Mwanzoni mwa miaka ya tisini, chama cha mapinduzi kilianzisha mradi mchafu wa kisiasa kilipobaini uwezekano wa kusombwa na kimbunga cha uchaguzi. Kiliogopa kukataliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa mwaka 1995. Katika kutimiza malengo hayo, chama cha mapinduzi kilitafuta wataalam wa propaganda ili wabuni mradi wa hofu. Wakaeneza uzushi eti vyama vingi husababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.


Chama cha mapinduzi kikajaza watu hofu ya kupoteza maisha, kukatwa viungo, kupoteza ndugu na jamaa kwa vita iwapo watachagua upinzani. Walitoa sababu nyingi za kutochagua upinzani kwa kuinganisha na mauaji ya Rwanda, Burundi, sudan na Somalia.


Vyombo vya habari, hasa vya elektroniki vikasambaza hofu kwa kuonyesha picha za mauaji ya Rwanda na Burundi vikiwa na lengo la kuhujumu ustawi wa demokrasia na vyama vingi. Na  Kwakuwa wakati vyama vingi vikianzishwa watu wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha juu ya mfumo wa siasa za vyama vingi, wengi wakalaani mfumo wa vyama vingi bila kujua kuwa vilianzishwa kikatiba


Walianza kuvuana magamba wenyewe kwa wenyewe wakasahau kuwa Kuvuana magamba kwa sasa ni sawa na kitendo cha kuweka maua mazuri juu ya kaburi la zamani. Maua hayo hayasaidii chochote kwa marehemu zaidi ya kufurahisha macho ya watu wengine wanaolitazama kaburi kwa nje.

Kwa wale watakaokumbuka, wakati ule chama cha wananchi CUF kilipokuwa ni chama kikuu cha Upinzani CCM walipandikiza chuki kwa propaganda kuwa CUF ni chama cha waislam hivyo kwa kiasi kikubwa wakafanikiwa kuigawa CUF na wakristo. Miaka michache baadae Chama Cha Demokrasia na maendeleo baada ya kuonekana kukubalika sana miongoni mwa watanzania CCM wakaja na propaganda ile ile waliyoitumia kwa CUF kwa kuiunganisha CHADEMA na ukristo na ukabila, ingawa propaganda hii haijawa na mashiko miongoni mwa watanzania wa leo lakini wapo baadhi ya watu ambao bado hawaelewi kama huo ni mchezo mchafu wa CCM................
(Maelezo haya yameelezwa kwa kirefu ndani ya kitabu changu cha shukrani)
  

photo ,

0 Responses so far.