President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly. 
  President Jakaya Mrisho Kikwete invites  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue and their delegation who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete bids farewell to Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
  President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete greets American civil rights activist and Baptist minister  Rev. Jesse Louis Jackson, Sr during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Mama Graca Machel when they met in Washington DC
 President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York.STATE HOUSE PHOTOS

photo , ,


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller wakati wa mkutano wa kuzungumzia masuala ya elimu kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya barani Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (wa pili kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika (wa pili kushoto). Aliyesimama wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi na wa kwanza kushoto ni Msaidizi wa Mke wa Rais wa Malawi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya masuala ya elimu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo ni sehemu ya Maandalizi ya Mkutano wa Mwaka wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya washiriki kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika ili wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa vijana wa bara la Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New York tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na wageni wengine mashuhuri wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kiafya ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani. Aliyekaa wa kwanza kushoto ni Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller akifuatiwa na Mama Getrude Mutharika na wa kwanza kulia ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Vijana Bwana Ahmed Alhendawi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Rais Malawi Mama Getrude Mutharika mwishoni mwa mkutano wa kujadili masuala ya elimu kwa vijana barani Afrika kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Aliyesimama katikati ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Dkt. Sheila Tlou, Mkurugenzi wa UNAIDS – Regional Support Team for Eastern and Southern Africa na Waziri Mstaafu wa Afya wa Botswana na kushoto ni Mke wa Rais wa Malawi Mama Getrude Mutharika mara baada ya kumalizika mkutano wa siku moja uliofanyika huko New York tarehe 22.9.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.

photo , ,


Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Lupembe (kulia) akimwagiwa maji baridi na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Ivan Tarimo (kushoto) akimwagiwa maji baridi na mmoja wa mfanyakazi mwenzake katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) naye akimwagiwa maji baridi ili kutimiza azma ya benki hiyo katika kutafuta fedha ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Binafsi na biashara ndogondogo na za kati, Isidori Msaki (katikati) akijitahidi kujizuia wakati wafanyakazi wenzake wakimmwagia ndoo za maji baridi katika hafla hiyo.
kaimu ofisa mwendeshaji mkuu wa benki ya nbc, Jamie Loden akijimwagia maji baradi ili kusaidia harakati za benki hiyo kuchangisha fedha katika tukio hilo liitwalo ‘Ice Bucket Challenge’ kusaidia wanawake wanaokabiliwa na ugonjwa wa fistula. Kiasi cha fedha kitakachopatika kitapelekwa katika Hospitali ya CCBRT kwa madhumuni hayo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Jaffari Matundu (kushoto) akimwagiwa maji na mfanyakazi mwenzake katika tukio la Ice Bucket Challenge lenye lengo la kukusanya fedha kusaidia wanawake wanaosumbulia na ugonjwa wa fistula.
Unaweza kuona kama mzaha Fulani lakini ndivyo ilivyokuwa kwa maofisa hawa wa NBC walipoamua kushiriki tukio la ‘Ice Bucket Challenge’ na kumwagiana maji baridi ili kuchangisha fedha kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula nchini.
Baadhi ya wakazi wa jiji waliojitokeza kushuhudia tukio la Ice Bucket Challenge la benki ya NBC wakiwa hawaamini macho yao wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipoamua kujimwagia maji baridi ili kutafuta fedha kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula.

photo , ,


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Assumpta Maina Mallya akizungumzia jinsi mfuko wa Pensheni wa PPF unavyoendeshwa katika Mkutano wa 24 wa wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha
Meneja Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw Selestine Some akizungumzia jinsi mfuko wa Pensheni wa PPF unavyoweza kutumia michango ya wanachama katika kulinda Michango.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mh Milton Makongoro Mahanga katika Mkutano wa 24 wa Wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha
 Mdau wa PPF akipitia jarida la PPF katika mkutano wa 24 wa Wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha
Wadau wakifuatilia Mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na viongozi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF katika Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa PPF Jijini Arusha
 
Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akiuliza swali katika Mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha
Wadau wa NSSF wakifuatilia Mada katika mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha
 Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifuatilia Mada mbalimbali zinazotolewa katika Mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha
 Mdau wa PPF akiuliza swali katika Mkutano wa 24 wa Wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha
 Meza Kuu
Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akipitia Jarida la PPF katika mkutano mkuu wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.Picha zote na Josephat Lukaza- Lukaza Blog Arusha

photo , ,


 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Godfrey Mtei akipokea zawadi ya saa ya ukutani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, juzi mjini hapa.
 picha ya pamoja .
 Picha ya pamoja baadhi ya waganga wakuu wa wilaya na mikoa wakiwa na Mgeni rasmi , Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia.
 Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia akikambishi zawadi ya saa ya ukutani Mganga Mkuu wa Serikali,Dk Donan Mmbando,saa hiyo iliyolewa na Taasisi ya Lab Eguip Limited.
 Baadhi ya waganga wakuu wa wilaya na Mikoa ya Tanzania Bara wakisiliza hotuba ya Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia ( hayupo pichani).
 Dk Frida Mokiti ( kushoto) akibadilishana mawazo na mwezake wakati wa mapumziko
Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando , baada ya waziri kufungua mkutano.

Na John Nditi, Morogoro
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Hawa Ghasia, amewaagiza  Waganga Wakuu wa Mikoa , na Halmashauri za wilaya nchini kuongeza zaidi kiwango cha kuchukua tahadhari katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa Ebola.
Waziri Ghasia alitoa agizo hilo jana mjini hapa wakati wa  hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Waganga wakuu wa mikoa, Halmashauri za wilaya na wakurugenzi wa Hospitali za rufaa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.
Kwa mujibu wa Waziri huyo kuwa, hapa nchini ugonjwa huo  haujathibitika kuingia na Serikali imechukua tahadhari zote kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hauingii  nchini na endapo utathibikika kuingia uweze kudhibitiwa kikamilifu.
Hata hivyo alisema , mwaka huu kumekuwepo na matukio ya hapa nchini na nje ya nchi yaliyotufanya tuongeze zaidi kiwango cha tahadhari , na tukio la kwanza ni la mlipuko wa ugonjwa wa Dengue , ambao uliwapata wagonjwa 1,384 kote nchini, na kusababisha vifo vya watu wanne , sehemu kubwa ya wagonjwa walikuwa ni wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri huyo , tukio la pili ni la ugonjwa wa ebola ,ambao kwanza ulianzia nchi za Afrika Magharibi,  na kati ya Machi hadi Agosti mwaka huu , watu 3,069 waliungua ugonjwa huo.
Hivyo  hadi kufikia Agosti 28, mwaka huu ,ugonjwa huo umeua watu 1,552 na hivi karibuni umeingia nchi ya Congo DRC na kufikia mwishoni mwa mwezi uliopita watu 24 wameripitiwa kuugua .
“ Ni matumaini yangu kuwa katika mkutano huu  , suala la magonjwa ya mlipuko kama haya yatajadilikwa kikamilifu ili kila mmoja wenu awe katika tahadhari kubwa” alisisitiza Waziri Ghasia
Hata hivyo , Waziri Ghasia alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za Serikali ya Tanzania kwa Watu wa Marekani kupitia Shirika lao la CDC na Shirika la Afya Duniani kwa kutoa vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo wa ebola.
Mbali na tahadhari ya magonjwa ya mlipuko, Waziri Ghasia alisema , katika ziara zake sehemu mbalimbali hapa nchini ameshuhudia juhudi zinazofanywa na wadau katika kuboresha upatikanaji  na utoaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii.
Kwa mujibu wa Waziri huyo kuwa juhudi hizo ni  kujenga vituo vipya vya huduma za afya , kukarabatiwa vituo ambavyo havipo katika hali nzuri  kuongeza watumishi na upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na kuimalisha utaratibu wa kukusanya mapato katika vituo.
Pia ulimalishaji wa utoaji wa huduma kwa makundi maalumu hususan , wanawake wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na  wazee  katika baadhi ya maeneo husika.
Hata hivyo alisema ,kutokana na juhudi hizo, malalamiko kuhusu uhaba wa dawa na vitendo vya rushwa yamepungua katika maeneo ambako juhudi hizo zimekwishafanyika.
“ Nimefurahishwa  na kasi ya ujenzi mpya wa Zahanati na Vituo vya Afya .... juhudi hizi zinapaswa kupongezwa  kwa vile ni utekeleaji wa Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)” alisema Waziri Ghasia .
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali , Dk Donan Mmbando, kabla ya kumkaribisha waziri , alisema lengo la mkutano huo ni kujadili masuala muhimu yanayolenga kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii hapa nchini na pia kuainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa wizara hiyo.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wataalamu hao wa sekta ya afya kujipanga kukabiliana magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa ebola na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kutolea huduma endapo kutakuwa na udhibitisho wa dalili za wagonjwa katika maeneo yao.
Pamoja na kuzungumzia changamoto zilizopo ikiwemo ya ya  usimamizi wa utendaji bora na uboreshaji wa  mazingira ya kazi na y a watumishi , pia aliwataka wataalamu wao kuangalia namna ya kukabiliana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo wa saratani.
Kwa mujibu wa Manga Mkuu wa Serikali, kuwa vituo vingi vya Afya vilijengwa kwa kuangalia upande mmoja wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na kusahau mengine yasiyoambukizwa na kwamba hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana nayo na kutaka yaingizwe kwenye mpango kazi wa mwaka 2016.

photo , ,