Moja ya mambo ambayo kijana wa leo anaweza kujivunia ni namna anavyoweza kushiriki kikamilifu katika mambo ya siasa. ni vema tukakumbuka kuwa hata mwasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Nyerere wakati wa harakati za kudai uhuru yeye pamoja na wapigania uhuru wengi wa afrika walikuwa bado vijana, wenye nguvu na hali ya pekee katika kupigania haki za wanyonge.
Kama vijana hawashiriki kikamilifu katika mambo ya siasa, siku moja watakuja kujikuta wametawaliwa na mtu wa Hovyo, mpumbavu na mwendawazimu, nchi zote zilizo huru duniani viongozi wake huchaguliwa kupitia michakato ya kisiasa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne navyo ni ardhi,watu, siasa safi na uongozi bora.
Ni vema tukatambua pia kuwa siasa sio chafu kwa asili yake bali kuna viongozi wachafu ndani ya siasa, hawa ndio wanaoichafua taswira nzuri ya siasa
hivyo basi......Ukiona vijana kama akina Mnyika, Tundu Lisu, Halima Mdee, David Silindi, Kafulila,Joshua Nassari na wengineo wengi wanapigania haki za wanyonge, usipowaunga mkono,ukiwapinnga sasa, nawe ukiwa mzee utapingwa pia
0 Responses so far.
Post a Comment