NAPE MOSES NNAUYE
MK09
MHE .MBONI MHITA
MK10
MHE. DAVID ZACHARIA KAFULILA
MK11
MHE. VICKY PASCHAL KAMATA
MK12
MHE. JOHN JOHN MNYIKA
MK13

Hatua hii ya upigaji wa kura ni hatua ya mwisho katika mchakato wa kumpata mshindi wa Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania (Kijana na Mtu Mzima). Aidha, katika uamuzi wa Mshindi, matokeo ya upigaji wa kura yatachukua asilimia Sabini (70%) na Asilimia Thelathini (30%) zitatumiwa na Majaji ambao ni Kamati ya Tuzo ya Jamii 2015.
Zoezi la kumpigia kura Mwanasiasa Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania limeanza tarehe 10/03/2015 na litaendelea hadi tarehe 13/04/2015.

MCHAKATO WA JUMLA WA KUWAPATA WASHINDI NA KUWATANGAZA
Uendeshaji wa Mchakato wa utoaji wa Tuzo ya Jamii huanzia kwenye Kitengo cha Utafiti, Kumbukumbu na Majadiliano. Kitengo hiki, ndicho chenye jukumu la kufanya tafiti mbalimbali kuhusiana na jambo husika.

  • Kitengo cha Utafiti, Kumbukumbu na Majadiliano, kinapomaliza kazi yake ya Utafiti,huwasilisha mapendekezo yake kwenye Sekretarieti ya Kampuni ambayo inaundwa na wakuu wote wa vitengo vya kampuni pamoja Wajumbe wengine watatu ambao hufanya idadi yao kufikia saba (7). Kazi ya Sekretarieti ni kupitia taarifa kutoka kitengo cha ya Utafiti, kuichambua na kutoa mapendekezo yake na  kuyawasilisha kwa Uongozi wa Kampuni.

  • Taarifa ya Sekretariat huwasilishwa kwa uongozi wa Kampuni kwa ajili ya mapitio, mapendekezo au kwa uongozi kufanya mawasiliano na Vyanzo mbalimbali kabla ya uongozi wa kampuni kuiwasilisha taarifa hiyo kwenye Kamati nzima ya Tuzo ya Jamii

  • Kamati ya Tuzo ya Jamii yenye Wajumbe ishirini na sita (26)  ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, hupitia, hujadili na  kuchambua taarifa nzima inayohusiana na kipengele husika cha Tuzo ya Jamii.

  • Kamati ya Tuzo ya Jamii baada ya kujiridhisha na uchambuzi iliyoufanya hupitisha, huthibitisha na kutangaza jina moja miongoni mwa yale yaliyohusishwa katika Utafiti husika. Maamuzi ya Kamati ya Tuzo ya Jamii huwa ni ya Mwisho.

  • Mhusika aliyeshinda Tuzo ya Jamii katika kipengele husika hupewa taarifa rasmi Kuhusu ushindi wake
Imetolewa Machi 18,2015
Na Deonatus Julius Malegesi
Mwenyekiti
Tanzania Awards International Ltd

photo , ,


 makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli  hii leo
Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro  (TLB), Protas Soka Akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo mbele ya mbunge wa jimbo la monduli
 Viongozi mbalimbali wa makundi ya kijamii wakiwa wanamkabidhi waziri mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa bahasha yenye fedha taslimu shilingi milioni mbili laki tano sitini na saba elfu na mia sita zilizochagwa na wananchi   kwa ajili ya kwenda kuchukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Urais
 mbunge wa jimbo la monduli akiangalia picha ambayo ametengenezewa na  vijana kutoka makundi wakati walipomtembelea nyumbani kwake monduli kwa ajili ya kumkabidhi fedha kidogo kwa ajili ya kuchukuwa fomu ya kugombea urais

 makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli  hii leo

 makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli  hii leo
Mratibu wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya Kaskazini, Noel Nnko,akiwa anamuonyesha picha ambayo ni ya kumbukumbu ya tukio la leo la kuja kumuunga mkono mbunge wa jimbo la monduli pamoja na kumuomba atangaze nia  ya kugombea nafasi ya urais
maandamano ya pikipiki yakiwa yanaelekea nyumbani kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
Na Woinde Shizza,Monduli
Wananachi zaidi ya 700 kutoka makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara, wamejitokeza nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowasa, wakimshawishi atangaze nia ya kugombea urais kupitia chama hicho.
Wananchi hao kutoka katika Makundi mbalimbali katika  ya  mikoa hiyo yamewasili leo nyumbani kwake,Kijiji cha Ngarashi, Wilaya ya Monduli baada ya kufanya maandamano makubwa yaliyoanzia njia panda ya Monduli, wakiimba nyimbo za matumaini kwamba 'wewe ni tumaini la walio wengi Tanzania, maamuzi na matumaini mapya, watanzania wako nyuma yako'.
Aidha akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo baada ya kuwasili nyumbani hapo , Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro  (TLB), Protas Soka alisema kwa nia thabiti isiyo na kigugumizi asilani, wanaharakati hao pamoja na watanzania wengine wanamhitaji  (Lowasa) kwa unyenyekevu na hivyo, wanamwomba atangaze nia ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2015.
"Leo watanzania tumepaza sauti zetu kwa pamoja kuanzia ngazi ya Kaya,Kitongoji,Kijiji,Kata,Tarafa,Wilaya, Kanda mpaka Taifa wakisema Viva Lowasa, Tobiko Lowasa. Kwa moyo mmoja bila kushawishiwa na mtu wala kikundi chochote;  wanaharakati hawa wamekuona wewe, mheshimiwa Edward Lowasa ndio kiongozi sahihi kwa mustakabali na manufaa ya taifa letu,"alisema Soka
Makundi hayo ambayo ni walemavu, waendesha bodaboda, walimu, wataalam wa afya, vijana na wanasiasa, walimchangia Lowasa kiasi cha shilingi milioni 2,567,600 kwa ajili ya kununua au kulipia fomu ya kugombea nafasi ya Urais pindi atakapotangaza nia.
"Kwa lugha nyingine sasa tunakuomba Mheshimiwa Lowasa sasa tunakuomba utangaze nia ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,"alisema Soka.
Makundi hayo yaliyoongozwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, Mratibu wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya Kaskazini, Noel Nnko,Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), mkoa wa Arusha, Robnson Meitinyiku, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Fred Mushi, Askofu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Christoher Madilu ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Abdalah Sadick kutoka mkoa wa Manyara.
Akizungumza mara baada ya kupokea makundi hayo mbunge huyo wa jimbo la monduli alisema kuwa amekubaliana nao na anatarajia kutangaza rasmi nia mwezi Aprili pindi tu chama chake kitakaporuhusu
 "Nitatangaza nia mwezi Aprili mwaka huu, pale uwanja wa Shekhe Amri Abeid mjini Arusha baada ya chama changu kupuliza kipenga. Ninachowaomba watanzania kwa sasa, mniombee katika safari yangu ya matumaini,"alisema Lowasa.
habari kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog

photo ,